Agano Jipya 2023
Desemba 18–24. Krismasi: “Habari Njema ya Furaha Kuu”


“Desemba 18–24. Krismasi: ‘Habari Njema ya Furaha Kuu’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2023 (2022)

“Desemba 18–24. Krismasi,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2023

Picha
mtoto mchanga

Mwanakondoo Mdogo, na Jenedy Paige

Desemba 18–24

Krismasi

“Habari Njema ya Furaha Kuu”

Fikiria jinsi gani kutafakari kuzaliwa kwa Mwokozi kunaweza kuleta roho ya amani na utakatifu kwa msimu wa Krismasi.

Andika Misukumo Yako

Kwa nini kuzaliwa kwa mtoto kunaleta furaha kuu kama hiyo? Labda kwa sababu mtoto mpya anaweza kuwa ishara ya matumaini. Kuna kitu kuhusu maisha mapya kabisa yaliyojaa uwezekano ambayo hutualika kutafakari maisha yanaweza kubeba nini kwa yule mtoto na mambo gani mazuri atakayofanikisha. Kamwe hili halijawahi kuwa kweli kuliko wakati wa kuzaliwa kwa Mwana wa Mungu, Yesu Kristo. Kamwe hakujawahi kuwa na tumaini la juu kabisa kuwekwa kwa mtoto, na kamwe hakujawahi kuwa na yeyote aliyezaliwa na ahadi nyingi.

Wakati malaika alipowaalika wachungaji kumtafuta mtoto mchanga aliyezaliwa ndani ya hori, aliwapa pia ujumbe kuhusu mtoto yule. Ulikuwa ujumbe wa matumaini—kwamba mtoto huyu alikuja duniani kutimiza misheni takatifu. Wachungaji walifanya ujumbe wao “kujulikana kila mahali … na wote waliousikia walistaajabu juu ya mambo hayo ambayo yalisemwa kwao na wale wachungaji. Lakini Mariamu aliyatunza mambo haya yote, na kuyatafakari moyoni mwake” (Luka 2:17–19). Pengine ingekuwa vizuri kufuata mfano wa Mariamu Krismasi hii: kutafakari moyoni mwako mambo uliyojifunza kuhusu Mwokozi mwaka huu. Ni kwa jinsi gani alitimiza misheni Yake ya ukombozi katika maelezo uliyosoma? Na muhimu zaidi, ni kwa jinsi gani wito Wake umebadilisha maisha yako? Kisha ungeweza kuhisi kushawishika kufuata mfano wa wachungaji: ni kwa jinsi gani wewe utafanya “ijulikane kote” kwa yale ambayo Yesu Kristo amekufanyia?

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa Ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Mathayo 1:18–25; 2:1–12; Luka 1:26–38; 2:1–20

Yesu Kristo alijishusha hadhi kwa kuzaliwa miongoni mwetu duniani.

Hata kama umesoma au kusikia hadithi ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo mara nyingi kabla, jifunze wakati huu ukiwa na wazo hili akilini: Krismasi siyo tu sherehe ya jinsi gani Yesu alikuja ulimwenguni bali pia ya kujua Yeye ni nani—Bwana na Mwokozi wetu, Yesu Kristo—na kwa nini alikuja” (Craig C. Christensen, “Utimilifu wa Hadithi ya Krismasi” [ibada ndogo ya Krismasi ya Urais wa Kwanza, Des. 4, 2016], broadcasts.ChurchofJesusChrist.org).

Ni nini unachojua kuhusu Yesu Kristo alikuwa nani kabla ya Yeye kuzaliwa? (ona, kwa mfano, Yohana 17:5; Mosia 3:5; Mafundisho na Maagano 76:13–14, 20–24; Musa 4:2). Ni kwa jinsi gani ufahamu huu huathiri jinsi unavyohisi unaposoma kuhusu kuzaliwa Kwake?

Je, unafahamu nini kuhusu kwa nini Yesu Kristo alikuja duniani? (ona, kwa mfano, Luka 4:16–21; Yohana 3:16–17; 3 Nefi 27:13–16; Mafundisho na Maagano 20:20–28). Ni kwa jinsi gani ufahamu huu huathiri jinsi unavyohisi kuhusu Mwokozi? Ni kwa jinsi gani hilo huathiri jinsi unavyoishi?

Ona pia 2 Wakorintho 8:9; Waebrania 2:7–18; 1 Nefi 11:13–33; Alma 7:10–13; “The Nativity” (video), ChurchofJesusChrist.org.

1 Wakorintho 15:21–26; Wakolosai 1:12–22; 1 Petro 2:21–25

Yesu Kristo alitimiza misheni Yake na kufanya iwezekane kwangu kuurithi uzima wa milele.

