Mafundisho na Maagano 2021
Uongofu Ndiyo Lengo Letu


”Uongofu Ndiyo Lengo Letu,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Uongofu Ndiyo Lengo Letu,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2021

Picha
mwanamke akisoma maandiko

Uongofu Ndiyo Lengo Letu

Dhumuni la kujifunza na kufundisha injili ni kuongeza uongofu wetu kwa Yesu Kristo na kutusaidia sisi kuwa zaidi kama Yeye. Kwa sababu hii, tunapojifunza injili, hatutafuti tu taarifa mpya; tunataka kuwa “kiumbe kipya” (2 Wakorintho 5:17). Hii inamaanisha kumtegemea Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo ili watusaidie kubadili mioyo yetu, mitazamo yetu, matendo yetu, na asili yetu hasa.

Lakini aina ya kujifunza injili inayoimarisha imani yetu na kutuongoza kwenye badiliko la kimiujiza la uongofu haitokei yote kwa wakati mmoja. Inakwenda zaidi ya darasani mpaka kwenye moyo wa mtu binafsi na nyumbani. Inahitaji uthabiti, juhudi za kila siku ili kuelewa na kuishi injili. Lakini Baba wa Mbinguni hategemei sisi kufanya hivyo peke yetu—Atamtuma Roho Mtakatifu kutusaidia kuwa waongofu.

Roho Mtakatifu hutuongoza kwenye ukweli na hushuhudia juu ya ukweli huo (ona Yohana 16:13). Yeye huangaza akili zetu, huchochea uelewa wetu, na hugusa mioyo yetu kwa ufunuo kutoka kwa Mungu, chanzo cha ukweli wote. Roho Mtakatifu hutakasa mioyo yetu. Yeye huchochea ndani yetu tamaa ya kuishi katika kweli, na hutunong’onezea njia za kufanya hili. Kwa kweli, “Roho Mtakatifu … atatufundisha [sisi] mambo yote” (Yohana 14:26).

Kwa sababu hizi, katika juhudi zetu za kuishi, kujifunza, na kufundisha injili, lazima kwanza na zaidi ya yote tutafute wenza wa Roho. Lengo hili linapaswa kutawala chaguzi zetu na kuongoza mawazo na matendo yetu. Tunapaswa kutafuta chochote kinachokaribisha ushawishi wa Roho na kukataa chochote kinachofukuza ushawishi huo—kwani tunajua kwamba kama tunaweza kuwa wenye kustahili uwepo wa Roho Mtakatifu, tunaweza pia kustahili kuishi katika uwepo wa Baba wa Mbinguni na Mwanaye, Yesu Kristo.

Chapisha