Agano Jipya 2023
Mei 8–14. Mathayo 19–20; Marko 10; Luka 18: “Nimepungukiwa na Nini Tena?”


“Mei 8–14. Mathayo 19-20; Marko 10; Luka 18: ‘Nimepungukiwa na Nini Tena?’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2023 (2022)

“Mei 8–14. Mathayo 19–20; Marko 10; Luka 18,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2023

Picha
vibarua katika shamba la mizabibu

Mei 8–14

Mathayo 19–20; Marko 10; Luka 18

“Nimepungukiwa na Nini Tena?”

Soma na kutafakari Mathayo 19–20; Marko 10; na Luka 18, ukitilia maanani ushawishi unaopokea. Andika ushawishi huo, na azimia jinsi utakavyoutendea kazi.

Andika Misukumo Yako

Kama ungepata nafasi ya kumuuliza Mwokozi swali, lingekua swali gani? Wakati kijana mmoja tajiri alipokutana na Mwokozi kwa mara ya kwanza, alimuuliza, “nitende jambo gani jema, ili nipate uzima wa milele?” (Mathayo 19:16). Jibu la Mwokozi lilionyesha vyote shukrani kwa mambo mema ambayo kijana tayari amekwisha tenda na kumtia moyo kwa upendo ili afanye zaidi. Tunapotafakari uwezekano wa uzima wa milele, tunaweza pia kujiuliza kama kuna zaidi tunayopaswa kufanya. Tunapouliza, katika njia yetu wenyewe, “Nimepungukiwa na Nini Tena?” (Mathayo 19:20), Bwana anaweza kutupatia majibu ambayo ni ya binafsi kama jibu Lake kwa kijana tajiri. Chochote Bwana anachotutaka tufanye, kufanyia kazi jibu Lake daima kutahitaji tumuamini Yeye zaidi kuliko wema wetu wenyewe (ona Luka 18:9–14) na kwamba “tuupokee ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo” (Luka 18:17; ona pia 3 Nefi 9:22).

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi maandiko

Mawazo kwa Ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Mathayo 19:3–9; Marko 10:2–12

Ndoa kati ya mwanamume na mwanamke imetakaswa na Mungu.

Majibizano haya kati ya Mwokozi na Mafarisayo ni moja kati ya matukio machache yaliyoandikwa ambapo Mwokozi alifundisha mahususi kuhusu ndoa. Baada ya kusoma Mathayo 19:3–9 na Marko 10:2–12, andika orodha ya maelezo kadhaa ambayo unahisi ni muhtasari wa mtazamo wa Mwokozi juu ya ndoa. Kisha jifunze baadhi ya taarifa zinazopatikana katika “Ndoa” katika (Mada za Injili, topics.ChurchofJesusChrist.org), na ongeza kauli zaidi kwenye orodha yako. Je, ni kwa jinsi gani ufahamu wako juu ya mpango wa Baba wa wokovu huathiri jinsi unavyofikiri na kuhisi kuhusu ndoa?

Mathayo 19:3–9; Marko 10:2–12

Je, Yesu alifundisha kwamba talaka kamwe haikubaliki au kwamba watu waliotalikiana wasiingie tena kwenye ndoa?

Katika hotuba juu ya talaka, Rais Dallin H. Oaks alifundisha kwamba Baba wa Mbinguni anakusudia kwamba uhusiano wa ndoa uwe wa milele. Hata hivyo, Mungu pia anaelewa kwamba talaka wakati mwingine inabidi. Rais Oaks alieleza kwamba Bwana “huruhusu watu waliotalikiana kuingia tena kwenye ndoa bila doa la ukosefu wa maadili ulioainishwa katika sheria ya juu. Isipokuwa muumini mtalikiwa amefanya uvunjaji mkubwa wa sheria, anaweza kustahili kibali cha hekaluni chini ya viwango vya ustahili vinavyotumika kwa waumini wengine” (“Talaka,” Liahona, Mei 2007, 70).

Mathayo 19:16–22; Marko 10:17–22; Luka 18:18–23

Kama nikimwomba Bwana, atanifundisha ninachohitajika kufanya ili kuurithi uzima wa milele.

Hadithi ya kijana tajiri inaweza kuleta kusita hata kwa mfuasi mwaminifu, wa maisha yote. Unaposoma Marko 10:17–22, unapata ushahidi gani wa uaminifu na unyofu wa kijana? Ni kwa jinsi gani Bwana alijisikia juu ya kijana huyu?

