Hadithi za Maandiko
Nabii Mormoni


“Nabii Mormoni,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)

Maneno ya Mormoni 1; Mormoni 1–8

Nabii Mormoni

Kuandika Kitabu cha Mormoni

watu wengi wakitengeneza silaha, na Mormoni kama mtoto pamoja na mama yake wanasimama karibu na meza iliyojaa panga

Mormoni alikuwa Mnefi aliyeamini katika Yesu Kristo. Alikulia katika wakati ambapo watu wengi hawakutii amri za Mungu. Watu walinyang’anyana na kuuana kwa sababu ya pesa na madaraka. Kulikuwa na vita vingi.

3 Nefi 5:12–13; 4 Nefi 1:27–49; Mormoni 1:1–3, 15, 18–19

Amaroni akizungumza na Mormoni na mama yake wakiwa wanavuna mazao, na watu wengi wakifanya kazi shambani karibu nao

Wakati Mormoni alipokuwa na miaka 10, mtu aliyeitwa Amaroni alimjia. Amaroni alitunza kumbukumbu za historia ya Wanefi. Amaroni alimwamini Mormoni na kumwambia kwamba kumbukumbu zilikuwa zimefichwa katika mlima. Amaroni alisema kwamba wakati Mormoni atakapokuwa na umri wa miaka 24, Mormoni alipaswa kuandika kile alichokiona kuhusu watu wao na kukiongeza kwenye kumbukumbu.

4 Nefi 1:47–49; Mormoni 1:2–4

kijana Mormoni anasali katika kijisitu cha miti, na nuru ikimzunguka

Mormoni alipokuwa anakua, alikumbuka kile Amaroni alichomwomba afanye. Wakati Mormoni akiwa na miaka 15, alitembelewa na Bwana. Mormoni alijifunza kuhusu wema wa Yesu.

Mormoni 1:5, 15

kijana Mormoni anavaa silaha na kutazama jeshi la Wanefi

Japokuwa Mormoni alikuwa kijana, alikuwa na nguvu. Wanefi walimchagua kuongoza majeshi yao. Mormoni aliwapenda watu kwa moyo wake wote. Aliwataka wamtii Mungu na wawe na furaha.

Mormoni 2:1–2, 12, 15, 19; 3:12

Akiwa mtu mzima, Mormoni anahuzunika na anasali, na ardhi inayowaka moto ikiwa nyuma yake

Mormoni alijaribu kuwasaidia watu. Alisali kwa ajili yao siku baada ya siku. Watu walijua walikuwa wakifanya mambo mabaya, lakini hawakutubu. Hawakuwa na nguvu za Mungu za kuwasaidia tena. Kwa sababu hawakuwa na imani, miujiza ilikuwa imekoma. Waliendelea kupigana, na wengi wao walikufa. Mormoni alihuzunika.

Mormoni 1:13–14, 16–19; 2:23–27; 3:1–12; 4:5, 9–12; 5:1–7

Mormoni anaandika na kupanga bamba za metali

Wakati Mormoni alipokuwa na miaka 24, alikwenda kwenye kilima ambapo kumbukumbu zilikuwa zimefichwa. Alianza kuandika hadithi na mafundisho ya watu kwenye mabamba ya metali. Mungu alimsaidia kujua kile alichopaswa kuandika. Mormoni aliandika kumbukumbu kwa miaka mingi. Leo, kumbukumbu hiyo inaitwa Kitabu cha Mormoni.

Maneno ya Mormoni 1:3–9; Mormoni 1:3–4; 2:17–18

Mormoni, mke wake, na watoto wake wanasafiri

Baada ya vita vingi, Walamani walikuwa wamewaua karibu Wanefi wote. Mormoni alijua watu wake wangeondoka karibuni. Alikuwa na huzuni kwa sababu hawakutubu na kumwomba Mungu msaada. Lakini alisali na kumwomba Mungu kuyalinda mabamba. Alijua mabamba yangekuwa salama kwa sababu yalikuwa na maneno ya Mungu.

Maneno ya Mormoni 1:11; Mormoni 5:11; 6:6, 16–22

Akiwa mzee, Mormoni anampa Moroni, mwanawe, mabamba ya metali

Mormoni aliwataka watu kuamini katika Kristo. Alitumaini kwamba watu wengi wangekisoma kitabu siku zijazo. Hasa alitaka familia za Walamani kukisoma siku moja. Kama wangefanya hivyo, wangejifunza kuhusu Yesu. Kabla Mormoni hajafa, alimpatia kumbukumbu Moroni, mwanawe, ili kwamba iwe salama.

Maneno ya Mormoni 1:1–2; Mormoni 3:17–22; 5:8–24; 6:6; 7; 8:1