“Septemba 16– 22: ‘Inua Kichwa Chako na Uchangamke.’ 3 Nefi 1–7,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Kitabu cha Mormoni 2024 (2023)
“Septemba 16–22. 3 Nefi 1–7,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2024 (2023)
Septemba 16–22: “Inua Kichwa Chako na Uchangamke”
3 Nefi 1–7
Kwa namna fulani, ulikuwa wakati wa kusisimua kuwa muumini katika Yesu Kristo. Unabii ulikuwa ukitimizwa—ishara kubwa na miujiza miongoni mwa watu viliashiria kuwa Mwokozi angezaliwa punde. Kwa upande mwingine, ulikuwa ni wakati wa wasiwasi kwa waaminio kwa sababu, licha ya miujiza yote, wasioamini walisisitiza kwamba “wakati umepita” wa kuzaliwa kwa Mwokozi (3 Nefi 1:5). Watu hawa walisababisha “makelele mengi kote nchini” (3 Nefi 1:7) na hata wakapanga siku ya kuwaua waaminio wote kama ishara iliyotabiriwa na Samweli Mlamani—usiku bila giza—haingetokea.
Katika hali hizi ngumu, nabii Nefi “aliomba kwa nguvu kwa Mungu wake kwa niaba ya watu wake” (3 Nefi 1:11). Jibu la Bwana ni la kutia msukumo kwa yeyote anayekabiliwa na mateso au wasiwasi na anahitaji kujua kwamba nuru itashinda giza: “Inua kichwa chako na uchangamke; … nitatimiza yote ambayo nimesababisha kuzungumzwa kwa midomo ya manabii wangu” (3 Nefi 1:13).
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani
Kuwa mwongofu katika injili ya Yesu Kristo kunahitaji subira na juhudi.
3 Nefi 1–7 huelezea watu ambao waliongoka kwa Bwana na injili Yake na wengine ambao hawakuongoka. Ni kipi kilileta tofauti kati ya makundi haya mawili? Chati kama hii ifuatayo ingeweza kukusaidia wewe uyapange mawazo yako:
Mambo ambayo yanayodhoofisha uongofu |
Mambo ambayo yanaimarisha uongofu | |
---|---|---|
Kutoamini maneno ya manabii na kuwadhihaki watu wema |
Kuwa na imani katika maneno ya manabii na kusali kwa ajili ya msaada | |
Kwa sababu ya Yesu Kristo, ninaweza “kuwa mchangamfu.”
Baba yako wa Mbinguni anajua kwamba maisha yako yatajumuisha nyakati ambazo ni ngumu, hata za kutisha. Lakini Yeye pia anataka upate furaha. Soma 3 Nefi 1:1–23 kujifunza kuhusu sababu za Wanefi waaminifu kuwa na hofu. Ni sababu ipi Bwana aliwapa wao ya “kuwa wachangamfu”?
Mwokozi alitumia kirai “jipeni moyo” mara kadhaa—kwa mfano Mathayo 14:24–27; Yohana 16:33; Mafundisho na Maagano 61:36; 78:17–19. Kitu gani kinakuvutia kuhusu mialiko hii? Ungeweza kusoma mistari inayohusika ili kuelewa hali ambazo kwazo Mwokozi alisema maneno haya. Katika kila hali, ni sababu ipi Yeye aliitoa kuwasaidia watu wakabiliane na hofu zao? Je, ni kwa jinsi gani amefanya hivi kwako?
Fikiria kujifunza hotuba ya Russell M. Nelson “Shangwe na Kunusurika Kiroho” (Liahona, Nov. 2016, 81–84). Ni kipi Rais Nelson anakufundisha kuhusu kupata shangwe katika kila hali? Tazama ni mara ngapi Rais Nelson anatumia neno fokasi. Pengine ungeweza kulinganisha kufokasi kamera au lenzi zingine na kufokasi juu ya Yesu Kristo. Ni kwa jinsi gani wewe utafokasi zaidi juu Yake?
Ona pia “Majonzi,” “Tumaini,” “Afya ya Akili,” au mada zingine katika sehemu ya “Msaada wa Maisha” ya Maktaba ya Injili.
Bwana atatimiza maneno Yake yote katika wakati Wake.
Soma 3 Nefi 1:4–7 na ufikirie kuhusu jinsi ambavyo ungeweza kuhisi kama ungekuwa mmoja wa waaminio. Je, walifanya nini ili kufanya imani yao iwe imara? (ona 3 Nefi 1:4–21 na 5:1–3). Je, ni kwa jinsi gani maneno ya Samweli yalitimizwa? (ona 3 Nefi 1:19–21). Ni kwa jinsi gani Bwana ametimiza maneno Yake katika maisha yako?
