Agano Jipya 2023
Mei 22–28. Joseph Smith—Mathayo 1; Mathayo 24–25; Marko 12–13; Luka 21: “Mwana wa Adamu Atakuja”


“Mei 22–28. Joseph Smith—Mathayo 1; Mathayo 24–25; Marko 12–13; Luka 21: ‘Mwana wa Adamu Atakuja’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya (2023)

“Mei 22–28. Joseph Smith—Mathayo 1; Mathayo 24–25; Marko 12–13; Luka 21” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2023

Picha
Ujio wa Pili

Ujio wa Pili, na Harry Anderson

Mei 22–28

Joseph Smith—Mathayo 1; Mathayo 24–25; Marko 12–13; Luka 21

“Mwana wa Adamu Atakuja”

Unaposoma Joseph Smith—Mathayo 1; Mathayo 24–25; Marko 12–13; na Luka 21, unaweza kujiuliza, “ni ujumbe gani sura hizi zinao kwa ajili yangu mimi? kwa ajili ya familia yangu? kwa ajili ya wito wangu?”

Andika Misukumo Yako

Wanafunzi wa Yesu lazima waliona unabii Wake kuwa wa kushtusha: hekalu kuu la Yerusalemu, kitovu cha mambo ya kiroho na kiutamaduni cha Wayahudi, lingeharibiwa kabisa kiasi kwamba “kusingesalia … jiwe juu ya jiwe.” Kiuhalisia wanafunzi walitaka kujua zaidi. “Je, mambo haya yatakuwa lini?” waliuliza. “Na ni nini dalili ya kuja kwako” (Joseph Smith—Mathayo 1:2–4). Majibu ya Mwokozi yalifunua kwamba angamizo kuu litakalokuja kwa Yerusalemu—unabii uliotimizwa mnamo miaka 70 B.K—kwa kiasi fulani lingekuwa dogo ikilinganishwa na dalili za kuja Kwake katika siku za mwisho. Vitu ambavyo huonekana thabiti hata kuliko hekalu katika Yerusalemu vitathibitisha kuwa vya muda mfupi—jua, mwezi, nyota, mataifa, na bahari. Hata “nguvu za mbingu zitatikiswa” (Joseph Smith—Mathayo 1:33). Kama tuko macho kiroho, ghasia hii inaweza kutufundisha kuweka matumaini yetu katika kitu ambacho kweli ni cha kudumu. Kama Yesu alivyoahidi, “Mbingu na dunia zitapita; lakini maneno yangu hayatapita. … Na yeyote mwenye kuyahifadhi katika hazina maneno yangu, hatadanganyika” (Joseph Smith—Mathayo 1:35, 37).

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa Ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Joseph Smith—Mathayo ni nini?

Joseph Smith—Mathayo, ipo ndani ya Lulu ya Thamani Kuu, ni Tafsiri ya Joseph Smith ya mstari wa mwisho wa Mathayo 23 na mistari yote katika Mathayo 24. Masahihisho ya Joseph Smith yenye mwongozo wa kiungu hurejesha kweli za thamani ambazo zilikuwa zimepotea Mistari 12–21 inahusu maangamizo ya kale ya Yerusalemu; mistari 21–55 ina unabii kuhusu siku za mwisho.

Joseph Smith—Mathayo1:21–37; Marko 13:21–37; Luka 21:25–38

Unabii kuhusu Ujio wa Pili wa Mwokozi unaweza kunisaidia kuukabili wakati ujao kwa imani.

Inaweza kuwa ya kutia wasiwasi kusoma kuhusu matukio kuelekea Ujio wa Pili wa Yesu Kristo. Lakini Yesu alipotoa unabii wa matukio haya, Aliwaambia wanafunzi Wake “msifadhaike” (Joseph Smith—Mathayo 1:23). Je, ni kwa jinsi gani unaweza “kutofadhaika” unaposikia kuhusu matetemeko, vita, uongo, na njaa? Fikiria kuhusu swali hili unaposoma mistari hii. Wekea alama au andika ushauri wowote wa hakikisho jipya unalopata.

Ona pia Mada za Injili, “Ujio wa Pili wa Yesu Kristo,” topics.ChurchofJesusChrist.org.

Joseph Smith—Mathayo 1:26–27, 38–55; Mathayo 25:1–13; Luka 21:29–36

Lazima niwe tayari daima kwa Ujio wa Pili wa Mwokozi.

Mungu hajafunua “siku wala saa atakapokuja Mwana wa Adamu” (Mathayo 25:13). Lakini hataki siku hiyo ije kwetu “ghafla” (Luka 21:34), hivyo ametupatia ushauri kuhusu jinsi ya kujiandaa.

Unaposoma mistari hii, tambua mafumbo na mifanano mingine ambayo Mwokozi aliitumia kutufundisha kuwa daima tujiandae kwa Ujio Wake wa Pili. Je, unajifunza nini kutoka mistari hiyo? Je, unashawishika kufanya nini?