Japokuwa hadithi ya kuzaliwa kwa Kristo ilizungukwa na matukio ya kimiujiza, kuzaliwa Kwake kungekuwa tu kama kuzaliwa kwingine isingekuwa kwa kazi kuu ambayo aliikamilisha baadaye katika maisha Yake. Kama Rais Gordon B. Hinckley alivyoiweka, “Mtoto Yesu wa Bethlehemu angekuwa tu kama mtoto mwingine bila Kristo mkombozi wa Gethsemane na Kalvari, na ukweli wenye shangwe wa ushindi wa Ufufuko” (“Maajabu na Hadithi ya Kweli ya Krismasi,” Ensign, Desemba. 2000, 5).

Picha
Yesu akiwa amepiga magoti katika Bustani ya Gethsemane

Gethsemane, na J. Kirk Richards

Ushahidi wa misheni takatifu ya Mwokozi na upendo Wake wenye nguvu kwa wengine unapatikana kote kwenye Agano Jipya. Je, ni vifungu vipi au hadithi gani hukujia akilini? Unaweza kuangalia nyuma kupitia nyenzo hii au shajara yako ya kujifunza na kurejelea baadhi ya misukumo uliyoandika. Ungeweza pia kusoma 1 Wakorintho 15:21–26; Wakolosai 1:12–22; 1 Petro 2:21–25 na kutafakari ni jinsi gani Mwokozi na kazi Yake vimebariki maisha yako. Je, unahisi kushawishika kubadili nini katika maisha yako? Je, ni kwa jinsi gani utaivuta nguvu ya Mwokozi?

Picha
ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Mathayo 1:18–25; 2:1–12; Luka 1:26–38; 2:1–20Ni kwa jinsi gani wewe unaweza kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu Kristo pamoja na familia yako? Hapa kuna baadhi ya mawazo, au unaweza kuja na ya kwako:

  • Someni na igizeni pamoja vipengele vya hadithi ya Kuzaliwa kwa Yesu Kristo.

  • Tazama video “The Christ Child” (ChurchofJesusChrist.org).

  • Chunguza baadhi ya nyenzo katika “Yesu Kristo” mkusanyiko katika Maktaba ya Injili, hasa katika sehemu yenye kichwa cha habari “Kuzaliwa Kwake (Krismasi),”

  • Tazama ibada ndogo ya Krismasi ya Urais wa Kwanza (broadcasts.ChurchofJesusChrist.org).

  • Imbeni pamoja nyimbo za kanisa za Krismasi, au chagueni majirani au marafiki wa kuwatembelea na kuwaimbia (ona Nyimbo za kanisa, na. 201–14).

  • Fanya tendo la huduma.

  • Waambie wanafamilia kutafuta maelezo katika hadithi ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo ambayo yanawapa mawazo kwa ajili ya madoido au mapambo wanayoweza kutengeneza ili kuwakumbusha juu ya Yesu Kristo.

1 Wakorintho 15:21–26; Wakolosai 1:12–22; 1 Petro 2:21–25Kwa nini tunashukuru kwamba Yesu Kristo alizaliwa? Ni zawadi gani Yeye ametupatia sisi? Tunawezaje kumwonyesha Yeye shukrani zetu? Familia yako ingeweza kuimba wimbo unaofundisha kuhusu misheni Yake, kama vile “He Sent His Son” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 34–35).

Kristo Aliye Hai: Ushuhuda wa Mitume.”Kama ukitaka kuisaidia familia yako kufokasi kwa Mwokozi wakati wa Krismasi, pengine mnaweza kutumia muda kusoma na kujifunza pamoja “Kristo Aliye Hai: Ushuhuda wa Mitume” (ChurchofJesusChrist.org). Pengine mnaweza kukariri vifungu kutoka “Kristo Aliye Hai” au kutafuta maelezo ya maisha ya Mwokozi ndani ya Agano Jipya ambayo huunga mkono kauli zilizomo. Unaweza pia kumualika kila mwanafamilia kuandika ushuhuda wake juu ya Yesu Kristo na, kama ameshawishika hivyo, ausome kwa familia.

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “Once within a Lowly Stable,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 41.

Kuboresha Kujifunza Binafsi

Mtafute Yesu Kristo. Maandiko yanatufundisha kwamba vitu vyote vinashuhudia juu ya Yesu Kristo (ona Musa 6:62–63), kwa hivyo tunapaswa kumtafuta Yeye katika mambo yote. Unaposoma maandiko, fikiria kuandika au kuwekea alama mistari inayokufundisha kuhusu Yeye. Tumia muda katika siku zinazoelekea Krismasi kuangalia vitu vinavyokuzunguka ambavyo vinashuhudia juu ya Yesu Kristo.

Picha
Mariamu, Yusufu, na wachungaji wakiwa wamemzunguka mtoto Yesu.

Kuzaliwa kwa Yesu Kristo, na Brian Call

Chapisha