Njoo, Unifuate 2024
Novemba 4–10: “Ninawazungumzia Kama Vile Mko Hapa.” Mormoni 7–9


“Novemba 4–10: ‘Ninawazungumzia Kama Vile Mko Hapa.’ Mormoni 7–9,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Kitabu cha Mormoni 2024 (2023)

“Novemba 4–10. Mormoni 7–9,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2024 (2023)

Picha
Moroni akiandika kwenye mabamba ya dhahabu

Moroni Akiandika kwenye Mabamba ya Dhahabu, na Dale Kilborn

Novemba 4–10: “Ninawazungumzia Kama Vile Mko Hapa”

Mormoni 7–9

Moroni alijua vile ilivyo kuwa mpweke katika ulimwengu wenye uovu—hasa baada ya baba yake kuuwawa vitani na Wanefi kuangamizwa. “Na hata nimebaki peke yangu,” aliandika. “Sina marafiki wala popote pa kwenda” (Mormoni 8:3, 5). Mambo pengine yalionekana yasiyo na tumaini, lakini Moroni alipata tumaini katika Yesu Kristo na ushuhuda wake kwamba “kusudi la milele la Bwana litaendelea” (Mormoni 8:22). Na Moroni alijua kwamba sehemu muhimu katika kusudi hilo la milele lingekuwa Kitabu cha Mormoni—kumbukumbu ambayo alikuwa sasa akiikamilisha kwa bidii, kumbukumbu ambayo siku moja ingewaleta watu wengi “kwenye ufahamu wa Kristo” (Mormoni 8:16; 9:36). Imani ya Moroni katika ahadi hizi ilimwezesha kutangaza kwa wasomaji wa siku zijazo wa kitabu hiki, “Ninawazungumzia kama vile mko hapa” na “Najua kwamba mtapokea maneno yangu” (Mormoni 8:35; 9:30). Na sasa tunayo maneno yake na kazi ya Bwana inaendelea kusonga, kwa kiasi fulani kwa sababu Mormoni na Moroni walibaki wakweli kwenye misheni yao, hata wakati walipokuwa peke yao.

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Mormoni 7

“Amini katika Yesu Kristo” na “shikilia injili [Yake].”

Baada ya kufupisha kumbukumbu ya watu wake, Mormoni alitoa ujumbe wa kuhitimisha katika Mormoni 7. Kwa nini unafikiri alichagua ujumbe huu? Unadhani inamaanisha nini kwako “kushikilia kwa bidii injili ya Kristo”? Mormoni 7:8).

Ona pia “Kristo Mwokozi,,” Nyimbo za Dini, na. 66.

Mormoni 7:8–10; 8:12–16; 9:31–37

Kitabu cha Mormoni ni cha thamani kubwa.

Rais Russell M. Nelson aliuliza: “Ikiwa ungepewa almasi au rubi au Kitabu cha Mormoni, ungechagua nini? Kwa kweli, ni kipi kilicho cha thamani kubwa kwako?” (“Kitabu cha Mormoni: Maisha Yako Yangekuwaje Bila Hicho?,” Liahona, Nov. 2017, 61).

Ni kipi unapata katika Mormoni 7:8–10; 8:12–22; na 9:31–37 ambacho hukusaidia uelewe kwa nini Kitabu cha Mormoni ni cha thamani katika siku yetu? Kwa nini kina thamani kwako? Unaweza kupata umaizi zaidi katika 1 Nefi 13:38–41; 2 Nefi 3:11–12; na Mafundisho na Maagano 33:16; 42:12–13.

Picha
nakala za Kitabu cha Mormoni katika lugha mbalimbali

Maandishi ya manabii wa Kitabu cha Mormoni yanatumika kwetu.

Mormoni 8:1–11

Ninaweza kutii amri hata wakati wengine hawafanyi hivyo.

Wakati mwingine unaweza kuhisi mpweke katika juhudi zako za kushika amri. Ni kipi unaweza kujifunza kutokana na mfano wa Moroni ambacho kingeweza kusaidia? (ona Mormoni 8:1–11). Kama ungeweza kumuuliza Moroni jinsi alivyobakia mwaminifu, unadhani angesema nini?

Ona pia “All May Know the Truth: Moroni’s Promise” (video), Maktaba ya Injili.

Mormoni 8:26–41; 9:1–30

Kitabu cha Mormoni kiliandikwa kwa ajili ya siku yetu.

Yesu Kristo alimuonesha Moroni kile ambacho kingekuwa kikitendeka wakati Kitabu cha Mormoni kitakapokuja (ona Mormoni 8:34–35), na hicho kilimsababisha yeye atoe maonyo makali kwa ajili ya siku yetu. Unaposoma Mormoni 8:26–41 na 9:1–30, tafakari jinsi maneno yake yanavyoweza kutumika kwako. Kwa mfano, katika mistari hii Moroni anauliza maswali 24. Ni ushahidi upi unauona katika maswali haya kwamba Moroni aliiona siku yetu? Je! ni kwa jinsi gani Kitabu cha Mormoni kinasaidia katika changamoto ambazo Moroni aliziona kabla?

Msikilize Roho. Kuwa makini kwa mawazo na hisia zako, hata kama zinaonekana hazihusiani na kile unachosoma. Misukumo hii inaweza kuwa kile ambacho Baba yako wa Mbinguni anakutaka ujifunze. Kwa mfano, ni misukumo ipi uliyonayo baada ya kutafakari maswali Moroni aliyouliza katika Moroni 9:1–30?

Mormoni 9:1–25

Picha
ikoni ya seminari
Yesu Kristo ni Mungu wa miujiza.

