Njoo, Unifuate
Agosti 26–Septemba 1: “Mwamba wa Mkombozi Wetu.” Helamani 1–6


Agosti 26–Septemba 1:‘Mwamba wa Mkombozi Wetu.’ Helamani 1–6,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Kitabu cha Mormoni 2024 (2023)

“Agosti 26–Septemba 1. Helamani 1–6,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2024 (2023)

mawimbi yakigonga miamba

Agosti 26–Septemba 1: “Mwamba wa Mkombozi Wetu”

Helamani 1–6

Kitabu cha Helamani kimeandika vyote, ushindi na misiba miongoni mwa Wanefi na Walamani. Kinaanza na “taabu kubwa miongoni mwa Wanefi” (Helamani 1:1), na taabu hizo zinaendelea kutokea kote katika kumbukumbu hii. Hapa tunasoma kuhusu njama za kisiasa, magenge ya wanyan’ganyi, kukataliwa kwa manabii na kiburi na kutoamini kote nchini. Lakini pia tunapata mifano kama vile Nefi na Lehi na “sehemu kubwa ya walio wanyenyekevu,” ambao si tu waliendelea kuishi bali walistawi kiroho (Helamani 3:34). Ni kwa jinsi gani walifanya hilo? Ni kwa jinsi gani waliendelea kuwa imara wakati ustaarabu wao ulianza kupungua na kusambaratika? Kwa njia sawa na vile ambavyo yeyote yule miongoni mwetu hubaki imara katika “dhoruba kali” ibilisi anazotuma “[kupiga] juu [yetu]”—kwa kujenga maisha yetu “juu ya mwamba wa Mkombozi wetu, ambaye ni Kristo, Mwana wa Mungu, … msingi ambako kama watu wakijenga hawataanguka” (Helamani 5:12).

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Helamani 1–6

Kiburi hunitenganisha na Roho na nguvu za Mungu.

Unaposoma Helamani 1–6, unaweza kuona mpangilio katika tabia ya Wanefi. Wakati wanapokuwa wenye haki, Mungu anawabariki, na wanastawi. Baada ya muda, wanakuwa wenye kiburi na waovu, wakifanya chaguzi ambazo zinaongoza kwenye maangamizo na mateso. Kisha wananyenyekezwa na kutiwa msukumo ili watubu, na Mungu anawabariki tena. Mtindo huu unajirudia mara nyingi hadi baadhi ya watu wanauita “mzunguko wa kiburi.”

mzunguko wa kiburi

“Mzunguko wa kiburi.”

Tafuta mifano ya mzunguko huu unaposoma Helamani 1–6. Hapa kuna baadhi ya maswali ya kukusaidia uelewe mpangilio huu:

Ona pia “Mlango wa 18: Beware of PrideTeachings of Presidents of the Church: Ezra Taft Benson (2014), 229–40; “Ninakuhitaji,” Nyimbo za Dini, na. 47.

Helamani 3:24–35

Imani katika Kristo hujaza nafsi yangu kwa shangwe.

Katika Helamani 3, Mormoni alieleza wakati wa kufurahia ambapo Kanisa lilibarikiwa sana kiasi kwamba hata viongozi walishangaa. Kutokana na yale uliyosoma katika mistari 24–32, unafikiri ni kipi kilileta hali ya shangwe? Ingawaje siyo waumini wote waliendelea katika shangwe. Tazama tofauti kati ya watu walioelezwa katika mistari 33–35. Je, unajifunza nini kutokana na mfano wao?

Tafuta matumizi binafsi. Nabii Mormoni alitumia kirai “na hivyo, tunaona” ili kusisitiza kweli muhimu alipokuwa anafupisha Kitabu cha Mormoni. Kwa mfano, alitaka tuone nini katika Helamani 3:27–30? Unapojifunza maandiko, ungeweza kupumzika mara kwa mara kukamilisha kirai “na hivyo tunaona” kwa mujibu wa kile ulichosoma.

Helamani 5:6–7

Ninaweza kuheshimu jina la Bwana.

Kusoma Helamani 5:6–7 kunaweza kukupa msukumo wa kufikiria majina mengi ambayo umepatiwa, ikijumuisha majina ya familia. Majina haya yana maana gani kwako? Ni kwa jinsi gani unaweza kuyaheshimu? Hata cha muhimu zaidi, fikiria kile ambacho inamaanisha kujichukulia jina la Mwokozi (ona Moroni 4:3). Ni kwa jinsi gani unaheshimu jina hilo takatifu?

Helamani 5:12–52

seminary icon
Kama ninamfanya Yesu Kristo kuwa msingi wangu, sitaanguka.

Inamaanisha nini kwako “kujenga msingi wako” juu ya “mwamba wa Mkombozi wetu”? (Helamani 5:12). Ni kwa jinsi gani umepata usalama katika Yesu Kristo kutokana na dhoruba za maisha? Unaposoma Helamani 5:12–52, gundua jinsi Nefi na Lehi walivyobarikiwa kwa kujenga imani yao juu ya mwamba wa Mkombozi wao.