3 Nefi 1:4–15; 5:12–26; 6:10–15; 7:15–26
Mimi ni mwanafunzi wa Yesu Kristo.
Mormoni alitamka, “Tazama, mimi ni mwanafunzi wa Yesu Kristo” (3 Nefi 5:1). Kifungu hiki cha maneno kinamaanisha nini kwako? Fikiria kuchunguza 3 Nefi 1:4–15; 5:12–26; 6:10–15; na 7:15–26, ukitafuta sifa, imani, na matendo ya wanafunzi wa Kristo.
Ona pia “I’m Trying to Be like Jesus,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 78.
Ninapoifanyia mazoezi imani katika Yesu Kristo, sitahitaji kuogopa.
Uzoefu wa Wanefi na magenge ya wanyang’anyi una mafunzo mengi ambayo yanaweza kukusaidia katika hatari za kiroho unazokabiliana nazo. Tafuta masomo haya katika 3 Nefi 2:11–12 na 3:1–26. Kwa mfano, ungeweza kuchunguza maneno ya Gidianhi katika 3 Nefi 3:2–10 na kuyalinganisha na jinsi Shetani anavyojaribu kukudanganya. Je, unajifunza nini kutoka katika mfano wa Lakoneyo?
Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto
Nyota mpya ilitokea wakati Yesu Kristo alipozaliwa.
-
Ukurasa wa shughuli ya wiki hii unaweza kusaidia kuwafundisha watoto wako kuhusu miujiza Wanefi waliyoishuhudia Yesu alipozaliwa. Unaweza pia kutumia “Mlango wa 41: Ishara za Kuzaliwa kwa Kristo” (Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 114–16), ili kuwafundisha hadithi hii—au kuwasaidia waisimulie kwako.
Maneno ya nabii daima yanatimia.
-
Wakati wewe na watoto wako mnaposoma 3 Nefi 1:4–10, waalike wazungumze kuhusu jinsi ilivyokuwa kuwa mmoja wa waaminio walioshi wakati huo. Kisha, wanaposoma tukio lote katika mistari 11–15, wangeweza kupendekeza njia za kukamilisha sentensi hii: “Funzo la hadithi hii kwangu ni …”
-
Pengine watoto wako wanaweza kukusaidia kufikiria juu ya nyakati ambapo Mungu alitimiza ahadi Zake zilizotolewa kupitia nabii Wake. Wanaweza kupenda kutafuta picha za hadithi hizi katika Kitabu cha Sanaa za Injili (ona, kwa mfano, na. 7–8 na 81). Waruhusu washiriki kile wanachokijua kuhusu hadithi hizi, ikijumuisha jinsi ahadi za Mungu zilivyotimizwa. Someni pamoja 3 Nefi 1:20, na mshiriki ushahidi wenu wenyewe wa kweli hizi.
3 Nefi 2:11–12; 3:13–14, 24–26
Tunakuwa imara zaidi pale tunapokusanyika pamoja.
-
Wasaidie watoto wako wagundue kwa nini Wanefi walikusanyika pamoja na baraka ambazo zilikuja juu yao katika 3 Nefi 2:11–12 na 3:13–14, 24–26. Kwa nini ni muhimu kwetu kukusanyika pamoja leo katika familia zetu na kanisani?
-
Je, unalijua somo la vitendo ambalo hufundisha kuhusu nguvu za umoja? Pengine watoto wangejaribu kuvunja kijiti kimoja na kisha fungu la vijiti au kuchana karatasi moja na kisha karatasi nyingi zilizowekwa pamoja. Ni kwa jinsi gani sisi ni kama vijiti au karatasi?
Mimi ni mwanafunzi wa Yesu Kristo.
-
Baada ya kusoma pamoja 3 Nefi 5:13, waalike watoto warudie kirai “Mimi ni mwanafunzi wa Yesu Kristo.” Ili kujifunza kile inachomaanisha kuwa mwanafunzi wa Yesu Kristo, someni pamoja baadhi ya mifano hii: Walamani walioongoka (ona 3 Nefi 6:14, Mormoni (ona 3 Nefi 5:12–26), na Nefi (ona 3 Nefi 7:15–26). Ungeweza pia kupata mawazo katika wimbo kama vile “I’m Trying to Be like Jesus” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 78–79).
-
Kwenye kipande cha karatasi, wasaidie watoto wako wachore mkono wao na wakate mchoro huo. Andika “Mimi ni mwanafunzi wa Yesu Kristo” kwenye upande mmoja na waalike wachore kitu wanachoweza kufanya ili kuwa mwanafunzi kwenye upande wa pili.