Hadithi za Maandiko
Abinadi na Mfalme Nuhu


“Abinadi na Mfalme Nuhu,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)

Mosia 11–17

Abinadi na Mfalme Nuhu

Ujumbe kutoka kwa nabii

Mfalme Nuhu ananyoosha kidole wakati makuhani wawili wakisimama nyuma yake

Mfalme Nuhu aliwatawala Wanefi walioishi katika nchi ya Nefi. Nuhu aliwafanya watu wake kumpa yeye fedha nyingi mno na kisha alizitumia kwa kununua vitu vya anasa kwa ajili yake mwenyewe. Aliwaita makuhani waliokuwa na kiburi ili kumsaidia kutawala. Nuhu hakutii amri za Mungu. Badala yake, alifanya mambo mengi maovu.

Mosia 11:1–13

Mfalme Nuhu

Nuhu aliongoza watu wake kuwa waovu pia. Hawakumfuata Bwana.

Mosia 11:7, 11, 14–15, 19

Abinadi anawatazama watu wakifanya mambo mabaya

Nabii wa Mungu aliyeitwa Abinadi aliishi katika nchi ile. Bwana alimtuma Abinadi kumwambia Nuhu na watu wake watubu.

Mosia 11:20

Abinadi anazungumza na watu

Abinadi aliwaambia watu kwamba Bwana aliwataka wao watubu. Kama hawangetubu, Bwana angewaacha maadui kuja kwenye nchi na kuwatawala. Maadui zao wangefanya maisha yao kuwa magumu kwa Nuhu na watu wake.

Mosia 11:20–25

Watu waliokasirika

Watu walimkasirikia Abinadi kwa ajili ya kile alichosema. Walitaka kumuua, lakini Bwana alimweka Abinadi salama na alimsaidia kutoroka.

Mosia 11:26

Mfalme Nuhu anaweka viganja pamoja na anazungumza na makuhani

Nuhu alitaka kumuua Abinadi pia. Nuhu hakuamini katika Bwana. Yeye na watu wake hawakutubu.

Mosia 11:27–29

Abinadi anashikilia mabamba na kuzungumza na familia

Miaka miwili baadaye, Bwana alimtuma Abinadi arudi tena kuwaonya watu. Abinadi aliwaambia watu kwamba maadui zao wangetwaa nchi kwa sababu walikuwa hawajatubu. Watu walimkasirikia Abinadi. Walisema hawakufanya kosa lolote na hawangetubu. Walimfunga Abinadi na kumpeleka kwa Nuhu.

Mosia 12:1–16

Abinadi anapiga magoti wakati mgongo ukimwelekea Mfalme Nuhu

Nuhu na makuhani wake walikuja na mpango. Makuhani walijaribu kumtega Nuhu kwa kumuuliza maswali mengi. Lakini Abinadi kwa ujasiri aliyajibu. Makuhani walistajabishwa na majibu ya Abinadi. Wao hawangeweza kumtega Abinadi. Abinadi aliwaambia makuhani kwamba walijali sana kuhusu pesa kuliko kile kilicho sahihi.

Mosia 12:17–37

Abinadi anasimama na anang’ara

Nuhu aliwaambia makuhani wake kumuua Abinadi. Lakini Abinadi aliwaonya wasimguse. Uso wake uling’ara kwa nguvu za Mungu. Abinadi alisema makuhani hawakuwa wanafundisha amri za Mungu. Abinadi aliwafundisha kwamba Yesu Kristo angezaliwa, kufa kwa ajili yetu, na kufufuka. Alisema Yesu angewasamehe kama wangetubu.

Mosia 13; 16: 6–15

Abinadi akimtazama Mfalme Nuhu

Abinadi alihitimisha ujumbe ambao Bwana alikuwa amemtuma kuutoa. Nuhu bado alikuwa amekasirika. Aliwaambia makuhani wake wamtwae Abinadi na kumuua.

Mosia 17:1

Mfalme Nuhu anamtazama Abinadi wakati Alma anafikiria na makuhani wengine wakiwa na hasira.

Kuhani mmoja, Alma, alimwamini Abinadi. Alma alijaribu kumwokoa Abinadi. Lakini sasa Nuhu alimkasirikia Alma pia na kumlazimisha aondoke.

Mosia 17:2–3

Alma anajificha mbali na makuhani waovu

Makuhani walimwambia Abinadi kwamba angeishi kama angesema kwamba kile alichofundisha si kweli. Lakini Abinadi alisema alikuwa amefundisha ukweli. Nuhu na makuhani wake wakakasirika sana tena. Wakamfanya Abinadi afe kwa moto. Walinzi wa Nuhu walijaribu kumuua Alma pia. Lakini Alma alijificha na kuandika maneno ya Abinadi.

Mosia 17:3–13, 20