Njoo, Unifuate
Sauti za Urejesho: Kukusanyika Ohio


“Sauti za Urejesho: Kukusanyika Ohio,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Mafundisho na Maagano 2025 (2025)

“Kukusanyika Ohio,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2025

ikoni ya sauti za urejesho

Sauti za Urejesho

Kukusanyika Ohio

Kirtland katika miaka ya 1830

Kijiji cha Kirtland, na Al Rounds

Phebe Carter

Picture of Phoebe Carter Woodruff, wife of Wilford Woodruff, circa 1840.

Miongoni mwa Watakatifu wengi waliokusanyika Ohio katika miaka ya 1830 alikuwa Phebe Carter. Alijiunga na Kanisa huko kaskazini mashariki mwa Marekani akiwa kwenye miaka ya ishirini, ingawa wazazi wake hawakujiunga. Baadaye aliandika juu ya uamuzi wake wa kuhamia Ohio ili kuungana na Watakatifu:

“Marafiki zangu walishangaa kwa mwelekeo wangu, kama mimi nilivyoshangaa, lakini kitu fulani ndani yangu kilinisukuma niendelee. Huzuni ya Mama yangu kwa kuondoka kwangu nyumbani ilikuwa takribani zaidi ya ninavyoweza kuvumilia; na isingekuwa roho ndani yangu ningesita mwishowe. Mama yangu aliniambia afadhali angeniona mimi nikizikwa kuliko kuondoka hivi peke yangu nje katika ulimwengu katili.

“‘[Phebe],’ alisema, kwa kuvutia, ‘je, utarudi kwangu kama utaona umormoni ni uongo?’

“Nilimjibu, ‘ndiyo, mama; nitarudi.’ … Jibu langu lilituliza wasiwasi wake; lakini lilitusababishia wote huzuni kubwa ya kutengana. Wakati muda ulipofika wa kuondoka kwetu sikuthubutu kujiamini mwenyewe kusema kwaheri; kwa hiyo niliandika kwaheri zangu kwa kila mmoja, na kuziacha juu ya meza yangu, nikakimbia kushuka ngazi na kurukia kwenye gari la farasi. Hivyo niliacha nyumba niliyoipenda ya utoto wangu kuunganisha maisha yangu na watakatifu wa Mungu.”

Katika moja ya jumbe hizo za kuagana, Phebe aliandika:

“Wazazi Wapendwa—Mimi sasa niko karibu kuacha paa la baba yangu kwa muda … sijui kwa muda gani—lakini sio bila hisia ya shukrani kwa ukarimu ambao nimeupata kutoka utoto wangu mpaka sasa—lakini Majaliwa yanaonekana kuamua vinginevyo sasa kuliko ilivyokuwa. Acha tuache vitu hivi vyote kwenye mikono ya Majaliwa na tuwe wenye shukrani kwamba tumeruhusiwa kuishi pamoja kwa muda mrefu chini ya hali za kufaa kama tulivyoishi, tukiamini kwamba vitu vyote vitafanya kazi kwa ajili ya faida yetu kama tunampenda Mungu kikamilifu. Acha tutambue kwamba tunaweza kusali kwa Mungu mmoja ambaye atasikia sala za dhati za viumbe vyake vyote na kutupatia kile ambacho ni kizuri zaidi kwa ajili yetu. …

“Mama, ninaamini ni mapenzi ya Mungu kwangu mimi kwenda magharibi na nimeshawishika kwamba imekuwa kwa muda mrefu. Sasa njia imefunguka … ; ninaamini kwamba ni roho wa Bwana ambaye amefanya kile ambacho kinatosha kwa ajili ya mambo yote. Usiwe na wasiwasi kwa ajili ya mtoto wako; Bwana atanifariji. Ninaamini kwamba Bwana atanitunza na kunipa kile kilicho bora zaidi. … Ninakwenda kwa sababu Bwana wangu anaita—ameweka wazi wajibu wangu.”

Muhtasari

  1. Edward W. Tullidge, The Women of Mormondom (1877), 412.

  2. Phebe Carter letter to her parents, no date, Church History Library, Salt Lake City; punctuation modernized. Phebe alijiunga na Kanisa mwaka 1834, akahamia Ohio karibia 1835, na akaolewa na Wilford Woodruff mwaka 1837.