“Novemba 13–19. Yakobo: ‘Iweni Watendaji wa Neno, wala Si Wasikiaji Tu’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2023 (2022)
“Novemba 13–19. Yakobo,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2023
Novemba 13–19
Yakobo
“Iweni Watendaji wa Neno, Wala Si Wasikiaji Tu”
Unaposoma Waraka wa Yakobo, tilia maanani virai vinavyojitokeza kwako. Je, ni kwa jinsi gani unashawishika kuwa “mtendaji” wa maneno haya? ((Yakobo 1:22).
Andika Misukumo Yako
Wakati mwingine mstari mmoja tu wa maandiko unaweza kuubadilisha ulimwengu. Yakobo 1:5 huonekana kama sehemu ndogo rahisi ya ushauri—ukihitaji hekima, omba dua kwa Mungu. Lakini wakati Joseph Smith wa miaka-14 aliposoma mstari huo, “ulionekana kuingia kwa nguvu kubwa katika kila hisia ya moyo [wake]” (Joseph Smith—Historia ya 1:12). Basi kwa mwongozo wa kiungu, Joseph alifanyia kazi ushauri wa Yakobo na kutafuta hekima kutoka kwa Mungu kupitia sala. Na Mungu kwa hakika alitoa kwa ukarimu, akimpa Joseph mojawapo ya matembezi ya kimbingu ya kusifika katika historia ya mwanadamu—Ono la Kwanza. Ono hili lilibadilisha mwenendo wa maisha ya Joseph na kuongoza kwenye Urejesho wa Kanisa la Yesu Kristo duniani. Sisi wote tumebarikiwa leo kwa sababu Joseph Smith alisoma na kufanyia kazi Yakobo 1:5.
Je, utapata nini unapojifunza Waraka wa Yakobo? Pengine mstari mmoja au miwili itakubadilisha wewe au mtu unayempenda. Unaweza kupata mwongozo unapotafuta kutimiza misheni yako katika maisha. Unaweza kupata kutiwa moyo kuzungumza kwa ukarimu au kuwa mvumilivu zaidi. Unaweza kusukumwa kufanya matendo yako yafungamane vyema na imani yako. Chochote kinachokushawishi, ruhusu maneno haya “yaingie … katika kila hisia ya moyo [wako].” Na kisha, wakati wewe “unapopokea kwa upole … neno,” kama Yakobo alivyoandika, iweni watendaji wa neno, sio wasikiaji tu (ona Yakobo 1:21–22).
Mawazo kwa Ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko
Yakobo alikuwa nani?
Kwa ujumla inaaminika kwamba mwandishi wa Waraka wa Yakobo alikuwa mwanawe Mariamu, mama wa Yesu Kristo, kwa hivyo huyu ni kaka wa kambo wa Mwokozi. Yakobo ametajwa katika Mathayo 13:55; Marko 6:3; Matendo ya Mitume 12:17; 15:13; 21:18; na Wagalatia 1:19; 2:9. Inaonekana kutoka katika maandiko haya kwamba Yakobo alikuwa kiongozi wa Kanisa katika Yerusalemu na alikuwa ameitwa kama Mtume (ona Wagalatia 1:19).
Kustahimili katika uvumilivu hutuongoza kwenye ukamilifu.
Baada ya kusoma Yakobo 1:2–4; 5:7–11, je, unaweza kusema ujumbe mkuu wa Yakobo kuhusu uvumilivu ulikuwa nini? Ingeweza kusaidia kutafakari kile familia ya Mzee Jeremy R. Jaggi ilichojifunza kuhusu subira kutoka kwenye mistari hii (ona “Subira na Iwe na Kazi Kamilifu, na Hesabuni ya Kuwa ni Shangwe Tupu!,” Liahona, Nov. 2020, 99–101). Je, “kazi kamilifu” ya subira ni nini? (Yakobo 1:4). Je, ni kwa jinsi gani unaweza kumuonyesha Bwana kwamba uko radhi kuwa mvumilivu?
Yakobo 1:3–8, 21–25; 2:14–26; 4:17
Imani huhitaji matendo.
Je, ni kwa jinsi gani wewe unajua kama una imani katika Yesu Kristo? Je, ni kwa jinsi gani matendo yako huonyesha imani yako kwa Mungu? Fikiria kuhusu maswali haya unapojifunza mafundisho ya Yakobo kuhusu imani. Inaweza kuwa ya kuvutia pia kusoma kuhusu Ibrahimu na Rahabu, mifano miwili iliyotajwa na Yakobo (ona Mwanzo 22:1–12; Yoshua 2). Je, ni kwa jinsi gani wao walionyesha kwamba walikuwa na imani katika Mungu?
