Hadithi za Maandiko
Alma, Amuleki, na Zeezromu


“Alma, Amuleki na Zeezromu,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)

Alma 4–12

Alma, Amuleki na Zeezromu

Kuchagua kuamini na kumtii Mungu

Alma akishambuliwa na watu

Alma aliona kwamba waumini wengi wa Kanisa walikuwa hawatii amri za Mungu. Kwa hiyo Alma alikwenda kutoka mji hadi mji akifundisha neno la Mungu. Watu wengi walitubu. Kisha Alma alifika kwenye mji uliloitwa Amoniha. Watu pale hawakumsikiliza. Walimtemea mate na kumfukuza nje ya mji

Alma 4:11–20; 5–7; 8:1–13

malaika akizungumza na Alma

Alma alihisi huzuni alipokuwa anaondoka katika mji ule. Alikuwa na wasiwasi kwa ajili ya watu. Kisha malaika alikuja kwake. Malaika alisema kwamba Alma angeweza kuwa na furaha kwa sababu yeye alimtii Mungu. Malaika alimwambia Alma arudi kwenye mji ule na awaonye watu. Kama hawatatubu,wataangamizwa. Alma haraka alirudi.

Alma 8:14–18

Alma akizungumza na Amuleki

Alma aliporudi kwenye mji ule, alikuwa na njaa sana. Alikuwa amefunga kwa siku nyingi. Alma alimuomba chakula mtu aliyeitwa Amuleki.

Alma 8:19, 26

Amuleki akimwalika Alma aingie ndani

Amuleki alimwambia Alma kuhusu ono aliloliona. Katika ono, malaika alimwambia Amuleki kwamba Alma alikuwa nabii wa Mungu. Amuleki alitaka kumsaidia Alma.

Alma 8:20

Alma akiisalimia familia ya Amuleki

Amuleki alimkaribisha Alma nyumbani na akampa chakula ale. Alma alikaa nyumbani mwa Amuleki kwa siku nyingi. Mungu alimbariki Amuleki na familia yake. Baadaye, Mungu alimwambia Alma na Amuleki kuwaambia watu katika mji ule watubu. Alma na Amuleki walitii. Mungu aliwapa nguvu Yake ili kuwasaidia kufundisha.

Alma 8:21–32; 9–13

Zeezromu anatoa fedha

Mmoja wa watu ambaye aliwasikia wakifundisha aliitwa Zeezromu. Alikuwa mjanja sana na alitaka kuwalaghai Alma na Amuleki. Zeezromu alimwambia Amuleki atampa fedha nyingi kama angesema Mungu hayupo. Alimtaka Amuleki kudanganya ili kwamba watu wasiamini kile ambacho Amuleki na Alma walikifundisha.

Alma 10:29–32; 11:21–25; 12:4–6

Alma na Amuleki wakizungumza na Zeezromu

Lakini Amuleki hangeweza kudanganya kuhusu Mungu. Yeye alisema kweli Mungu yupo. Amuleki na Alma walijua mawazo ya Zeezromu. Zeezromu alishangazwa na aliwauliza maswali mengi. Walimfundisha Zeezromu kwamba Mungu ana mpango kwa ajili ya watu wote. Zeezromu aliamini kile ambacho Alma na Amuleki walifundisha kuhusu Mungu na Yesu Kristo

Alma 11:23–46; 12:1–18, 24–34; 14:6–7; 15:6–7

Zeezromu akitembea na Alma na Amuleki

Zeezromu alisikitika sana kwa mambo mabaya aliyofanya. Akawa mgonjwa. Alma na Amuleki walimtembelea. Alma alisema Zeezromu angeweza kuponywa kwa sababu ya imani ya Zeezromu katika Yesu. Alma alimwomba Mungu amponye. Zeezromu aliruka kwa miguu yake. Alikuwa ameponywa! Alibatizwa na aliwafundisha watu kwa muda wa maisha yake yote.

Alma 15:1–12; 31:6, 32