Agano Jipya 2023
Desemba 11–17. Ufunuo 6–14: “Nao Wakamshinda … kwa Damu ya Mwana-Kondoo”


“Desemba 11–17. Ufunuo 6–14: ‘Nao Wakamshinda … kwa Damu ya Mwana-Kondoo’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2023 (2022)

“Desemba 11–17. Ufunuo 6–14,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2023

Picha
Yesu amesimama miongoni mwa nyota

Sanaa changamani na Eric Johnson: Baraza Kuu, na Robert Barrett; kundi la nyota kwa hisani ya European Space Agency

Desemba 11–17

Ufunuo wa Yohana 6-14

“Nao Wakamshinda … kwa Damu ya Mwana-Kondoo”

Rais Boyd K Packer alishauri: “Kama lugha ya maandiko mwanzoni inaonekana ngeni kwako, endelea kusoma. Punde utakuja kugundua uzuri na nguvu zinazopatikana kwenye hizo kurasa” (“Ufunguo wa Ulinzi wa Kiroho,” Liahona, Nov. 2013, 27).

Andika Misukumo Yako

Fikiria mwanamke “hali ana utungu na kuumwa katika kuzaa.” Sasa fikiria “joka kubwa jekundu, likiwa na vichwa saba na pembe kumi” likimzunguka mwanamke, likisimama “ili azaapo amle mtoto wake” (Ufunuo 12:2–4). Ili kuelewa mistari hii ya ufunuo wa Yohana, kumbuka kwamba taswira hizi huwakilisha Kanisa na ufalme wa Mungu na hatari ambazo wangekabiliana nazo. Kwa Watakatifu ambao walipitia matukio ya mateso makali katika siku za Yohana, ushindi dhidi ya uovu yaweza kuwa haikuonekana kuwezekana. Ushindi huu pia unaweza kuwa mgumu kutabiri katika siku kama yetu, wakati adui anapokuwa “vitani na watakatifu” na ana “nguvu … juu ya jamaa zote, na ndimi, na mataifa” (Ufunuo 13:7). Lakini mwisho wa ufunuo wa Yohana kwa utukufu unaonyesha kwamba wema utashinda dhidi ya uovu. Babeli itaanguka. Na Watakatifu watatoka “katika dhiki ile iliyo kuu” wakiwa na mavazi meupe—sio kwa sababu mavazi yao kamwe hayakuwa na madoa bali kwa sababu Watakatifu “nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo” (Ufunuo 7:14).

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa Ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Ufunuo 6–11

Yohana aliona matukio mengi ya historia ya dunia, hasa yale ya siku za mwisho.

Katika sura hizi utasoma kuhusu kitabu kilicho na mihuri saba. Kama unajiuliza hiyo inamaanisha nini, wewe hauko peke yako. Nabii Joseph Smith alifanya hivyo pia. Bwana alimfunulia Joseph kwamba kitabu hiki na mihuri yake huwakilisha hadithi ya “kipindi cha muda” cha ulimwengu, kwa kila mhuri ukiwakilisha miaka elfu moja (ona Mafundisho na Maagano 77:6–7). Ungeweza kuvutiwa kujua kwamba matukio ya mihuri minne ya kwanza yamefanyiwa mhutasari katika ono la Yohana kwa mistari minane tu (Ufunuo 6:1–8). Mistari mitatu inayofuata inaelezea mhuri wa tano (mistari 9–11). Matukio ya mihuri mwili ya mwisho yanachukuwa karibu kitabu chote cha Ufunuo. Kwa maneno mengine, fokasi kubwa ya ono la Yohana ni siku za mwisho—siku zetu. Unaposoma, tafakari kwa nini kuna thamani kujua kile Yohana alichoandika kuhusu siku za mwisho.

Unaposoma kuhusu matukio Yohana aliyoyatolea unabii, fikiria mapendekezo na maswali yafuatayo.

Ufunuo 12–13

Ile Vita ya Mbinguni inaendelea duniani.

Hatujui mengi kuhusu Vita ya Mbinguni, lakini kuna maelezo yake ya wazi ingawa mafupi katika Ufunuo 12:7–11. Unaposoma mistari hii, jitazame wewe mwenyewe kama sehemu ya mapigano yale kabla ya kuja duniani. Unajifunza nini kuhusu jinsi Shetani anavyoshindwa? (ona mstari wa 11).

Hii vita ambayo ilianza mbinguni inaendelea duniani, Shetani anang’ang’ania “kufanya vita na [wale ambao] wana ushuhuda juu ya Yesu Kristo” (Ufunuo 12:17). Je, unajifunza nini kutoka Ufunuo 13 kuhusu jinsi yeye anavyovipiga vita hivyo leo? Ni kwa jinsi gani “damu ya Mwanakondoo” na “neno la ushuhuda [wako]” (Ufunuo 12:11) vinaendelea kukusaidia katika vita hii?