Kusoma Yakobo 1:3–8, 21–25; 2:14–26; 4:17 kunaweza kukusaidia kufikiria njia za kuweza kuwa mtendaji mzuri wa neno. Andika misukumo yoyote unayopokea, na uweke mipango ya kuifanyia kazi.
Ona pia Alma 34:27–29; 3 Nefi 27:21.
Maneno ninayozungumza yana nguvu ya kuwaumiza au kuwabariki wengine.
Miongoni mwa matumizi mengi ya tamathali za semi Yakobo alizotumia kote katika waraka wake, baadhi ya lugha yake dhahiri kabisa inapatikana katika ushauri wake kuhusu lugha. Fikiria kutengeneza orodha ya njia zote Yakobo alizouelezea ulimi au mdomo. Je, ni nini kila linganisho au picha hupendekeza kuhusu maneno tunayozungumza? Fikiria juu ya kitu unachoweza kufanya ili kumbariki mtu kwa maneno yako (ona Mafundisho na Maagano 108:7).
Kama mfuasi wa Yesu Kristo, ninapaswa kuwapenda watu wote, bila kujali hali zao.
Yakobo aliwaonya Watakatifu hususani dhidi ya kuwapendelea matajiri na kuwadharau maskini, lakini onyo lake linaweza kutumika kwa upendeleo wowote au chuki tunayoweza kuwa nayo kwa wengine. Kwa sala unapojifunza Yakobo 2:1–9, jichunguze mwenyewe moyoni mwako na sikiliza ushawishi wa Roho Mtakatifu. Inaweza kuwa yenye msaada kubadilisha virai katika mistari hii, kama vile “maskini, mwenye mavazi mabovu” (mstari wa 2), kwa maneno au virai ambavyo vinamwelezea mtu ambaye ungeweza kujaribiwa kumhukumu pasipo haki. Je, unahisi mabadiliko yoyote unayohitaji kufanya juu ya jinsi unavyowachukulia wengine au kuwafikiria wengine?
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani
-
Yakobo 1:5.Baada ya kusoma Yakobo 1:5, familia yako ingeweza kufupisha maelezo ya Ono la Kwanza (ona Joseph Smith—Historia ya 1:8–20, au kutazama video “Ask of God: Joseph Smith’s First Vision” (ChurchofJesusChrist.org). Waalike wanafamilia kushiriki shuhuda zao juu ya Nabii Joseph Smith na uzoefu ambapo Baba wa Mbinguni alijibu sala zao.
6:35 -
Yakobo 1:26–27.Fikiria kutazama video “True Christianity” (ChurchofJesusChrist.org). Kisha soma maana ya maelezo ya Yakobo ya dini safi katika Yakobo 1:26–27, na jadili njia ambazo familia yako inaweza kufanya utekelezaji wa dini safi zaidi.
-
Yakobo 3.Yakobo 3 hujumuisha taswira nyingi ambazo zinaweza kushawishi somo la vitendo la kukumbukwa ili kuisaidia familia yako kukumbuka kuzungumza kwa ukarimu. Kwa mfano, mngeweza kukoka moto pamoja na kuzungumza kuhusu jinsi neno dogo, lisilo la ukarimu linavyoweza kuleta shida kubwa (ona mstari wa 5–6). Au ungeweza kuandaa kitu kichachu katika kitu ambacho kwa kawaida hutumika kwa chakula kitamu—kama vile juisi ya limao ndani ya chupa ya asali. Hii ingeweza kuwapeleka kwenye mjadala kuhusu kutumia maneno mazuri na yenye kuinua (ona mistari 9–14).
-
Yakobo 4:5-8.Kwa nini “tusogee karibu na Mungu” (Yakobo 4:8) tunapokabiliwa na majaribu?
-
Yakobo 5:14–16.Rais Dallin H. Oaks alifundisha kwamba “wazazi wanapaswa kuhimiza kuwa na baraka zaidi za ukuhani katika familia” (“Nguvu za Ukuhani,” Liahona, Mei 2018, 67). Pengine kusoma Yakobo 5:14–16 na kushiriki uzoefu kuhusu kupokea baraka za ukuhani kungeweza kuhimiza wanafamilia kuomba baraka wanapougua au wanapohitaji nguvu za kiroho.
Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.
Wimbo uliopendekezwa: “Have I Done Any Good?,” Nyimbo za Kanisa, na. 223.