Njoo, Unifuate
Februari 10–16. 2 Nefi 6–10: “Ee Jinsi Gani Ulivyo Mkuu Mpango wa Mungu Wetu!”


“Februari 10–16. 2 Nefi 6–10: ‘Ee Jinsi Gani Ulivyo Mkuu Mpango wa Mungu Wetu!’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2020 (2020)

“Februari 10–16. 2 Nefi 6–10,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2020

Picha
Yesu anaomba katika Gethsemane

Si Mapenzi Yangu, Bali Yako Yatendeke, na Harry Anderson

Februari 10–16

2 Nefi 6–10

“Ee Jinsi Gani Ulivyo Mkuu Mpango wa Mungu Wetu!”

Unaposoma 2 Nefi 6–10, tafakari kile ambacho Bwana anajaribu kukufundisha. Unapogundua kweli hizi, ziandike na uzingatie kwa sala jinsi unavyoweza kutumia kile unachojifunza.

Andika Misukumo Yako

Ilikuwa takriban miaka 40 tangu familia ya Lehi itoke Yerusalemu. Walikuwa katika nchi mpya ya ajabu, upande mwingine wa dunia mbali na Yerusalemu na watu wengine wa agano wa Mungu. Lehi alikuwa amefariki, na uzao wake ulikuwa tayari umeanza kile ambacho kingekuwa vita vya karne nyingi kati ya Wanefi—“wale ambao waliamini maonyo na ufunuo wa Mungu”—na Walamani, ambao hawakuamini (2 Nefi 5:6). Katika hali hizi, Yakobo, ambaye alikuwa kaka mdogo wa Nefi na sasa akiwa ametawazwa kama mwalimu kwa Wanefi, alitaka watu wa agano wafahamu ya kwamba Mungu kamwe asingewasahau, kwa hiyo kamwe wasimsahau. Huu ni ujumbe ambao hakika tunauhitaji katika dunia yetu, ambamo maagano yanadhalilishwa na ufunuo kukataliwa. “Hebu tumkumbuke, … kwani hatujatupiliwa mbali. … Kubwa ni ahadi za Bwana,” alitangaza (2 Nefi 10:20–21). Miongoni mwa ahadi hizo, hakuna iliyo kubwa kuliko ahadi ya “upatanisho usio na kipimo” ili kushinda kifo na jahanamu (2 Nefi 9:7). “Kwa hivyo,” Yakobo alihitimisha, “chagamsheni mioyo yenu”! (2 Nefi 10:23).

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi

2 Nefi 6–8

Bwana atawarehemu watu wake na atatimiza ahadi Zake.

Ili kuwasaidia watu wake waelewe kwamba walikuwa sehemu ya nyumba ya Israeli na wangeweza kumuamini Mungu na ahadi Zake, Yakobo alidondoa utabiri wa Isaya, katika 2 Nefi 6–8. Isaya alielezea kutawanywa kwa Israeli na kukusanyika ambako kuliahidiwa na Mwokozi na ukombozi wa watu Wake. Unaposoma, tafakari maswali kama yafuatayo:

  • Ninajifunza nini kuhusu upendo wa kukomboa wa Mwokozi kwangu mimi?

  • Ni faraja gani Mwokozi anawapa wale wanaomtafuta?

  • Ni nini naweza kufanya ili kwa uaminifu zaidi “nimsubiri” Mwokozi na baraka Zake zilizoahidiwa?

2 Nefi 9:1–26

Kupitia Upatanisho Wake, Yesu Kristo anakomboa watu wote kutokana na kifo cha kimwili na cha kiroho.

Ni maneno gani au picha gani unaweza kutumia kumuelezea mtu juu ya hitaji letu kuu la Mkombozi ili atuokoe kutoka kwenye kifo na dhambi? Yakobo alitumia maneno “mwovu” na “mnyama.” Ni nini Yakobo alifundisha kuhusu “huyo mnyama, kifo na jahanamu” na “njia ya kuepuka” ambayo Mungu ametutayarishia? (2 Nefi 9:10). Unaposoma 2 Nefi 9:1–26, zingatia kupaka rangi ya aina moja kile ambacho kingetendeka kwetu bila Upatanisho wa Yesu Kristo. Kisha, kwa rangi nyingine tofauti, unaweza kuwekea alama kile tunachoweza kupata kupitia Upatanisho wa Mwokozi. Ni kweli zipi unazogundua kuhusu Upatanisho wa Yesu Kristo zinazokusababisha usifu “hekima ya Mungu, huruma zake na neema”? (2 Nefi 9:8).

Ona pia “Upatanisho wa Yesu Kristo,” Mada za Injili, topics.ChurchofJesusChrist.org.

2 Nefi 9:27–54

Naweza kuja kwa Kristo na kupokea baraka tukufu za Upatanisho Wake.

