Njoo, Unifuate
Ahadi za Kinabii


“Ahadi za Kinabii” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Ahadi za Kinabii,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2020

Ahadi za Kinabii

Kujifunza Kitabu cha Mormoni kutakubadili. Kitaibadili familia yako. Manabii wa siku za mwisho wametoa ahadi kuhusu nguvu za Kitabu cha Mormoni tangu Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho liliporejeshwa. Tafakari kauli zifuatazo, na uzifanyie mapitio mara kwa mara. Ni ipi kati ya baraka hizi ungependa kupokea? Unaposoma Kitabu cha Mormoni, zingatia kurekodi na kushiriki na wengine jinsi ahadi hizi zinavyotimizwa maishani mwako.

Nabii Joseph Smith: “Niliwaambia ndugu kwamba Kitabu cha Mormoni kilikuwa kitabu kilicho sahihi kuliko kingine duniani, na jiwe la katikati la teo la dini yetu, na kuwa mwanadamu angemkaribia Mungu zaidi kwa kufuata mafunzo yake, zaidi ya kitabu kinginekitabu kingine” (Mafundisho ya Marais wa Kanisa: Joseph Smith [2007], 64).

Rais Ezra Taft Benson: “Sio tu kwamba Kitabu cha Mormoni hutufunza sisi ukweli, ingawaje kwa kweli hufanya hivyo. Sio tu kwamba Kitabu cha Mormoni hushuhudia juu ya Kristo, ingawaje kwa kweli hufanya hivyo, pia. Lakini kuna kitu zaidi ya hivyo. Kuna uwezo katika kitabu hiki ambao utatiririka katika maisha yako wakati utakapoanza kujifunza kitabu hiki kwa bidii. Utapata uwezo mkuu wa kushinda majaribu. Utapata uwezo wa kuepuka kudanganywa. Utapata uwezo wa kukaa katika njia iliyosonga na nyembamba. Maandiko yanaitwa ‘maneno ya uzima’ (MM 84:85), na hakuna popote palipo na kweli nyingi kuliko ilivyo katika Kitabu cha Mormoni. Utakapoanza kuwa na njaa na kiu ya maneno hayo, utapata uzima kwa wingi mno” (Mafundisho ya Marais wa Kanisa: Ezra Taft Benson [2014], 141).

Rais Gordon B. Hinckley: “Akina kaka na akina dada, bila kusita ninawaahidi kwamba kama mtakisoma Kitabu cha Mormoni kwa maombi, bila ya kujali ni mara ngapi umekisoma hapo awali, kutakuja katika mioyo yenu ongezeko la Roho wa Bwana. Kutakuja mwamko imara kutembea katika utiifu kwa amri zake, na kutatokea ushuhuda imara zaidi wa uhalisia wa uhai wa Mwana wa Mungu” (Mafundisho ya Marais wa Kanisa: GordonB. Hinckley [2016],233).

Rais Russell M. Nelson: “Wapendwa akina kaka na akina dada, ninaahidi kwamba unaposoma kwa maombi Kitabu cha Mormoni kila siku, utafanya maamuzi mazuri—kila siku. Ninaahidi kwamba mnapotafakari kile mnachojifunza, madirisha ya mbinguni yatafunguka, na utapata majibu ya maswali yako na mwongozo wa maisha yako mwenyewe. Ninaahidi kwamba unapozama kila siku kwenye Kitabu cha Mormoni, unaweza kuepushwa dhidi ya maovu ya siku, yakiwemo tauni ya ponografia na uraibu mwingine wenye kuleta kupooza kwa akili” (“Kitabu cha Mormoni: Je, Maisha Yako Yangekuwaje Bila Hicho?Ensign au Liahona, Nov. 2017, 62–63).

Chapisha