Scripture Stories
Ishmaeli na Familia Yake


“Ishmaeli na Familia Yake,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)

1 Nefi 7

Ishmaeli na Familia Yake

Kujiunga na safari ya kwenda nchi ya ahadi.

Picha
Nefi, na kaka zake, wakitembea kuelekea linakozama jua karibu na mto

Familia ya Lehi na Saria iliishi peke yake nyikani. Siku moja Bwana alimwambia Lehi kuwatuma wanawe, Lamani, Lemueli, Samu na Nefi kwenda Yerusalemu. Walitumwa kumwomba Ishmaeli na familia yake kuuungana nao. Pamoja familia zao zingeweza kulea watoto katika nchi ya ahadi.

1 Nefi 7:1–3

Picha
Nefi akizungumza na familia ya Ishmaeli

Ishmaeli na familia yake walitaka kumfuata Bwana. Waliamini Bwana aliwataka wajiunge na familia ya Lehi na Saria. Walichagua kuondoka Yerusalemu na kukutana na Lehi nyikani.

1 Nefi 7:4–5

Picha
Lamani na Lemueli wakiongea

Wakiwa kwenye njia yao, baadhi ya watu hawakutaka tena kutii. Walitaka kurudi nyumbani. Nefi aliwaomba kuwa na imani katika Bwana.

1 Nefi 7:6–13

Picha
Nefi akiwa amefungwa kwenye mti

Nefi alisema Bwana angeweza kufanya cho chote kama wangekuwa na imani. Lakini Lamani na Lemueli walikuwa na hasira kali. Walimfunga Nefi na walitaka kumwacha nyikani.

1 Nefi 7:12, 16

Picha
Binti wa Ishmaeli anamlinda Nefi

Nefi akisali kwa ajili ya msaada. Kamba zikalegea, na Nefi akasimama wima. Lakini Lamani na Lemueli bado walitaka kumuumiza. Mmoja wa mabinti wa Ishmaeli alimlinda Nefi. Mama yake na mmoja wa kaka zake pia walimlinda. Lamani na Lemueli waliwasikiliza na wakaacha kujaribu kumuumiza Nefi.

1 Nefi 7:17–19

Picha
Lamani na Lemueli wakipiga magoti mbele ya Nefi

Lamani na Lemueli.walisikitika kuhusu kile walichokuwa wamekifanya. Walimwomba Nefi awasamehe. Nefi aliwasamehe kaka zake. Kisha Lamani na Lamueli walisali na kumwomba Bwana kuwasamehe.

1 Nefi 7:20–21

Picha
Lehi na Ishmaeli wakitazama familia zao

Wao wote waliendelea na safari yao na kufika kwenye hema la Lehi na Saria. Hatimaye, familia hizo mbili zilikuwa pamoja. Walimshukuru Bwana na walimwabudu Yeye.

1 Nefi 7:21–22

Chapisha