Yesu Kristo alikuja “ulimwenguni ili awaokoe wanadamu wote kama watakubali sauti yake” (2 Nefi 9:21; msisitizo umeongezwa). Hii ina maana, ni lazima tuwe tayari kukubali baraka za wokozi anazotupatia. Baada ya kufafanua mpango mkuu wa ukombozi, Yakobo alitoa maonyo na mialiko muhimu, inayopatikana katika 2 Nefi 9:27–54, ili kutusaidia kupokea baraka za Upatanisho. Zingatia kuziandika katika chati kama hii hapa:

Maonyo

Mialiko

Maonyo

Mialiko

Maonyo

Mialiko

Unahisi umesukumwa na Roho kufanya nini katika kuitikia maonyo na mialiko hii?

2 Nefi 10:20, 23–25

Kwa sababu ya dhabihu ya Yesu Kristo, naweza “kuchangamsha” moyo wangu.

Ujumbe wa Yakobo ulikuwa wa shangwe. “Nawazungumzia vitu hivi,” alisema, “ili kwamba mshangilie, na muinue vichwa vyenu juu milele” (2 Nefi 9:3). Unaposoma 2 Nefi 10:20, 23–25, ni nini unachokipata kinachokupa tumaini? Ni kipi kingine ambacho umekipata katika 2 Nefi 9–10 ambacho kimekupa tumaini? Utafanya nini ili kukumbuka vitu hivi wakati unahisi kufa moyo?

Ona pia Yohana 16:33.

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia.

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani

Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Haya ni baadhi ya mawazo.

2 Nefi 8:3–7

Unaposoma 2 Nefi 8:3, unaweza ukaonyesha picha za jangwa na bustani. Je, ni kwa jinsi gani Bwana anageuza majangwa ya maisha yetu kuwa bustani? Katika mistari 4–7, ni nini Bwana anatushauri tufanye ili tuweze kupata shangwe iliyoelezewa katika mstari wa 3?

2 Nefi 8:24–25

Ni namna gani maneno ya Isaya yenye kutia moyo kwa watu wa Sayuni yanaweza kutuimarisha katika juhudi zetu za kuwa wafuasi waaminifu wa Yesu Kristo? Ni jinsi gani kuamka na kuvaa nguo kunafanana na kile ambacho Mungu anataka tufanye kiroho?

2 Nefi 9:1–26

Ni nini familia yako inaweza fanya ili iweze kuelewa vizuri zaidi ukubwa wa “upatanisho usio na kipimo” wa Yesu Kristo? (mstari wa 7). Pengine wanaweza kutazama au kufikiri kuhusu vitu ambavyo vinaonekana kutokuwa na kipimo kwa idadi—majani ya nyasi katika kiwanja, chembe za changarawe kwenye ufuo wa bahari, au nyota katika anga. Ni jinsi gani Upatanisho wa Mwokozi hauna kipimo? Ni vifungu gani vya maneno katika 2 Nefi 9 vinasababisha shukrani zetu kuwa za dhati kwa ajili ya kile Mwokozi alichofanya kwa ajili yetu?

2 Nefi 9:27–44

Pengine siku moja wiki hii familia yako inaweza kupekua 2 Nefi 9:27–38, ili kupata maonyo (yanayotanguliwa na “ole”). Ni yapi kati ya haya yanaonekana muhimu hasa kwa familia yako kujadili? Katika siku tofauti, mnaweza kupekua 2 Nefi 9:39–44, kwa ajili ya kujua kile Yakobo aliwaaalika watu wake kukumbuka.

2 Nefi 9:28–29, 50–51

Ni nini baadhi ya mifano ya “Utupu, na ugoigoi, na upumbavu wa wanadamu”? (mstari wa 28). Tunaweza kufanya nini ili kuweka thamani kubwa zaidi kwenye vitu vya Mungu na kidogo kwenye vitu vya ulimwengu.

2 Nefi 9:45

Familia yako inaweza kufurahia kutengeneza mnyororo wa karatasi na kisha kufanya zamu kuuvaa na kujifungua. Ni namna gani dhambi ni kama minyororo? Ni jinsi gani Mwokozi anatusaidia kujifungua minyororo?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Kuwa mwenye kupatikana na kufikika. “Baadhi ya nyakati nzuri zaidi za kufundisha huanza kama swali au wasiwasi katika moyo wa mwana [familia]. … Acha wajue kupitia maneno na matendo yako kwamba una shauku ya kuwasikiliza” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 16).

Picha
Yesu akiwaponya watu

Mwokozi atawaokoa watoto wote wa Mungu “kama watakubali sauti yake” (2 Nefi 9:21). Aliponya Magonjwa Mengi Ya Kila Aina, na J. Kirk Richards

Chapisha