Hadithi za Maandiko
Koriantoni


“Koriantoni,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)

Alma 39–42

Koriantoni

Kumgeukia tena Bwana

Koriantoni akiwafundisha watu

Koriantoni alikuwa mmoja wa wana wa Alma. Alikwenda na baba yake, kaka yake Shibloni, na wengine kufundisha kikundi cha watu walioitwa Wazoramu kuhusu injili ya Yesu Kristo.

Alma 31:5–7; 32:1

Koriantoni akinywa na watu

Koriantoni alipokuwa na watu, alijaribiwa kutenda dhambi. Badala ya kumtii Bwana, alichagua kufanya mambo ambayo yalikuwa kinyume na amri za Mungu Kwa sababu ya kile alichofanya, baadhi ya Wazoramu hawakuamini kile Alma na wanawe walichofundisha.

Alma 39:2–5, 11–12

Alma akiongea na Koriantoni

Alma alimwalika Koriantoni atubu na kumgeukia Bwana kwa ajili ya msamaha. Koriantoni alikuwa na wasiwasi kuhusu sehemu za mpango wa Bwana. Alma alimsaidia mwanawe kuelewa mpango wa Bwana wa furaha, Upatanisho wa Kristo, ufufuko, na maisha baada ya kifo. Alma alimkumbusha kwamba Bwana alikuwa na kazi kwa ajili yake kuifanya.

Alma 39:7–9, 13–19; 40–42

Koriantoni akiwafundisha watu

Koriantoni alimsikiliza baba yake. Alikuwa na imani katika Yesu na alitubu dhambi zake. Alijifunza kwamba Bwana alikuwa mwenye haki na pia mwenye upendo na mpole. Koriantoni alifundisha tena pamoja na baba na kaka yake. Waliwafundisha watu wengi kuhusu furaha na amani ya toba na ya kuishi Injili ya Yesu Kristo.

Alma 42:30–31; 43:1–2; 48:17–18