Hadithi za Maandiko
Jeshi la Vijana


“Jeshi la Vijana,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)

Alma 53; 56–57

Jeshi la Vijana

Wana ambao walimtumainia Mungu

askari vijana wanashikilia ngao, mikuki na panga

Wanefi walikuwa vitani na Walamani na walihitaji msaada. Waanti‑Nefi­Lehi walitaka kusaidia. Lakini walikuwa wameweka ahadi na Bwana kutopigana. Vijana wao wadogo elfu mbili walikuwa hawajafanya ahadi hiyo. Badala yake, wana hawa waliahidi kupigana ili kulinda familia zao. Wana hawa walikuwa wakiitwa askari vijana.

Alma 53:8, 13–18, 22; 56:1–8

Helamani anaongoza askari vijana kuelekea kwenye mji.

Askari vijana hawa walimchagua nabii Helamani kuwaongoza wao. Walikuwa kikundi kidogo kulinganisha na jeshi kubwa la Walamani. Lakini Helamani alijua askari hawa vijana walikuwa waaminifu, jasiri na wenye imani. Helamani akiwa anawaongoza, walienda kuwasaidia Wanefi.

Alma 53:19–22; 56:9–10, 17, 19

askari vijana wanajenga ngome pamoja na askari wa Wanefi, na wazazi wakileta chakula

Askari Wanefi walikuwa wamechoka. Lakini wakati askari vijana walipokuja, Wanefi walikuwa na furaha. Jeshi la vijana liliwapa tumaini na nguvu. Kwa pamoja, walienda kupigana na Walamani. Wazazi wa askari vijana pia walisaidia kwa kuleta chakula na vifaa kwao.

Alma 56:16–17, 19–20, 22, 27

Viongozi wa Wanefi na askari vijana wanakutana ndani ya hema

Walamani walikuwa wameteka miji mingi na kuweka majeshi yao kwenye miji hiyo. Viongozi Wanefi walitaka kuwaondoa Walamani kutoka kwenye mojawapo ya miji hii. Walifanya mipango na kuwaomba askari vijana msaada.

Alma 56:18–30

Jeshi la Walamani wakiwa na silaha linawakimbilia askari vijana

Askari vijana wanajifanya kubeba chakula kwa ajili ya Wanefi walioishi mji ulio karibu. Wakati Walamani walipoona kundi ndogo, waliacha mji wao na kuwafukuza askari vijana. Walamani walifikiri ingekuwa rahisi kuwateka.

Alma 56:30–36

askari vijana wanatembea katika mstari mrefu, jeshi la Walamani linawafuata, na jeshi la Wanefi linafuata nyuma ya jeshi la Walamani

Askari vijana wanawakimbia Walamani. Kisha jeshi la Wanefi linawakimbiza Walamani. Walamani wanataka kuwashika askari vijana kabla ya Wanefi kuwafikia. Wanefi waliona askari vijana walikuwa kwenye mtatizo na hivyo wakatembea upesi ili kuwasaidia.

Alma 56:36-41

askari kijana anatazama majeshi mengine na ana hofu

Baada ya muda fulani, askari vijana hawakuweza kuwaona Walamani. Walianza kujiuliza kama Wanefi walikuwa wamewafikia Walamani na walikuwa wanapigana.

Alma 56:42–43

Helamani anashikilia upanga wake

Helamani alikuwa na hofu. Alifikiria Walamani yawezekana wanajaribu kuwatia mtegoni. Aliwauliza askari wake vijana kama wangeenda kupigana na Walamani.

Alma 56:43–44

askari vijana wananyanyua panga zao

Askari vijana walikumbuka kile mama zao walikuwa wamewafundisha. Mama zao walikuwa wamewafundisha kumtumainia Mungu na kutokuwa na shaka, kwa sababu Yeye angewasaidia. Hawa wana waliamini katika Mungu na walitaka kutimiza ahadi yao ya kuzilinda familia zao. Walimwambia Helamani kwamba walikuwa tayari kwenda kupigana.

Alma 56:46–48

Helamani anatembea pamoja na askari vijana

Helamani alishangazwa na ujasiri wao. Aliwaongoza kurudi nyuma kupigana na Walamani.

Alma 56:45, 49

Helamani na askari vijana wanasimama kilimani wakiwa na silaha

Askari vijana waliwaona Walamani na Wanefi wakipigana. Wanefi walikuwa wamechoka. Walikuwa karibu kushindwa wakati askari vijana walipofika.

Alma 56:49–52

Askari Walamani wanaonekana kuogopa

Askari vijana walipigana kwa nguvu za Mungu. Walamani waliwaogopa na wakaacha kupigana. Askari vijana walikuwa wamesaidia kushinda mapigano yale!

Alma 56:52–54, 56

Helamani anawanyoshea mkono wale askari vijana

Katika mapigano haya, Wanefi na Walamani wengi walikufa. Helamani alikuwa na hofu kwamba baadhi ya askari wake vijana yawezekana kuwa walikufa pia. Lakini baada ya mapigano, Helamani alihesabu kila mmoja. Alikuwa na furaha sana kuona kwamba hakuna kati ya askari vijana aliyeuawa. Mungu alikuwa amewalinda.

Alma 56:55–56

askari vijana wamejeruhiwa na wote wanasimama pamoja

Wana zaidi walijiunga na askari vijana. Wao waliendelea kuwasaidia Wanefi kupigana. Katika haya mapigano mengine, askari vijana wote walijeruhiwa, lakini hakuna kati yao aliyekufa. Walikumbuka kile mama zao walikuwa wamewafundisha. Walimtumainia Mungu, na Yeye aliwalinda.

Alma 57:6, 19–27; 58:39–40