Scripture Stories
Nefi na Mabamba ya Shaba


“Nefi na Mabamba ya Shaba,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)

1 Nefi 4–5

Nefi anapata Mabamba ya Shaba

Kujifunza kumfuata Roho

Picha
Nefi akikaribia jengo na kaka zake wakiangalia

Lamani, Lemueli, Samu na Nefi walirudi Yerusalemu usiku. Nefi alikwenda nyumbani kwa Labani wakati kaka zake wakiwa wamejificha nje ya jiji.

1 Nefi 4:4–5

Picha
Nefi akimwangalia Labani chini adhini.

Nefi alimruhusu Roho amuongoze. Hakujua alipaswa kufanya nini, lakini alijua Bwana atamsaidia kupata mabamba ya shaba.

1 Nefi 4:6

Picha
Nefi akishikilia upanga wa Labani

Lehi alipokaribia nyumba ya Labani alimkuta Labani akiwa chini ardhini. Labani alikuwa amelewa. Nefi aliuona upanga wa Labani na kuuchukua.

1 Nefi 4:7–9

Picha
Nefi akiondoka kutoka kwa Labani

Nefi alipoangalia upanga, Roho alimwambia amwue Labani. Lakini Nefi hakutaka kumuua. Roho alimwambia Nefi kwamba ilikuwa vyema kwa Labani kufa kuliko kwa familia ya Nefi kutokuwa na maandiko. Walihitaji amri za Mungu ambazo ziliandikwa kwenye mabamba ya shaba.

1 Nefi 4:10–11, 13–17

Picha
Nefi akisali

Nefi alijua kwamba Labani alikuwa amejaribu kumuua. Labani pia aliwahi kuiba mali zao na hangetii amri za Mungu.

1 Nefi 4:11

Picha
Nefi akiwa amevaa mavazi ya Labani

Roho akamwambia Nefi tena amwue Labani. Nefi alijua Bwana ametayarisha njia kwa ajili yake kuyapata mabamba ya shaba. Alichagua kumtii Roho. Nefi alimwua Labani na kuvaa mavazi ya Labani.

1 Nefi 4:12–13, 17–19

Picha
Nefi akizungumza na Zoramu

Nefi kisha alikwenda kwenye hazina ya Labani na alimkuta mtumishi wa Labani Zoramu. Nefi aliigiza na alisema kama Labani.

1 Nefi 4:20–23; 35

Picha
Zoramu akishikilia mabamba ya shaba

Nefi alimwambia Zoramu alihitaji mabamba ya shaba. Kisha Nefi alimwambia Zoramu amfuate. Zoramu alifikiri Nefi alikuwa Labani, hivyo alifanya kile Nefi alichotaka.

1 Nefi 4:24–26

Picha
kaka zake wanamkimbia Nefi

Nefi na Zoramu walipotoka nje ya jiji, Lamani, Lemueli, na Samu walifikiri Nefi alikuwa Labani. Waliogopa na walianza kukimbia.

1 Nefi 4:28

Picha
kaka zake wanaongea na Zoramu anaangalia nyuma

Nefi aliwaita kaka zake. Walipojua alikuwa Nefi waliacha kukimbia. Lakini kisha Zoramu akawa mwoga na alijaribu kurudi Yerusalemu.

1 Nefi 4:29–30

Picha
Nefi akionge na Zoramu

Nefi alimsimamisha Zoramu Alimwambia Zoramu kwamba Bwana amewaamuru kuchukua mabamba. Alimtaka Zoranu kwenda pamoja nao kwenye nchi ya ahadi. Zoramu alijua kwamba angeweza kuwa mtu huru, sio mtumishi, na aliahidi kwenda pamoja na Nefi na familia yake.

1 Nefi 4:31–37

Picha
Nefi, kaka zake, na Zoramu wakiwaamkia Saria na Lehi

Walisafiri kurudi kwa Lehi na Saria. Lehi na Saria walifurahi sana kuwaona wana wao. Saria alikuwa amefikiria wanawe walikuwa wamekufa. Kwa sababu Bwana alikuwa amewaweka wanawe salama, sasa aliamini kwamba familia yao imeamriwa kuondoka Yerusalemu. Familia ya Lehi na Saria.ilitoa dhabihu ili kumshukuru Bwana.

1 Nefi 4:38; 5:1–9

Picha
Lehi akisoma mabamba ya shaba pamoja na familia yake

Lehi akisoma mabamba ya shaba. Aliona kwamba mabamba yalikuwa na mafundisho ya manabii. Pia alijua kwamba mmoja wa mababu zake alikuwa Yusufu ambaye aliuzwa Misri na kaka zake zamani sana. Lehi alijua mabamba ya shaba yalikuwa ya muhimu sana. Alijua Bwana alitaka familia yake kuwa na hizo amri.

1 Nefi 5:10–22

Chapisha