“Liahona na Upinde Uliovunjika,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)
Liahona na Upinde Uliovunjika
Kutafuta msaada wa Bwana
Familia za Lehi na Ishmaeli zilisafiri katika nyika kwa miaka mingi. Bwana aliwaongoza kupitia sehemu nzuri za nchi. Ilibidi wawinde na kukusanya chakula wakiwa njiani. Ilikuwa safari ngumu.
Bwana aliahidi kuziongoza familia kwenda kwenye nchi mzuri kama watashika amri. Hawakujua jinsi ya kuipata nchi ile, lakini Yeye angewaongoza.
Asubuhi moja, Lehi alishangazwa kuona mpira wa shaba nje ya hema lake. Mpira ule uliitwa Liahona. Ndani ya Liahona, mshale ulionesha njia ambayo kundi lile lilihitaji kusafiria. Wakati mwingine walipata jumbe kutoka kwa Bwana zilizoandikwa kwenye Liahona. Hivi ndivyo Bwana alivyowaongoza.
1 Nefi 16:10,16, 26–29; Alma 37:38
Siku moja Nefi alipokuwa anawinda upinde wake wa chuma cha pua ulivunjika. Familia zisingeweza kupata chakula bila upinde huo. Kaka zake Nefi walimkasirikia.yeye na Bwana.
Wote walikuwa wamechoka sana na wenye njaa. Baadhi yao walikuwa wenye huzuni na walilalamika. Walikuwa na hofu kwamba watakufa kwa njaa. Hata Lehi alilalamika kwa Bwana.
Nefi alitengeneza upinde mpya na mshale kutoka kwenye mbao. Alikuwa na imani kwamba Bwana atamsaidia kupata chakula.
Nefi alimwuliza Lehi wapi pa kwenda kuwinda. Lehi alisikitika kwamba alikuwa amelalamika. Alitubu na kumwomba Bwana kwa ajili ya msaada. Bwana alimwambia Lehi atazame Liahona. Ujumbe uliandikwa juu yake. Familia zilijifunza kwamba Liahona ilifanya kazi tu wakati wanapokuwa na imani katika Bwana na kutii amri.
Bwana wakati mwingine alibadilisha ujumbe kwenye Liahona ili kuwasaidia wakati wa safari zao. Liahona ilimsaidia Nefi kujua wapi pa kwenda kuwinda. Alirudi na chakula cha kuliwa, na wote walikuwa na furaha. Walitubu na walimshukuru Bwana.