Scripture Stories
Mti wa Uzima


“Mti wa Uzima,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)

“Mti wa Uzima,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni

1 Nefi 8

Mti wa Uzima

Ndoto ya Lehi yenye mwongozo wa kiungu

Picha
Lehi akiongea na familia yake

Usiku mmoja, Lehi alipata ndoto kutoka kwa Bwana. Aliwaambia familia yake kuhusu ndoto hiyo.

1 Nefi 8:2–4

Picha
malaika akizungumza na Lehi

Katika ndoto yake, Lehi alimwona mtu akiwa katika joho jeupe. Mtu yule almwambia Lehi amfuate.

1 Nefi 8:5–6

Picha
Lehi gizani

Lehi aliona kwamba alikuwa gizani na mahali palipo wazi. Walitembea kwa masaa mengi. Lakini giza halikutoka. Hatimaye, Nefi alisali kwa ajili ya msaada.

1 Nefi 8:7–8

Picha
Lehi akiangalia mti wenye tunda

Lehi alipomaliza kusali aliona uwanja mkubwa. Katika uwanja ule kulikuwa na mti wenye tunda jeupe. Lehi alifikiri tunda lile litamfanya awe na furaha, kwa hiyo akala lile tunda. Nafsi yake ilijawa na furaha.

1 Nefi 8:9–12

Picha
Lehi akila tunda wakati Saria, Samu, na Nefi wakisimama karibu na mto

Tunda lilikuwa na ladha mzuri zaidi kuliko tunda lingine lolote. Lilikuwa tamu na la kupendeza sana. Lehi alitaka kushiriki tunda lile na familia yake. Alijua litawafanya pia wawe na furaha. Lehi aliwaona Saria, Samu, na Nefi wakisimama karibu na mto. Walionekana wamepotea. Lehi aliwaita kwa sauti kubwa. Aliwaomba waje na kula tunda.

1 Nefi 8:11–15

Picha
Lamani na Lemueli wakiondoka

Saria, Samu, na Nefi walikuja kwenye mti na walikula lile tunda. Lehi, aliwatafuta Lamani na Lemueli. Aliwataka nao pia wafurahie lile tunda. Lakini hawakutaka kuja kula tunda.

1 Nefi 8:16–18

Picha
watu wakija kwenye mti

Kisha Lehi aliona njia pamoja na fimbo ya chuma ambayo iliongoza kwenye mti. Aliwaona watu wengi wakitembea kwenye njia ile. Ghafla, giza nzito likaja. Giza lilifanya iwe vigumu kuona. Njia ya pekee kufika kwenye mti ilikuwa kushikilia kwenye fimbo ya chuma.

1 Nefi 8:19–24

Picha
mkono ukishikilia fimbo

Baadhi ya watu waliacha njia na kupotea. Wengine walishikilia kwa nguvu fimbo ya chuma na wakasonga.mbele.

1 Nefi 8:23–24

Picha
mwanamke akila tunda

Walipofika kwenye mti, walikula tunda.

1 Nefi 8:24

Picha
mti, mto, na jengo kubwa

Lehi alitazama juu na aliona jengo kubwa lililojazwa na watu wengi. Waliwafanyia mzaha watu waliokula tunda. Baadhi ya wale ambao walikula tunda walijsikia vibaya wakati wengine wakiwacheka, kwa hiyo waliondoka kwenye ule mti Walizurura mbali na wakapotea.

1 Nefi 8:25–28; 31–32

Picha
watu kwenye mti

Katika ndoto yake, Lehi aliona watu zaidi walioshikilia kwa nguvu fimbo ya chuma. Walisonga mbele hatua kwa hatua mpaka walipofika kwenye mti. Kisha walipiga magoti kwenye mti na wakala tunda. Hawakuwasikiliza watu katika lile jengo. Walichagua kubaki kwenye mti.

1 Nefi 8:30, 33

Picha
Lehi akiongea na familia yake

Lehi alipoamka, alikuwa na wasiwasi kuhusu Lamani na Lemueli. Katika ndoto yake wao hawakula tunda. Lehi aliwapenda Lamani na Lemueli. Alitumaini watabaki karibu na Bwana. Aliwaalika kutii amri za Mungu.

1 Nefi 8:36–38

Chapisha