Scripture Stories
Kurudi Yerusalemu


“Kurudi Yerusalemu,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)

“Kurudi Yerusalemu,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni

1 Nefi 3

Kurudi Yerusalemu

Safari kwa ajili ya mabamba ya shaba

Picha
familia ikijenga hema

Familia ya Lehi na Saria ilisafiri nyikani. Katika ndoto, Bwana alimwambia Lehi kuhusu maandiko kwenye mabamba ya shaba. Mtu aliyeitwa Labani alikuwa nayo huko Yerusalemu. Bwana alisema familia ya Lehi ilihitaji kuchukua mabamba ya shaba pamoja nao kwenye safari yao.

1 Nefi 3:1–3, 19–20

Picha
Lehi akiongea na familia yake

Bwana alimwambia Lehi kuwatuma wanawe kurudi Yerusalemu kuchukua hayo mabamba ya shaba. Kaka zake Nefi walilalamika. Walimwambia Lehi ilikuwa kazi ngumu kufanya. Hawakutaka kwenda.

1 Nefi 3:4–5

Picha
Saria, Lehi, na Nefi wakizungumza.

Ilikuwa kazi ngumu sana kufanya, lakini Nefi alitaka kutii. Alijua Bwana atamsaidia yeye na kaka zake. Nefi alimwambia Lehi kwamba atarudi Yerusalemu na kuchukua mabamba ya shaba.

1 Nefi 3:6–8

Picha
akina kaka karibu na Yerusalemu.

Lamani, Lemueli, Samu na Nefi walirudi Yerusalemu. Walipofika kule, waliamua kwamba Lamani atakwenda nyumbani kwa Labani na kuomba mabamba hayo ya shaba.

1 Nefi 3:9–11

Picha
Labani na Lamani

Lamani alipoomba mabamba ya shaba, Labani alimwita mnyag’anyi. Alisema angemuua Lamani.

1 Nefi 3:11–13

Picha
Lamani akiwakimbia walinzi

Lamani alikimbia na aliwaambia ndugu zake nini kilichotokea.

1 Nefi 3:14

Picha
Nefi akiongea na kaka zake

Kaka wote wanne walihuzunika. Lamani, Lemueli, na Samu walitaka kurudi nyumbani kwa wazazi wao huko nyikani, lakini Nefi alikuwa na wazo. Alisema wangeweza kufanya biashara na Labani ili kupata yale mabamba ya shaba. Walirudi nyumbani kwao jijini na kuchukuwa dhahabu yao yote na fedha ili kufanyia biashara.

1 Nefi 3:14–16; 22–24

Picha
akina kaka wakiwakimbia walinzi

Walipoonyesha dhahabu na fedha kwa Labani, yeye alitaka vyote. Lakini bado hakutaka kuwapa hayo mabamba ya shaba. Badala yake, aliwaambia watumishi wake kuwaua wale kaka ili aweze kuchukua dhahabu na fedha zao

1 Nefi 3:16, 23–25

Picha
kaka wakijificha wasionekana na walinzi

Wale kaka wanne walikimbia kwa ajili ya maisha yao na waliacha dhahabu yao na fedha nyuma. Watumishi wa Labani hawakuweza kuwakamata. Wale kaka walijificha ndani ya pango.

1 Nefi 3:26–27

Picha
Lamani na Lemueli wakiwakasirikia Nefi na Samu

Baada ya mambo yote haya magumu, Lamani na Lemueli walimkasirikia sana Nefi. Waliwapiga Nefi na Samu kwa fimbo.

1 Nefi 3:28

Picha
malaika akizungumza na Lamani na Lemueli

Ghafla, malaika alikuja na kuuliza kwa nini walikuwa wanampiga Nefi. Malaika alisema kwamba Nefi alikuwa amechaguliwa kuwaongoza. Kisha malaika aliwaambia kurudi Yerusalemu. Bwana atatayarisha njia kwa ajili yao ili kupata mabamba ya shaba.

1 Nefi 3:29

Chapisha