Scripture Stories
Makao Mapya Katika Nchi ya Ahadi


“Makao Mapya Katika Nchi ya Ahadi,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)

“Makao Mapya Katika Nchi ya Ahadi,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni

2 Nefi 4–5

Makao Mapya Katika Nchi ya Ahadi

Wanefi na Walamani

Picha
familia ikimzunguka Lehi

Familia ya Lehi na Saria iliendelea kukua katika nchi ya ahadi. Watoto wao wakawa na watoto wao wenyewe. Lehi alikuwa akizeeka. Kabla hajafa, alitoa baraka kwa watu katika familia yake. Aliwaambia kwamba watakapotii amri za Mungu, Bwana angewasaidia.

2 Nefi 4:3–12

Picha
Lamani na Lemueli wakimwangalia Nefi

Baada ya Lehi kufa, Nefi aliwaongoza watu. Aliwaambia wamtii Bwana. Lamani na Lemueli walikuwa na hasira mno. Walitaka kumuua Nefi ili waweze kuongoza badala yake.

2 Nefi 4:13; 5:1–4

Picha
kundi la watu wakisafiri

Bwana alimwamuru Nefi kuondoka na familia yake na mtu mwingine ye yote aliyetaka kumfuata Bwana. Walisafiri kwa siku nyingi na kupata eneo jipya la kuishi.

2 Nefi 5:1, 5–8

Picha
watu wanalima

Wale waliokwenda na Nefi waliitwa Wanefi, na wale waliobaki waliitwa Walamani. Wanefi walimwomba Nefi awaongoze Walifanya kazi kwa bidii. Walilima, walifuga wanyama, na kujenga hekalu na majengo mengine. Makuhani na waalimu waliwafundisha kuhusu Bwana na watu walikuwa na furaha.

2 Nefi 5:9–11, 13–17, 26–27

Chapisha