Njoo, Unifuate 2024
Novemba 18–24: “Kwamba Uovu Huu Uweze Kuondolewa.” Etheri 6–11


“Novemba 18–24: ‘Kwamba Uovu Huu Uweze Kuondolewa.’ Etheri 6–11,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Kitabu cha Mormoni 2024 (2023)

“Novemba 18–24. Etheri 6–11,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2024 (2023)

Picha
Mashua za Wayaredi baharini

Nitawarudisha Juu Tena Kutoka kwenye Kilindi cha Bahari, na Jonathan Arthur Clarke

Novemba 18–24: “Kwamba Uovu Huu Uweze Kuondolewa”

Etheri 6–11

Mamia ya miaka baada ya Wayaredi kuangamizwa, Wanefi waligundua mabaki ya ustaarabu wao wa kale. Miongoni mwa mabaki haya ilikuwa kumbukumbu za ajabu—mabamba ya “dhahabu safi” yaliyokuwa “yamejaa michoro” na Wanefi “walitamani sana” kuyasoma (Mosia 8:9; 28:12). Leo hii unao ufupisho wa kumbukumbu hii, na inaitwa kitabu cha Etheri. Wanefi walipoisoma, “walijawa na huzuni” kujifunza juu ya janga lililowapata Wayaredi. “Walakini iliwapa ufahamu mwingi, ambao uliwafurahisha” (Mosia 28:12, 18). Wewe pia, unaweza kupata nyakati za huzuni katika kitabu hiki. Lakini unaweza pia kufurahia kipawa hiki cha maarifa. Kwa hiyo Moroni aliandika “ni hekima katika Mungu kwamba hivi vitu vinapaswa kuoneshwa kwenu … ili uovu upate kuondolewa mbali, na ili wakati ungekuja ambapo Shetani hawezi kuwa na uwezo kwenye mioyo ya watoto wa watu” (Etheri 8:26).

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Etheri 6:1–12

Bwana ataniongoza kupitia safari ya maisha yangu hapa duniani.

Unaweza kupata utambuzi wa kiroho kama utalinganisha safari ya Wayaredi kuvuka bahari na safari yako ya maisha yote. Kwa mfano, ni kipi Bwana ametoa ambacho kinaangaza njia yako kama yale mawe ndani ya mashua za Wayaredi? Mashua zingeweza kuwakilisha nini, au pepo ambazo “zinavuma kuelekea nchi ya ahadi”? (Etheri 6:8). Je, unajifunza nini kutokana na vitendo vya Wayaredi kabla, wakati na baada ya safari? Je, ni kwa jinsi gani Bwana anakuongoza wewe kuelekea kwenye nchi yako ya ahadi?

“Imbeni sifa kwa Bwana.” Wayeradi walionesha shukrani zao na upendo kwa ajili ya Mungu kupitia wimbo na sifa (ona Etheri 6:9). Ungeweza kutafuta au kuandaa nafasi za kutumia muziki na ushuhuda wa kumsifu Mungu nyumbani na kanisani. Kwa mfano, ingeweza kuwa sahihi kuimba wimbo wa sifa kama “Praise the Lord with Heart and Voice” (Nyimbo za Dini, 73) wakati unapojifunza Etheri 6:1–12.

Picha
Familia ya Wayaredi ndani ya mashua yao

Mtoto ndani ya Mashua,, na Kendal Ray Johnson

Etheri 6:5–18, 30; 9:28–35; 10:1–2

“Tembea kwa unyenyekevu mbele za Bwana.”

Ingawa kiburi na uovu vinaonekana kutawala historia ya Wayaredi, ipo pia mifano ya unyenyekevu katika sura hizi—hasa katika Etheri 6:5–18, 30; 9:28–35; na 10:1–2. Kutafakari maswali yafuatayo kunaweza kukusaidia ujifunze kutokana na mifano hii: Kwa nini Wayaredi hawa walijinyenyekeza katika hali hizi? Ni kwa jinsi gani walionesha unyenyekevu wao? Ni kwa jinsi gani Mungu aliwabariki kama matokeo? Fikiria kile unachoweza kufanya kwa hiari yako ili “kujinyenyekeza mbele za Bwana” (Etheri 6:17) badala ya kulazimishwa kuwa mnyenyekevu (ona Mosia 4:11–12; Alma 32:14–18).

Ona pia Dale G.Renlund, “Fanya kwa Haki, Penda Rehema na Tembea kwa Unyenyekevu pamoja na Mungu,” Liahona, Nov. 2020, 109–12.

Etheri 7–11

Picha
ikoni ya seminari
Ninaweza kuwa kiongozi aliye kama Kristo.

Sura 7–11 za Etheri zinazungumzia angalau vizazi 28. Ingawa ni maelezo machache yanaweza kutolewa kwenye nafasi ndogo kama hii, mpangilio unajitokeza kwa haraka kuhusu matokeo ya uongozi wa haki. Je, unajifunza kipi kuhusu uongozi kutokana na mifano hii—hasi au chanya—ya wafalme walioorodheshwa hapa?

Mzee Dieter F. Uchtdorf alitoa ushauri wenye msaada kuhusu uongozi katika ujumbe wake, “Mkuu miongoni Mwenu” (Liahona, Mei 2017, 78–81). Fikiria kujifunza ujumbe huu—hasa hadithi ambazo yeye alisimulia—ukitafuta kanuni au mipangilio ya uongozi kama wa Kristo. Ni lini umeona kanuni au mipangilio hii ikidhihirishwa na watu ambao wanaongoza?