Moroni alihitimisha maandishi ya baba yake kwa ujumbe wenye nguvu kwa ajili ya watu katika siku yetu ambao hawaamini katika miujiza (ona Mormoni 8:26; 9:1, 10–11). Je, kwa nini unahisi imani katika miujiza inahitajika leo? Chunguza Mormoni 9:9–11, 15–27 na Moroni 7:27–29 na utafakari maswali kama vile:

  • Ninajifunza nini kuhusu Mwokozi kutoka kwenye mistari hii?

  • Ninajifunza nini kuhusu miujuza, ya zamani na ya sasa?

  • Ni yapi manufaa ya kuamini kwamba Yesu Kristo ni Mungu wa miujiza? Ni yapi matokeo ya kutoamini hili?

  • Ni miujiza ipi—mikubwa na midogo—Mwokozi ameifanya katika maisha yangu? Miujiza hii inanifundisha nini kumhusu Yeye?

Rais Russell M. Nelson alifundisha: “Mwokozi na Mkombozi wetu, Yesu Kristo, atafanya baadhi ya kazi Zake kubwa kati ya sasa na wakati atakapokuja tena. Tutaona dalili za kimiujiza kwamba Mungu Baba na Mwanaye, Yesu Kristo, wanaongoza Kanisa hili katika ukuu wa enzi na utukufu” (“Ufunuo kwa ajili ya Kanisa, Ufunuo kwa ajili ya Maisha Yetu,” Liahona, Mei 2018, 96). Unahisi baadhi ya miujiza hii inaweza kuwa ipi? Unaweza kufanya nini ili kumsaidia Mwokozi aitimize?

Ni kipi unajifunza kuhusu imani na miujiza kutokana na uzoefu wa Watakatifu wa Samoa, Tonga, Fiji na Tahiti wakati Rais na Dada Nelson walipowatembelea? (ona Russell M. Nelson, “Kristo Amefufuka; Imani Kwake Itahamisha Milima,” Liahona, Mei 2021, 101–4).

Ona pia Ronald A. Rasband, “Tazama! Mimi ni Mungu wa Miujiza,” Liahona, Mei 2021, 109–12 Mada za Injili, “Miujiza,” Maktaba ya Injili.

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Mormoni 7:8–10

Kitabu cha Mormoni na Biblia vinashuhudia juu ya Yesu Kristo.

  • Ili kusisitiza uhusiano kati ya Biblia na Kitabu cha Mormoni, kama Moroni alivyofanya, ungeweza kucheza na watoto wako mchezo kama huu: Waombe waseme “Agano la Kale, Agano Jipya” wakati ukinyanyua nakala ya Biblia na “Ushuhuda Mwingine” wakati ukinyanyua nakala ya Kitabu cha Mormoni. Ungeweza pia kuchagua matukio kadhaa ambapo vyote, Biblia na Kitabu cha Mormoni vinashuhudia juu yake—kama vile kuzaliwa kwa Yesu, kifo, na Ufufuko—na uwaalike watoto wako watafute picha za matukio haya (kwa mfano, katika Kitabu cha Sanaa za Injili).

  • Ili kuwasaidia watoto wako wajifunze makala ya nane ya imani ungeweza kuandika kila neno katika vipande tofauti tofauti vya karatasi. Waalike watoto wako wafanye kazi pamoja kuweka maneno katika mpangilio sahihi na waisome mara kadhaa.

Mormoni 8:1–7

Ninaweza kutii amri hata wakati ninapohisi nipo peke yangu.

  • Mfano wa Moroni ungeweza kuwatia msukumo watoto wako kutii amri za Mungu hata wakati wanapohisi kuwa wapweke. Baada ya kusoma Mormoni 8:1–7 pamoja nao, wangeweza kushiriki ni kwa jinsi gani wangehisi kama wangekuwa Moroni. Katika mistari 1, 3, na 4, ni kipi aliamriwa kufanya, na kwa jinsi gani alitii? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa zaidi kama Moroni?

  • Pengine wewe na watoto wako mngeweza kuzungumza kuhusu hali hizi ambapo wanapaswa kufanya uchaguzi kati ya mema na mabaya wakati ambapo hakuna anayetazama. Ni kwa jinsi gani kuwa na imani katika Yesu Kristo kunatusaidia katika hali hizi? Wimbo kama “Stand for the Right” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 159) ungeweza kuongezea kwenye mjadala huu.

Mormoni 8:24–26; 9:7–26

Yesu Kristo ni “Mungu wa miujiza.”

  • Ungeweza kutaka kuelezea kwa watoto wako kwamba muujiza ni jambo ambalo Mungu hufanya ili aoneshe nguvu Zake na abariki maisha yetu. Kisha ungeweza kusoma virai kutoka katika Mormoni 9:11–13, 17 ambavyo vinaelezea baadhi ya miujiza ya Mungu, na watoto wako wangeweza kufikiria miujiza mingine (picha kutoka kwenye Kitabu cha Sanaa za Injili, kama vile na. 26, 40, 41, na 83, zinaweza kusaidia). Zungumza kuhusu miujiza ambayo Mungu ameifanya katika maisha yako.

  • Waoneshe watoto wako maelezo ya upishi, na zungumza kuhusu kile ambacho kingetokea kama ungesahahu kiungo muhimu. Someni pamoja Mormoni 8:24 na 9:20–21 mtafute “viungo” ambavyo vingeongoza kwenye miujiza kutoka kwa Mungu.

Kwa ajili ya mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la gazeti la Rafiki.

Picha
Moroni akitazama maangamizo ya Wanefi

Moroni Akitazama Maangamizo ya Wanefi, na Joseph Brickey

Chapisha