“Teankumu,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)
Teankumu
Kuwalinda watu Wake
Teankumu alikuwa kiongozi katika jeshi la Kapteni Moroni. Alikuwa anajaribu kuiweka miji ya Wanefi kuwa salama dhidi ya Walamani.
Amalikia alikuwa Mnefi ambaye alikuja kuwa mfalme wa Walamani. Yeye alitaka pia kuwatawala Wanefi. Alitaka kuwashambulia Wanefi na kutwaa miji mingi.
Alma 47:1, 35; 48:1–4; 51:23–28
Jeshi la Teankumu lilienda kuzuia jeshi la Amalikia lisishambulie miji ya Wanefi.
Majeshi yalipigana kwa siku nzima. Teankumu na jeshi lake walipigana kwa nguvu na ujuzi zaidi kuliko jeshi la Amalikia. Lakini hakuna jeshi lililoshinda. Wakati giza lilipoingia, majeshi yote yaliacha kupigana ili kwamba wangeweza kupumzika.
Alma 51:31—32
Lakini Teankumu hakupumzika. Yeye na watumishi wake kwa siri walienda kwenye kambi ya Amalikia.
Teankumu alinyemelea hadi ndani ya hema la Amalikia. Alimuua Amalikia kabla ya Amalikia hajaweza kuamka. Kisha Teankumu alienda kwenye kambi yake na kuwaambia askari wake wawe tayari kwa ajili ya kupigana.
Wakati Walamani walipoamka, waligundua kwamba Amalikia alikuwa amekufa. Waliona pia kwamba Teankumu na jeshi lake walikuwa tayari kupigana nao.
Walamani waliogopa na wakakimbilia. Mpango wa Teankumu ulikuwa umewafanya Walamani kuwa na uoga sana kushambulia miji zaidi ya Wanefi. Teankumu sasa alikuwa na muda wa kuifanya miji ya Wanefi kuwa salama. Alifanya bidii kuwalinda watu wake. Aliweza kuiweka miji mingi ya Wanefi kuwa salama.