“Nyenzo za Zaida,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)
“Nyenzo za ziada,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2020
Nyenzo za Ziada
Nyenzo hizi zote zinaweza kupatikana katika Gospel Library app na kwenye ChurchofJesusChrist.org.
Nyimbo za kanisa na Kitabu cha Nyimbo za Watoto
Muziki mtakatifu humwalika Roho na hufundisha injili katika njia ya kukumbukwa. Kwa kuongezea kwenye matoleo yaliyochapishwa ya Nyimbo za Kanisa na Kitabu cha Nyimbo za Watoto, unaweza kupata rekodi ya kusikiliza na video ya nyimbo nyingi za Kanisa na nyimbo za watoto kwenye music.ChurchofJesusChrist.org na katika LDS Music app.
Magazeti ya Kanisa
Magazeti ya Friend, New Era, Ensign, na Liahona hutoa hadithi na shughuli ambazo zinaweza kuwa nyongeza za kanuni unazofundisha kutoka katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia.
Hadithi za Kitabu cha Mormoni
Hadithi za Kitabu cha Mormoni zinaweza kuwasaidia watoto kujifunza mafundisho yanayopatikana katika Kitabu cha Mormoni. Unaweza pia kupata video za hadithi hizi katika Gospel Library app na kwenye medialibrary.ChurchofJesusChrist.org.
Vitabu vya Kiada vya Seminari na Chuo
Vitabu vya Kiada vya Seminari na Chuo hutoa historia ya nyuma na mawazo ya kimafundisho kwa kanuni na matukio yanayopatikana katika maandiko.
Maktaba ya Vyombo vya Habari
Kazi ya sanaa, video, na vyombo vingine vya habari vinaweza kukusaidia wewe na familia yako kupata taswira ya mafundisho na hadithi zinazopatikana katika Kitabu cha Mormoni. Tembelea medialibrary.ChurchofJesusChrist.org kupitiapitia mkusanyiko wa nyenzo za vyombo vya habari, ikijumuisha mfululizo wa Video za Kitabu cha Mormoni, ambazo zinaonyesha kwa michoro matukio katika Kitabu cha Mormoni. Media Library pia inapatikana kama app ya simu ya mkononi.
Mada za Injili
Kwenye topics.ChurchofJesusChrist.org unaweza kupata taarifa muhimu kuhusu mada mbali mbali za injili, pamoja na viunganisho kwenye nyenzo za kusaidia, kama vile mahubiri ya mkutano mkuu yanayoshabihiana, makala, maandiko, na video. Unaweza pia kupata Insha za Mada za Injili, ambazo hutoa kwa kina majibu ya maswali ya injili.
Kweli katika Imani
Kama unahitaji msaada zaidi kuelewa kanuni muhimu za injili, fikiria kuangalia kwenye Kweli katika Imani. Nyenzo hii ina orodha ya kialfabeti ya mada za injili zilizoelezewa kwa maneno rahisi.