Scripture Stories
Yakobo na Sheremu


“Yakobo na Sheremu,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)

Yakobo 7

Yakobo na Sheremu

Ushuhuda wa nabii juu ya Yesu Kristo

Picha
Yakobo akiwafundisha watoto

Yakobo alikuwa nabii aliyemwona Yesu.Kristo. Aliwataka watu kuamini katika Kristo. Yakobo aliwafundisha watu kutii amri za Mungu. Alifanya kazi kwa bidii ili kuwafundisha watu kuhusu Yesu.

2 Nefi 11:2–3; Yakobo 1:1–8, 17–19

Picha
Sheremu akiongea na watu

Siku moja, mtu aliyeitwa Sheremu alianza kuwafundisha watu. Lakini Sheremu alifundisha kwamba Yesu hayupo. Sheremu alikuwa mzungumzaji mzuri, na Wanefi wengi waliamini kile alichosema. Kwa sababu yake, watu wengi waliacha kuamini katika Yesu. Sheremu pia alimtaka Yakobo kuacha kuamini katika Yesu.

Yakobo 7:1–5

Picha
Sheremu akiongea na kumnyoshea kidole Yakobo

Sheremu alisema hakuna mtu ambaye angeweza kujua nini kitatokea hapo baadaye. Alisema hii ilimaanisha hakuna hata mmoja ambaye angeweza kujua kama Yesu yupo, kwa sababu Yesu hajaja bado duniani. Lakini Yakobo alisema maandiko na manabii wote walifundisha kuhusu Yesu. Mungu alikuwa amemwonesha Yakobo kwamba Yesu atakuja duniani.

Yakobo 7:6–12

Picha
Sheremu akiongea na akikenua meno

Sheremu bado hakuweza kuamini. Alimtaka Yakobo kumwonesha ishara kwamba kweli kuna Yesu

Yakobo 7:13

Picha
Yakobo akiinua mkono wake.

Yakobo alisema Sheremu alijua kwamba Yesu atakuja na hakuhitaji ishara. Lakini Yakobo alisema Mungu atamfanya Sheremu azirai ili kuonesha kwamba Mungu ana nguvu na kwamba kweli Yesu yupo.

Yakobo 7:14

Picha
Sheremu akiangukia magoti yake na watu wakiwa karibu naye

Ghafula, Sheremu akawa mgonjwa na akaanguka chini. Baada ya siku nyingi, alijua alikuwa anakufa. Aliwambia watu kwamba alikuwa amedanganywa na Shetani. Alisema alikuwa amedanganya kwa Mungu. Alijua wakati wote kwamba Yesu kweli yupo Kisha Sheremu alikufa. Watu walisoma maandiko na waliamini katika Yesu.

Yakobo 7:15–23

Chapisha