Hadithi za Maandiko
Enoshi


“Enoshi,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)

“Enoshi,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni

Enoshi 1

Enoshi

Sala kuu kwa Bwana

Enoshi akiwinda

Yakobo alimpa mabamba mwanawe Enoshi. Enoshi aliandika juu yake kama alivyofanya Yakobo. Siku moja Enoshi alikwenda kuwinda ndani ya msitu. Alikumbuka kile baba yake alifundisha kuhusu Bwana. Yakobo alikuwa amemfundisha Enoshi kwamba kumfuata Bwana kutamletea furaha.

Yakobo 7:27; Enoshi 1:2–3

Enoshi akisali wakati wa mchana

Enoshi alitaka kuiona shangwe ambayo baba yake alizungumza juu yake. Aliamua kusali kwa Bwana. Alisali siku mzima na usiku kucha.

Enoshi 1:3–4

Enoshi akiangalia juu

Bwana alimwambia Enoshi kwamba dhambi zake zilikuwa zimesamehewa. Enoshi alijisikia kuwa mwenye furaha sana. Enoshi alibarikiwa kwa sababu ya imani yake Katika Yesu Kristo.

Enoshi 1:3, 5–8

Enoshi akisali usiku

Enoshi aliwataka Wanefi kuhisi furaha hii pia. Aliendelea kusali. Alimwomba Bwana kwa ajili ya Wanefi kuhisi furaha ile ile.

Enoshi 1:9

Enoshi akionekana mwenye furaha

Bwana alimwambia Enoshi kwamba Yeye atakuwa pamoja na Wanefi kama watazitii amri Zake Enoshi aliposikia hili, imani yake katika Bwana ikawa hata yenye nguvu zaidi.

Enoshi 1:10–11

Enoshi akiandika juu ya mabamba ya dhahabu

Enoshi alisali tena. Alimwomba Bwana kuwabariki Walamani na kuyaweka salama maandishi yale yaliyo juu ya mabamba. Aliwataka Walamani kuweza kusoma mabamba haya na kuamini katika Bwana. Bwana alimwahidi Enoshi kwamba Walamani watasoma yale maandishi siku moja.

Enoshi 1:11–17