Baadhi ya watu wanapata msaada kuvuta twasira ya kile wanachojifunza. Ili kufafanua Helamani 5:12, ungeweza kujenga jengo dogo kwenye aina tofauti za misingi. Kisha ungeweza kutengeneza “dhoruba kali” kwa kunyunyizia maji juu yake na kutumia feni ili kusababisha upepo. Ni utambuzi gani hii inakupatia kuhusu kujenga msingi wako juu ya Yesu Kristo? Nini kingine unajifunza kutokana na video “A Secure Anchor”? (Maktaba ya Injili).

Mstari wa 50 hutaja “ushahidi mwingi” ambao Wanefi waliupata. Kusoma Helamani 5:12–52 kunaweza kukuletea akilini mwako ushahidi ambao Mungu amekupa wewe. Kwa mfano, pengine “mnong’ono” kutoka kwa Roho umeimarisha imani yako katika Mwokozi (Helamani 5:30; ona pia Mafundisho na Maagano 88:66). Au Pengine umekuwa katika giza na kumlilia Mungu kwa ajili ya imani kubwa zaidi (ona Helamani 5:40–47). Ni uzoefu upi mwingine umekusaidia ujenge msingi wako juu ya Yesu Kristo?

Ona pia Russell M. Nelson, “Hekalu na Msingi Wako wa Kiroho,” Liahona, Nov. 2021, 93–96; Sean Douglas, “Kukabiliana na Vimbunga Vyetu vya Kiroho kwa Kuamini katika Kristo,” Liahona, Nov. 2021, 109–11; Mada za Injili, “Imani katika Yesu Kristo,” Maktaba ya Injili.

Kwa mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la Liahona na magazeti ya Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana.

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Helamani 3:24, 33–33; 4:11–15

Baba wa Mbinguni ananitaka niwe mnyenyekevu.

  • Fikiria kuwaalika watoto wako kuchora toleo lao wenyewe la “mzunguko wa kiburi” kulingana na mchoro uliopo hapo juu. Kisha, mnaposoma pamoja Helamani 3:24, 33–34 na 4:11–15, wangeweza kuonesha sehemu za mzunguko ambazo mistari hii inazielezea. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa wanyenyekevu—na kubaki katika njia hiyo?

Helamani 5:12

Nitajenga msingi wangu juu ya Yesu Kristo.

  • Fikiria kutumia picha ya hekalu kuanzisha mazungumzo kuhusu kwa nini majengo yanahitaji misingi imara. Au ungeweza kutazama msingi wa nyumba yako au jengo la Kanisa. Ili kusisitiza nguvu za msingi imara kama mwamba, watoto wako wangejaribu kusogeza mwamba kwa kuupuliza. Mnaposoma pamoja Helamani 5:12, waulize watoto wako kwa nini wanadhani Yesu Kristo ni “msingi imara” kwa maisha yetu. Ni kwa jinsi gani tunaweza kujenga maisha yetu juu yake Yeye? (ona Helamani 3:27–29, 35 na Makala ya Imani 1:4).

  • Waalike watoto wako wajenge mnara kwa kutumia matofali au vifaa vingine juu ya aina tofauti za misingi (kama vile madonge ya pamba au jiwe pana). Je, ni kwa jinsi gani msingi imara ni kama Yesu Kristo? Wangeweza kuongeza tofali moja kwenye jengo kwa kila wazo wanaloshiriki kuhusu kile wanachofanya kumfuata Yeye.

Helamani 5:21–52

Roho Mtakatifu hunong’oneza kwa sauti ndogo, tulivu.

  • Sauti iliyoelezwa katika Helamani 5:29–30, 45–47 hutufundisha njia moja ambayo Roho Mtakatifu huzungumza nasi. Ili kuwasaidia watoto wako waelewe ukweli huu, fikiria kusoma “Mlango wa 37 Nefi na Lehi Gerezani” (Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 99–102). Wakati unapozungumza kuhusu sauti ambayo watu waliisikia, zungumza kwa sauti ya upole. Rudia hadithi mara kadhaa na waalike watoto wanong’one pamoja nawe. Wasaidie wafikirie njia zingine ambazo Roho Mtakatifu anaweza kuzungumza nasi. Ili kuimarisha kanuni hii, mngeweza kuimba pamoja “The Still Small Voice” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 106–7).

Helamani 5:20–52

Toba hubadilisha giza la kiroho kuwa nuru.

  • Ili kusisitiza kile Helamani 5:20–41 inachofundisha kuhusu giza na nuru, jaribu kusoma au kufanyia muhtasari mistari hii gizani, ukitumia tochi kwa ajili ya nuru. Watoto wako wangeweza kusikiliza kitu ambacho watu wanahitaji kufanya ili kwamba giza liweze kuondolewa. Kisha washa taa, na someni mistari 42–48 pamoja. Ni kipi mistari hii inatufundisha kuhusu toba?

Kwa ajili ya mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la gazeti la Rafiki.

Nefi na Lehi gerezani

Hata gerezani, Nefi na Lehi walilindwa kwa nguvu ya Mungu.

© Kitabu cha Mormoni kwa ajili ya Wasomaji Wadogo, Nefi na Lehi Wamezungukwa na Nguzo ya Moto, na Briana Shawcroft; isinakiliwe