Unapotafakari kile ambacho umejifunza, fikiria kuhusu nafasi ambazo unaweza kuwa nazo kuongoza au kuwashawishi wengine nyumbani kwako, katika jumuia, kwenye wito wa Kanisa, na kadhalika. Ni kwa jinsi gani wewe unaweza kukuza sifa kama za Kristo, hata kama huna kazi mahususi ya uongozi?

Ona pia Mada za Injili, “Kuhudumu katika Wito wa Kanisa, Maktaba ya Injili; “Kanuni za Uongozi katika Kanisa; Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 4.2 (ChurchofJesusChrist.org).

Etheri 8:7–26

Bwana hafanyi kazi gizani.

Wakati watu wanapopanga kufanya vitendo vyao viovu kuwa siri, wanajihusisha katika kundi ovu la siri. Kwa kuongezea kwenye kundi ovu la siri lililoelezwa katika Etheri 8:7–18, mifano mingine yaweza kupatikana katika Helamani 1:9–12; 2:2–11; 6:16–30, na Musa 5:29–33. Fikiria kutofautisha mistari hii na 2 Nefi 26:22–24, ambapo Nefi alieleza jinsi Bwana anavyoifanya kazi Yake. Kwa nini unadhani Moroni aliamriwa kuandika kile yeye alichofanya kuhusu makundi maovu ya siri?

Umejifunza nini kutoka katika kitabu cha Etheri ambacho kinaweza kukusaidia upate baraka zilizoelezwa katika Etheri 8:26?

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Etheri 6:1–12

Ninaweza kumtumainia Baba wa Mbinguni anifariji wakati ninapokuwa na hofu.

  • Kila mtu anakuwa na siku ngumu—hata watoto wadogo. Pengine ungeweza kuwasaidia watoto wako watafute maneno na virai katika Etheri 6:1–12 ambavyo vinaonesha jinsi Wayaredi walivyomtumaini Mungu wakati wa baadhi ya siku ngumu na za kuogofya sana. Fikiria kushirikiana mmoja na mwingine baadhi ya uzoefu ambapo Mungu alikusaidia wakati wa nyakati ngumu katika maisha yako.

Etheri 6:9, 12, 30; 7:27; 10:2

Kukumbuka kile ambacho Bwana amekufanyia kunaleta shukrani na amani.

  • Baada ya kufika salama katika nchi ya ahadi, Wayaredi walikuwa na shukrani kiasi kwamba “machozi ya shangwe yakatiririka” (Etheri 6:12). Ungeweza kuwatia msukumo watoto wako wahisi shukrani kwa ajili ya baraka za Mungu kwa kuwasaidia wapate virai kutoka Etheri 6:9, 12 ambavyo vinaonesha jinsi Wayaredi walivyotoa shukrani zao kwa Mungu. Wanaweza kufurahia kuimba, kama Wayaredi walivyofanya, wimbo ambao unaelezea shukrani, kama vile “I Thank Thee, Dear Father” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 195). Waombe watoto wako wakuambie kuhusu baadhi ya mambo waliyo na shukrani kwayo.

  • Pengine watoto wako wangeweza kusoma Etheri 6:30; 7:27; na 10:2 na kutafuta kile ambacho wafalme hawa wenye haki walikikumbuka. Ni kwa jinsi gani hii iliathiri jinsi walivyowaongoza watu wao? Wewe na watoto wako mngeweza kujadili njia za kujikumbusha ninyi wenyewe juu ya kitu ambacho Mungu amewafanyia. Kwa mfano, pengine ungeweza kuandika kuhusu kitu hicho au kuchora picha yake. Ungeweza kupendekeza kwamba wajenge tabia ya kuandika kila mara baraka wanazogundua kutoka kwa Bwana (ona “O Remember, Remember” [video, Maktaba ya Injili).

Etheri 7:24–27

Ninabarikiwa pale ninapomfuata nabii wa Mungu.

  • Pengine wewe na watoto wako mngeweza kufurahia kuigiza baadhi ya vitu ambavyo nabii ametufundisha tufanye. Ungeweza hata kuligeuza kuwa mchezo ambapo mnakisia matendo yanawakilisha kitu gani. Hii ingeweza kuwaandaa watoto wako kujadili kwa nini ni muhimu kumfuata nabii wa Mungu. Mngeweza kisha kusoma Etheri 7:24–27 na mtafute kile kilichotendeka wakati watu walipotii maneno ya nabii wa Mungu. Ni kwa jinsi gani tunabarikiwa tunapomfuata nabii leo?

Etheri 9:28–35; 11:5–8

Bwana ana huruma wakati ninapotubu.

  • Kutafuta mipangilio ni ujuzi wenye msaada wa kujifunza maandiko. Kitabu cha Etheri kina mpangilio unaorudiwa ambao unasisitizia rehema ya Bwana. Ili kuwasaidia watoto wako wapate mpangilio huu, waalike wasome Etheri 9:28–35 na Etheri 11:5–8, wakitafuta mifanano katika matukio haya mawili. Tunajifunza nini kutoka kwenye hadithi hizi? Pengine wangeweza kutafuta picha katika Kitabu cha Sanaa za Injili za watu wengine katika maandiko ambao walitubu na kusamehewa.

Kwa ajili ya mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la gazeti la Rafiki.

Picha
Mashua za Wayaredi baharini

Mashua za Wayaredi, na Gary Ernest Smith

Chapisha