Njoo, Unifuate 2024
Agosti 19–25: “Kulindwa na Nguvu Zake za Ajabu.” Alma 53–63


Agosti 19–25: ‘Kulindwa na Nguvu Zake za Ajabu.’ Alma 53–63,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Kitabu cha Mormoni 2024 (2023)

“Agosti 19–25. Alma 53–63,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2024 (2023)

Picha
vijana mashujaa elfu mbili

Vijana Mashujaa Elfu Mbili, na Arnold Friberg

Agosti 19–25: “Kulindwa na Nguvu Zake za Ajabu”

Alma 53–63

Linapolinganishwa na majeshi ya Walamani, “jeshi dogo” la Helamani (Alma 56:33) la wavulana halikuwa na uwezo wa kushinda. Licha ya kuwa wachache kwa idadi, wanajeshi wa Helamani “wote … walikuwa wadogo sana,” na “walikuwa hawajawahi kupigana” (Alma 56:46–47). Kwa namna fulani, hali yao yaweza kuonekana inayofahamika kwetu sisi ambao wakati mwingine tunahisi kuzidiwa na kushindwa katika vita yetu ya siku za mwisho dhidi ya Shetani na majeshi ya uovu ulimwenguni.

Lakini jeshi la Helamani lilikuwa na hali fulani bora kuliko Walamani ambayo haikuhusika na chochote kwenye idadi au ujuzi wa kijeshi. Walimchagua Helamani, nabii, awe kiongozi wao (ona Alma 53:19); “walikuwa wamefundishwa na mama zao, kwamba ikiwa hawatakuwa na shaka, Mungu angewaokoa” (Alma 56:47); na walikuwa na “imani kubwa kwa yale ambayo walikuwa wamefundishwa.” Kama matokeo, walilindwa na “uwezo wa kimiujiza wa Mungu” (Alma 57:26). Kwa hiyo wakati tunakabiliana na vita vya maisha, tunaweza kuwa majasiri. Jeshi la Helamani hutufundusha kwamba “yupo Mungu mwenye haki, na yeyote asiyemtilia mashaka, [atahifadhiwa] kwa uwezo wake wa ajabu” (Alma 57:26).

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Alma 53:10–22; 56:43–49, 55–56; 57:20–27; 58:39–40

Picha
seminary icon
Kuwa na imani katika Mungu hunisaidia nishinde hofu.

Kama haingekuwa imani yao, askari vijana wa Helamani wangekuwa na sababu nzuri ya kuhisi uoga. Kwa sababu ya imani yao, walikuwa hata na sababu zaidi ya kuwa majasiri. Unaposoma kuwahusu wao katika Alma 53–58, tafuta vitu ambavyo vinakusaidia unapokabiliana na hofu yako kwa imani katika Yesu Kristo. Fikiria kufokasi juu ya mistari ifuatayo: Alma 53:10–22; 56:43–49, 55–56; 57:20–27; 58:39–40. Jedwali lifuatalo linaweza kukusaidia uandike kile unachokipata.

Sifa za askari vijana wa Helamani:

Sababu yamkini za imani yao katika Kristo kuwa imara sana:

Walifanya nini ili kutumia imani katika Kristo:

Ni kwa jinsi gani Mungu aliwabariki:

Ili kushinda vita vyetu vya kiroho, sisi pia tunahitaji kupata nguvu ya Yesu Kristo. Ni kwa jinsi gani unaweza kupata nguvu Zake? Tafuta majibu katika ujumbe wa Rais Russell M. Nelson “Kuvuta Nguvu ya Yesu Kristo kwenye Maisha Yetu” (Liahona, Mei 2017, 39–42). Ungeweza kulinganisha ushauri wake na vitu ambavyo askari wa Helamani walifanya.

Baada ya kujifunza vitu hivi, fikiria kuhusu vita vyetu wenyewe vya kiroho. Andika kile unachohisi umetiwa msukumo kufanya ili kutumia imani yako katika Yesu Kristo.

Ona pia Neil L. Andersen, “Kujeruhiwa,” Liahona, Nov. 2018, 83–86; “Tupo Waaminifu wa Imani,” Nyimbo za Dini, na. 147; “Drawing upon the Power of God in Our Lives” (video), Maktaba ya Injili; Mada za Injili, “Imani katika Yesu Kristo,” Maktaba ya Injili.

Picha
askari vijana na mama zao

Hawakuwa na Shaka, na Joseph Brickey

Alma 58:1–12, 31–3761

Wafuasi wa Yesu Kristo hawakwaziki kwa urahisi.

Helamani na Pahorani walikuwa na sababu za kukwazika. Helamani hakuwa akipokea msaada kwa ajili ya majeshi yake, na Pahorani alilaumiwa kimakosa na Moroni kwa kuzuia msaada huo (ona Alma 58:4–9, 31–32; 60). Nini kinakuvutia kuhusu kuitikia kwao katika Alma 58:1–12, 31–37 na Alma 61? Kwa nini unahisi walijibu kwa njia hii?

Mzee David Bednar alimtaja Parohani kama mfano wa unyenyekevu na kufundisha kwamba “mifano mikuu na yenye maana ya unyenyekevu inapatikana katika maisha ya Mwokozi Mwenyewe” (“Unyenyekevu na Upole wa Moyo,” Liahona, Mei 2018, 32). Tafakari jinsi ambavyo Mwokozi alionesha unyenyekevu. Ona, kwa mfano, Mathayo 27:11–26; Luka 22:41–42; Yohana 13:4–17. Ni kwa jinsi gani unaweza kufuata mfano Wake?

Alma 60:7–14

Nina wajibu wa kuwainua watu wanaonizunguka.

