“Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)
“Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2020
Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia
Nyenzo Hii Ni Kwa Ajili ya nani?
Nyenzo hii ni kwa ajili ya kila mtu binafsi na familia katika Kanisa. Imetengenezwa ili kukusaidia wewe kujifunza injili—iwe peke yako au na familia yako. Kama hukuwa ukijifunza injili kila mara siku za nyuma, nyenzo hii inaweza kukusaidia kuanza. Kama tayari una mazoea mazuri ya kujifunza injili, nyenzo hii inaweza kukusaidia kuwa na uzoefu mwingi wa maana.
Je, Ni Kwa Namna Gani Ninapaswa Kuitumia Nyenzo Hii?
Tumia nyenzo hii katika njia ambayo ina manufaa kwako. Unaweza kuona ina manufaa kama mwongozo au msaada wa kujifunza maandiko kwako binafsi na kifamilia. Unaweza pia kuitumia kwa jioni ya familia nyumbani. Mihutasari huonyesha kanuni muhimu zinazopatikana ndani ya Kitabu cha Mormoni, hupendekeza mawazo ya kujifunza na shughuli kwa ajili ya watu binafsi na familia, na hutoa sehemu za kuandika mawazo yako.
Wewe na familia yako yawezekana tayari mnajifunza injili kila mara. Kwa mfano, pengine unasoma maandiko tofauti na Kitabu cha Mormoni kwa ajili ya darasa la seminari au chuo. Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia hakikusudiwi kuchukua nafasi au kushindana na mambo mazuri unayofanya. Kunaweza kukawa na njia za kujifunza kutoka kwenye Kitabu cha Mormoni kila mara na bado ukaweza kufikia malengo yako mengine ya kusoma maandiko. Kwa mfano, unaweza kusoma kitabu kimoja cha maandiko kwa kujifunza kwako maandiko kibinafsi na kusoma Kitabu cha Mormoni na familia yako (au kinyume chake). Fuata mwongozo wa Roho ili kuamua jinsi ya kuanza kujifunza kwako mwenyewe neno la Mungu.
Ni Kwa Jinsi Gani Nyenzo Hii Inahusiana na Kile Kinachotokea Kanisani?
Mihutasari katika nyenzo hii imepangwa kulingana na ratiba ya kusoma kila wiki. Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi na Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili zinafuata ratiba sawa. Ili kusaidia juhudi zako za kujifunza na kuishi injili nyumbani, walimu wako kanisani watakupa fursa za kuelezea uzoefu wako, mawazo, na maswali kuhusu vifungu vya maandiko ambavyo umekuwa ukijifunza ukiwa nyumbani.
Kwa sababu Shule ya Jumapili inafundishwa mara mbili tu kwa mwezi, walimu wa Shule ya Jumapili wanaweza wakachagua kuunganisha au kuacha mihutasari ili kuenda pamoja na ratiba ya kila wiki. Hii yaweza pia kuhitajika katika wiki ambapo mikutano ya kawaida ya Kanisa haifanyiki kwa ajili ya mkutano wa kigingi au kwa sababu zinginezo. Katika muda wa wiki hizi unaalikwa kuendelea kujifunza Kitabu cha Mormoni nyumbani.
Je, Ninahitajika kufuata Ratiba?
Ratiba itakusaidia kumaliza kusoma Kitabu cha Mormoni kufikia mwisho wa mwaka. Kwa kuongezea, kufuata ratiba sawa na wengine katika kata yako kunaweza kukaleta uzoefu wa maana kanisani. Lakini usijisikie kufungwa na ratiba; ni mwongozo tu wa kukusaidia kujipima mwenyewe. Kitu cha muhimu ni kwamba unajifunza injili wewe binafsi na kama familia.