“Waanti‑NefiLehi,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)
Waanti‑NefiLehi
Watu ambao walichagua kuwapenda maadui zao
Walamani wengi walijifunza kuhusu Mungu kutoka kwa Amoni na kaka zake. Walamani hawa walikuwa na imani imara katika Bwana na walifuata amri za Mungu. Wao walitaka jina jipya, kwa hiyo walijiita Waanti-Nefi Lehi badala ya Walamani.
Waanti‑NefiLehi walibadilika kwa sababu ya imani yao katika Mungu. Walitubu mambo mabaya waliyokuwa wamezoea kufanya. Walijua Mungu aliwapenda na amewasamehe.
Walamani walikasirika sana na wallijiandaa kuwashambulia Waanti-Nefi-Lehi. Badala ya kupigana, Waanti‑NefiLehi waliweka ahadi na Mungu. Walisema kamwe hawangewaumiza watu tena. Kwa kuonyesha hili, walizika silaha zao. Wao walichagua kuwapenda maadui zao badala ya kuwaumiza au kuwaua.
Walamani ambao hawakuamini katika Mungu waliwashambulia Waanti-Nefi-Lehi.
Waanti-Nefi Lehi walikuwa na imani kwamba kama wangeuawa, wangeishi tena na Mungu. Walishika ahadi yao na Mungu na hawakupigana na wale Walamani.
Badala ya kupigana, Waanti-Nefi Lehi walisali. Wakati Walamani walipoona hili, wengi wao waliacha kuwashambulia. Walijisikia vibaya kuwaua watu. Walamani hao pia walichagua kamwe kutowaumiza watu tena. Walijiunga na Waanti-Nefi Lehi.
Kadiri muda ulivyosonga, watu zaidi walishambulia. Amoni na kaka zake walihuzunika Waanti-Nefi Lehi walikuwa wanateseka. Walimuomba mfalme awapeleke watu wake kuishi na Wanefi. Mfalme alisema wangeenda kama Bwana aliwataka wao wafanye hivyo. Amoni alisali. Bwana alisema wanapaswa kwenda na kwamba Yeye atawalinda wawe salama.
Wanefi waliwapa Waanti-Nefi Lehi ardhi ya kuishi na kuwalinda. Kama shukrani, Waanti-Nefi Lehi waliwapa Wanefi chakula. Waanti-Nefi Lehi walikuwa na imani kuu na walimpenda Mungu. Walikuwa waaminifu kwa kila mmoja na walishika ahadi yao kamwe wasipigane. Walikuwa waaminifu maisha yao yote.