Moroni aliandika kwamba Mungu angemwajibisha Pahorani kama kwa kujua alikuwa akiacha kutimiza mahitaji ya jeshi la Wanefi. Unajifunza nini kutoka Alma 60:7–14 kuhusu kuwatunza watu walio na shida? Je, unaweza kufanya nini ili kujua mahitaji ya wengine na kuyatimiza?

Alma 62:39–51

Kama mimi ni mnyenyekevu, changamoto za maisha zinaweza kuugeuza moyo wangu kwa Mungu.

Weka yai bichi na kiazi katika maji yanayochemka ili kukusaidia ufikirie kuhusu jinsi unavyoweza kuchagua kufanywa “laini” au “mgumu” kwa majaribu yako. Wakati yai lako na kiazi chako vinapikwa, jifunze Alma 62:39–51, na kuona jinsi watu walivyoitikia huduma ya Helamani baada ya vita vyao vya muda mrefu na Walamani. Ungeweza kisha kulinganisha hili na jinsi walivyokuwa wameitikia miaka 13 ya kuhubiri kwake hapo awali (ona Alma 45:20–24). Ni kwa jinsi gani Wanefi waliathirika kitofauti kwa mateso sawa na hayo? Wakati yai na kiazi vimeiva kabisa, pasua yai na ukate kiazi. Ni kwa jinsi gani maji yanayochemka yanaviathiri kwa namna taofauti? Unajifunza nini kuhusu jinsi tunavyoweza kuchagua kuitikia mateso? Ni kwa jinsi gani unaweza kumgeukia Mungu wakati wa mateso yako?

Tumia uzoefu kutoka nyumbani. Kama unafundisha darasa la Kanisa, waombe washiriki wa darasa kushiriki kile walichojifunza nyumbani. Kwa mfano, waulize kile walichojifunza kuhusu mateso na unyenyekevu kutokana na kuchemsha mayai na viazi.

Kwa mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la Liahona na magazeti ya Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana.

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Alma 53:20–21; 56:47–48

Ninaweza kuwa mwaminifu kwa Mungu kama askari vijana wa Helamani.

  • Unaweza kutumia nyenzo nyingi ili kushiriki hadithi ya askari wa Helamani, ikijumuisha picha katika muhtasari huu na “Mlango wa 34: Helamani na Mashujaa Vijana 2000” (Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 93–94). Ukurasa wa shughuli ya wiki unaweza kuwasaidia watoto wako wafikirie jinsi wanavyoweza kuwa kama jeshi la Helamani. Fikiria kushiriki baadhi ya sifa za askari vijana kutoka Alma 53:20–21 ili kuwawezesha waanze. Mngeweza pia kuimba pamoja “We’ll Bring the World His Truth” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 172–73).

Alma 56:45–48; 57:21

Naweza kuwa mwaminifu kufanya kile ambacho wazazi wangu wanafundisha kwa haki.

  • Askari vijana wa Helamani walitegemea imani ya mama zao walipokuwa wakikabiliana na changamoto kubwa. Pengine ungesoma Alma 56:46–48 pamoja na watoto na uwaalike wasikilize kile ambacho akina mama wa wavulana hawa waliwafundisha kuhusu imani. Ungeweza kuwauliza kitu ambacho wamejifunza kutoka kwa wazazi wao—au watu wazima waaminifu wengine—kuhusu Mwokozi. Kwa nini ni muhimu kutii “kwa ukamilifu”? (Alma 57:21).

  • Ni kwa jinsi gani wewe—kama akina mama wa wale askari mashujaa—unahakikisha watoto wako wanajua juu ya imani yako katika Mungu? Njia moja ni kushiriki jinsi imani yako inavyoyagusa maisha yako. Kwa mfano, ni kwa jinsi gani Yeye “alikukomboa” wakati wewe “ulipokuwa huna shaka?

Picha
mama akimfundisha mwanaye

Mbegu ya Imani, na Jay Ward

Alma 53:10–18

Ninaweza kushika maagano yangu kwa Baba wa Mbinguni.

  • Watoto wako wangeweza kuzungumza kuhusu wakati mtu fulani alipofanya nao ahadi na kuishika ahadi hiyo. Walihisi vipi wakati ahadi ilipotimizwa? Ungeweza kusoma Alma 53:10–18 na uwaalike watoto wako watafute jinsi Helamani, watu wa Amoni, na wana wa watu wa Amoni walivyofanya na kuzishika ahadi zao au maagano yao. Ungeweza kushiriki jinsi Baba wa Mbinguni anavyokubariki wakati unaposhika maagano yako.

Alma 61:3–14

Ninaweza kuchagua kutokasirika.

Fikiria kuwaalika watoto wako wafikirie kuhusu wakati ambapo walituhumiwa kwa kufanya jambo ambalo hawakulifanya. Waambie kuhusu jinsi hili lilivyotokea kwa Parohani (ona Alma 60:61; ona pia “Mlango wa 35: Kapteni Moroni na Parohani,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 95–97). Ili kujifunza kuhusu jinsi Pahorani alivyojibu, fanyeni zamu kusoma mistari kutoka Alma 61:3–14. Pahorani alifanya nini pale Moroni alipomtuhumu? (ona Alma 61:2–3, 8–9). Je, tunajifunza nini kuhusu msamaha kutoka kwenye mfano wa Mwokozi? (ona Luka 23:34).

Kwa ajili ya mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la gazeti la Rafiki.

Picha
vijana mashujaa elfu mbili

Ni Kweli, Bwana, Wote Wapo na Wamehesabiwa, na Clark Kelley Price

Chapisha