Scripture Stories
Merikebu Kwa Kuvukia Bahari


“Merikebu Kwa Kuvukia Bahari,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)

“Merikebu Kwa Kuvukia Bahari.” Hadithi za Kitabu cha Mormoni

1 Nefi 17–18

Merikebu ya Kuvuka Bahari

Kujitayarisha kwenda nchi ya ahadi

Picha
familia zikiwa pembeni mwa bahari

Neema ilikuwa nchi iliyojaa matunda na asali. Palikuwa mahali pazuri pa kuishi. Familia ya Lehi na Saria iliishi karibu na bahari na walikuwa na kila kitu walichohitaji.

1 Nefi 17:5–6

Picha
Nefi akisali

Baada ya siku nyingi, Bwana alimwambia Nefi kwenda mlimani kusali. Kule, Bwana alimwambia kujenga merikebu itakayobeba familia yake kuvuka bahari.

1 Nefi 17:7–8

Picha
Nefi akiangalia mawe

Bwana alimwonyesha jinsi ya kujenga merikebu. Lakini Nefi hakujua wapi atapata chuma ya kutengenezea zana. Bwana alimwonyesha Nefi wapi pa kutafuta chuma.

1 Nefi 17:8–10

Picha
Nefi akifanya kazi wakati Lamani na Lemueli wakizungumza

Baadae, Nefi aliwasha moto ili kutengeneza zana. Lamani na Lemueli walimwangalia kaka yao mdogo Nefi. Hawakutaka kumsaidia kujenga merikebu. Walifikiri lilikuwa wazo baya la kujaribu kuvuka bahari.

1 Nefi 5:11, 16–18

Picha
Lamani na Lemueli wakiwa wamemkasirikia sana Nefi

Lamani na Lemueli hawakuamini kwamba Bwana alimwambia Nefi ajenge merikebu. Nefi aliwauliza kwa nini bado hawakuwa na imani katika Bwana. Aliwakumbusha kaka zake kwamba wamemwona malaika na kujua juu ya nguvu za Bwana. Lamani na Lemueli wakawa na hasira mno kiasi kwamba walitaka kumwua Nefi.

1 Nefi 5:18–19; 45–48

Picha
Lamani na Lemueli wakiwa ardhini

Lakini Nefi alikuwa amejawa na nguvu za Mungu. Nefi aliwaonya Lamani na Lemueli wasimguse. Waliogopa na hawakuthubutu kumgusa Nefi kwa siku nyingi. Kisha Bwana akamwambia Nefi aunyooshe mkono wake kwa kaka zake. Nefi alipowanyooshea mkono wake, walihisi kutikiswa na nguvu za Bwana.

1 Nefi 17:48, 52–55

Picha
kila mmoja akifanya kazi kwenye merikebu

Lamani na Lemueli walimwabudu Bwana na wakamsaidia Nefi kujenga merikebu. Nefi aliomba kwa Bwana mara nyingi kwa ajili ya msaada. Merikebu ambayo familia ya Nefi iliijenga ilikuwa nzuri sana. Baada ya siku nyingi, merikebu ilimalizika, na waiona kwamba ilikuwa nzuri. Familia ya Nefi walijua kwamba Bwana alikuwa amewasaidia.

1 Nefi 18:1–4

Chapisha