Ona pia 1 Nefi 14:12–14; Moroni 7:12–13; Musa 4:1–4; Mafundisho na Maaano 29:36–37; Mada za Injili, “Vita Mbinguni,” topics.ChurchofJesusChrist.org.

Ufunuo 14:6–7

“Nikaona malaika mwingine … mwenye injili ya milele.”

Utimizwaji mmoja wa unabii huu ilio katika mistari hii ulitokea wakati Moroni alipomtokea Joseph Smith na kumuongoza kwenye kumbukumbu ambazo alizitafsiri na kuzichapisha kama Kitabu cha Mormoni. Kitabu hiki kina “injili ya milele” ambayo sisi tumepewa jukumu la kuihubiri kwa “kila taifa, na kabila, na lugha, na jamaa” (Ufunuo 14:6).

Ili kujifunza kuhusu malaika wengine ambao walishiriki katika kurejesha injili ya milele, ona Mafundisho na Maagano 13; 27:5–13; 110:11–16; 128:20–21).

Ona pia “Kumbukizi ya Miaka Mia Mbili ya Urejesho wa Utimilifu wa Injili ya Yesu Kristo: Tangazo kwa Ulimwengu,” ChurchofJesusChrist.org.

Picha
ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Ufunuo 7:9,13–15.Je, mistari hii inaweza kutufundisha nini kuhusu kwa nini tunavaa mavazi meupe kwa ajili ya ibada za ubatizo na hekaluni?

Ufunuo 7:14–17.Fikiria kuwaalika wanafamilia kuelezea hisia zao kuhusu ahadi za Bwana katika mistari hii. Ni kwa jinsi gani ahadi Zake hutusaidia tunapokuwa katika “dhiki ile iliyo kuu”? (mstari wa 14).

Ufunuo 12:7–11; 14:6.Baadhi ya wanafamilia wangeweza kufurahia kuchora picha za maono yaliyoelezewa katika Ufunuo. Kwa mfano, kuchora picha kulingana na Ufunuo 12 kunaweza kuwaongoza kwenye mijadala kuhusu Vita Mbinguni (ona mstari wa 7–11). Picha kulingana na Ufunuo 14:6 zinaweza kuwaongoza kwenye mijadala kuhusu Urejesho wa injili.

Baada ya kusoma Ufunuo 14:6 kwa pamoja, fikiria kuonyesha picha za malaika Moroni na za malaika wengine ambao walisaidia kurejesha injili katika siku yetu (ona picha mwisho wa muhtasari huu.) Pengine wanafamilia wangeweza kufanya zamu kushikilia mojawapo ya picha na kuelezea sababu za kuwa na shukrani kwamba malaika hao walikuja “wakiwa na injili ya milele ili kutuhubiria [sisi].”

Ufunuo 12:11.Kirai “neno la ushuhuda wao” kinaweza kinamaanisha nini? Je, ni kwa jinsi gani shuhuda zetu juu ya Yesu Kristo hutusaidia sisi na wengine kumshinda Shetani?

Ufunuo 13:11–14.Je, ni mawazo gani wanafamilia wako wanayo kuhusu mnyama mdanganyifu? Je, ni kwa jnsi gani tunagundua na kuepukana na uongo tunaouona ulimwenguni leo?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa “I Will Be Valiant,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto,162.

Kuboresha Kujifunza Binafsi

Jizamishe mwenyewe katika maandiko. Rais Russell M. Nelson alifundisha, “Kuzama kila siku kwenye neno la Mungu ni muhimu kwa uhai wa kiroho, hasa katika siku hizi za ongezeko la mabadiliko ya ghafla (“Msikilize Yeye,” Liahona, Mei 2020, 89). “Kuzama kwenye neno la Mungu” kunamaanisha nini kwako?

Picha
Kristo akibisha mlangoni

Kuzunguka kutoka juu kushoto: Moroni Akilete Mabamba ya Dhahabu, na Gary L. Kapp; Juu Yenu Ninyi Watumishi Wenzangu, na Linda Curley Christensen na Michael T. Malm (Yohana Mbatizaji anatunuku Ukuhani wa Haruni juu ya Joseph Smith); Funguo za Ufalme, na Linda Curley Christensen na Michael T. Malm (Petro, Yakobo, na Yohana wanatunuku Ukuhani wa Melkizedeki juu ya Joseph Smith; Ono katika Hekalu la Kirtland, na Gary E. Smith (Musa, Elia, na Eliya wanawatokea Joseph Smith na Sidney Rigdon).

Chapisha