Hadithi hii inaweza kukufanya uulize, “Nimepungukiwa na Nini Tena?” (Mathayo 19:20). Ni kwa jinsi gani Bwana hutusaidia kufidia kwa yale tunayopungukiwa? (ona Etheri 12:27). Ni nini tunaweza kufanya ili kujiandaa kupokea ukosoaji Wake na msaada tunapotafuta kujiboresha?

Ona pia Larry R. Lawrence, “Nimepungukiwa na Nini Tena?,” Liahona, Nov. 2015, 33–35; S. Mark Palmer, “Kisha Yesu Akamtazama Akampenda,” Liahona, Mei 2017, 114–16.

Mathayo 20:1–16

Kila mmoja anaweza kupokea baraka ya uzima wa milele, bila kujali lini wameikubali injili.

Je, unaweza kujilinganisha na uzoefu wa yeyote kati ya watendakazi katika shamba la mizabibu? Ni masomo gani unapata kwa ajili yako katika kifungu hiki? Ujumbe wa Mzee Jeffrey R. Holland “Wakulima katika Shamba la Mizabibu” (Liahona, Mei 2012, 31–33) unaweza kukusaidia kuona njia mpya za kutumia fumbo hili. Je, ni ushawishi gani wa ziada Roho anaokupatia?

Picha
mtu mnyenyekevu na Mfarisayo

Mtoza Ushuru Anayetubu na Mfarisayo Anayejifanya Mwenye Haki wakiwa Hekaluni, na Frank Adams

Luka 18:9–14

Ninapaswa kutumainia rehema za Mungu, sio kwa haki zangu wenyewe.

Je! Unawezaje kufanya muhtasari wa tofauti kati ya sala mbili hizi katika fumbo hili? Tafakari kile unachohisi unapaswa kufanya ili kuwa zaidi kama mtoza ushuru katika hadithi hii na si kuwa kama Mfarisayo.

Ona pia Wafilipi 4:11–13; Alma 31:12–23; 32:12–16.

Picha
ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Marko 10:13–16; Luka 18:15–17.Ili kuwasaidia wanafamilia kutafakari hadithi katika mistari hii, mnaweza kuimba pamoja wimbo unaohusiana, kama vile “I Think When I Read That Sweet Story” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 56). Ingekuwaje kuwa miongoni wa watoto ambao Yesu aliwabariki? Inamaanisha nini “kupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo”? (Marko 10:15).

Marko 10:23–27.Je, nini tofauti kati ya kuwa na utajiri na kutumaini katika utajiri? (ona Marko 10:23–24). Unaposoma mstari wa 27, unaweza kutaka kuonyesha Tafsiri ya Joseph Smith: “Kwa watu wanaotumaini katika utajiri, haiwezekani; lakini sivyo kwa watu wanaomtumaini Mungu na kuacha vyote kwa ajili yangu, kwani kama hao mambo yote haya yanawezekana” (katika Tafsiri ya Joseph Smith, Marko 10:27, tanbihi a). Kama familia, Je, ni kwa jinsi gani tunaonesha kwamba tunamtumaini Mungu kuliko vitu”?

Mathayo 20:1–16.Ili kuonyesha kanuni zilizopo katika Mathayo 20:1–16, unaweza kufanya shindano rahisi, kama vile mbio fupi. Baada ya kila mtu kumaliza shindano, mzawadie kila mmoja zawadi inayofanana, ukianzia na aliyemaliza mwisho na kumalizia na aliyemaliza wa kwanza. Je, hii inatufundisha nini kuhusu anayepokea baraka ya uzima wa milele katika mpango wa Baba wa Mbinguni?

Mathayo 20:25–28; Marko 10:42–45..Je, nini maana ya kirai hiki “na mtu yeyote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu”? (Mathayo 20:27). Je, ni kwa jinsi gani Yesu Kristo alionyesha mfano wa kanuni hii? Je, ni kwa jinsi gani sisi tunaweza kufuata mfano Wake katika familia zetu, kata au tawi letu, na ujirani wetu?

Luka 18:1–14.Je, tunajifunza nini kuhusu sala kutoka kwenye haya mafumbo wawili katika mistari hii?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “Dearest Children, God Is Near You,” Nyimbo za Kanisa, na. 96.

Kuboresha Kujifunza Binafsi

Tafuta muda ambao unafaa kwako. Ni rahisi kila mara kujifunza pale unapoweza kusoma maandiko bila kubugudhiwa. Tafuta muda ambao unafaa kwako, na fanya kadiri uwezavyo kuwa na uthabiti wa kujifunza katika muda ule ule kila siku.

Picha
Kristo na kijana tajiri

Kristo na Kijana Tajiri Mtawala, na Heinrich Hofmann

Chapisha