Unaweza kufikiria pia jinsi Mwokozi anavyokutaka usaidie kuundaa ulimwengu kwa ajili ya Ujio Wake wa Pili. Unahisi inamaanisha nini kuwa tayari kumpokea Mwokozi wakati Yeye anapokuja? Ujumbe wa Mzee D. Todd Christofferson “Kujiandaa kwa ajili Kurudi kwa Bwana” (Liahona, Mei 2019, 81–84) unaweza kukusaidia kutafakari hili.

Ona pia Russell M. Nelson, “Kumbatia Siku za Usoni kwa Imani,” Liahona, Nov. 2020, 73-76.

Mathayo 25:14–30

Baba wa Mbinguni anategemea nitumie zawadi Zake kwa busara.

Katika fumbo la Mwokozi, “talanta” ilimaanisha pesa. Lakini fumbo la talanta linaweza kutusukuma tutafakari jinsi tunavyotumia baraka zetu, si tu pesa. Unaposoma fumbo hili, ungeweza kutengeneza orodha ya baadhi ya baraka na fursa ambazo Baba wa Mbinguni amekukabidhi. Je, Yeye anatarajia ufanye nini na baraka hizi? Je, ni kwa jinsi gani unaweza kuzitumia zawadi hizi kwa busara zaidi?

Mathayo 25:31–46

Ninapowatumikia wengine, Ninamtumikia Mungu.

Ikiwa unajiuliza ni kwa jinsi gani Bwana atayahukumu maisha yako, soma fumbo la kondoo na mbuzi. Kwa nini unafikiria kutunza wenye mahitaji kutakusaidia kujiandaa “kuurithi ufalme” wa Mungu?

Ni kwa jinsi fumbo hili ni sawa na yale mengine mawili katika Mathayo 25? Je, ni jumbe zipi zinafanana katika mafumbo haya matatu?

Ona pia Mosia 2:17; 5:13.

Picha
ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Joseph Smith—Mathayo.Ili kuisaidia familia yako kutafiti sura hii, waalike watafute mafundisho ya Mwokozi kuhusu jinsi tunavyoweza kujiandaa kwa Ujio Wake wa Pili (ona, kwa mfano, mstari wa 22–23, 29–30, 37, 46–48). Je, tunaweza kufanya nini ili kufuata ushauri huu? Familia yako ingeweza kufurahia kuimba “When He Comes Again” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 82–83) na kuchora picha za vile wanavyodhani Ujio wa Pili utakuwa.

Joseph Smith—Mathayo 1:22, 37.Je, inamaanisha nini kuyahifadhi katika hazina maneno ya Mungu? Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kufanya hili kama watu binafsi na kama familia? Je, ni kwa jinsi gani kufanya hivyo kutatusaidia kuepuka kudanganywa?

Mathayo 25:1–13.Unaweza kutumia picha ya wanawali kumi ambayo huambatana na muhtasari huu kujadili Mathayo 25:1–13. Je, ni maelezo gani ya kina tunayaona katika picha hii ambayo yanaelezewa katika mistari hii?

Unaweza kukata karatasi katika umbo la matone ya mafuta na kuyaficha matone nyumbani mwenu. Unaweza kushikisha matone kwenye vitu kama vile maandiko au picha ya hekalu. Wakati wanafamilia wanapoyapata matone haya, mngeweza kujadili jinsi vitu hivi vinavyotusaidia kujiandaa kwa Ujio wa Pili.

Marko 12:38–44; Luka 21:1–4.Mistari hii inafundisha nini kuhusu jinsi Mwokozi anavyoyaona matoleo yetu? Waonyeshe familia yako jinsi ya kulipa zaka na matoleo kwa Bwana. Ni kwa jinsi gani matoleo haya hutusaidia kujenga ufalme wa Mungu? Ni zipi baadhi ya njia tunazoweza kutoa matoleo “yale yote [tuliyonayo]” kwa Bwana? (Marko 12:44).

Picha
mwanamke akiweka sarafu ndani ya sanduku

Senti ya Mjane, na Sandra Rast

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa “When He Comes Again,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 82–83.

Kuboresha Kujifunza Binafsi

Andaa Mazingira yako. “Mazingira yetu kwa kiasi kikubwa yanaweza kuathiri uwezo wetu wa kujifunza na kuhisi ukweli” (Kufundisha Katika Njia ya Mwokozi15). Jaribu kutafuta mahali pa kujifunza maandiko ambapo pataalika ushawishi wa Roho Mtakatifu. Muziki wenye kutia moyo na picha vinaweza pia kumwalika Roho.

Picha
wanawake wameshikilia taa za mafuta

Watano kati Yao Walikuwa wenye Busara, na Walter Rane

Chapisha