Agano Jipya 2023
Desemba 11–17. Ufunuo 6–14: “Walishinda … kwa Damu ya Mwanakondoo”


“Desemba 11–17. Ufunuo 6–14: “Walishinda … kwa Damu ya Mwanakondoo,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2021)

“Desemba 11–17. Ufunuo 6–14.“ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023

Yesu amesimama miongoni mwa nyota

Sanaa ya mchanganyiko na Eric Johnsen: Baraza Kuu, na Robert T. Barrett; kishada cha nyota kwa hisani ya European Space Agency

Desemba 11–17

Ufunuo 6– 14

“Walishinda … kwa damu ya Mwanakondoo”

Unaposoma Ufunuo 6–14, fikiria kuhusu watoto unaowafundisha. Roho Mtakatifu anaweza kukusaidia kuzitambua kweli ambazo zitaeleweka kwao.

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waonyeshe baadhi ya picha ambazo zitawasaidia watoto kukumbuka vitu walivyojifunza hivi karibuni nyumbani au katika Msingi. Waalike watoto kushiriki vitu wanavyojua kuhusu picha hizo.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Ufunuo 7:9,13–14

Yesu Kristo ananisaidia niwe safi.

Yohana aliwaona watu wengi waliovikwa mavazi “yaliyofanywa … meupe katika damu ya Mwanakondoo” (mstari wa 14). Fikiria jinsi ono hili linavyoweza kuwasaidia watoto kuelewa umuhimu wa kufanywa wasafi kutokana na dhambi zetu kwa njia ya Upatanisho wa Yesu Kristo.

Shughuli Yamkini

  • Waonyeshe watoto baadhi ya mavazi meupe (au picha ya baadhi ya nguo hizo) na picha ya Yesu. Wasomee watoto Ufunuo 7: 9, 13–14, na waombe kuonesha picha na nguo kila wakati wanaposikia neno nyeupe. Eleza kwamba nguo nyeupe inawakilisha usafi na kutukumbusha kwamba Yesu Kristo anaweza kutufanya kuwa wasafi kutoka kwa makosa yetu.

  • Waonyeshe watoto kipande cha nguo nyeupe, au kipande cha karatasi na waache waichafue kwa kuiweka alama na kalamu au kuweka uchafu juu yake. Eleza kwamba tunapoacha kutii amri, inaweza kuonekana kama kuwa na uchafu juu ya nguo zetu. Onyesha picha ya Yesu katika Gethsemane (kama vile Kitabu cha Sanaa za Injili, na. 56), ondoa nguo chafu, na waoneshe iliyo safi. Shuhudia kwamba Yesu Kristo anaweza kutusaidia kuwa safi.

  • Imbeni wimbo kuhusu ubatizo, kama vile “When I Am Baptized” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 103), na shuhudia kwamba Yesu anatusaidia kuwa wasafi wakati tunapobatizwa.

Ufunuo wa Yohana 12:7–11

Nilionyesha imani katika Yesu Kristo katika maisha kabla ya kuja duniani.

Katika Vita huko Mbinguni, watoto waaminifu wa Mungu walimshinda Shetani kwa “neno la ushuhuda wao” na kwa kuonyesha imani katika Yesu Kristo (Ufunuo 12:11). Wanaendelea kufanya hivyo leo.

Shughuli za Yakini

  • Ili kuwasaidia watoto kuelewa ina maana gani kufuata mfano wa mtu fulani, mchague mtoto mmoja kuwa “kiongozi” na waombe wengine kumfuata kwa kufanya cho chote kile anachokifanya yeye. Kisha acha mtoto mwingine awe kiongozi. Wasomee watoto Ufunuo 12:7–11 na uelezee kwamba kabla hatujazaliwa, sisi tulichagua kumfuata Yesu na sio Shetani.

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu maisha kabla ya kuja duniani, kama vile “I Lived in Heaven” au “I Will Follow God’s Plan” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 4, 164-65). Uliza maswali kama, “Ni nini kilitokea Mbinguni kabla hatujazaliwa?” na “Sisi tulichagua kufanya nini?” (Ona pia “Utangulizi: Mpango wa Baba Yetu wa Mbinguni” katika Hadithi za Agano Jipya, 1-5, au video inayofanana katika ChurchofJesusChrist.org.)

Ufunuo 14:6–7

Injili ilirejeshwa katika siku yetu.

Yohana aliandika kuhusu malaika ambaye angeleta “injili isiyo na mwisho” (Ufunuo 14:6). Kujadili Ufunuo 14:6–7 kunatoa fursa kwa ajili yako kushuhudia juu ya Urejesho wa injili ya Yesu Kristo katika siku yetu.

Shughuli Yamkini

  • Waonyeshe watoto picha ya Moroni akizungumza na Joseph Smith unaposoma Ufunuo 14:6 (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 91). Waalike watoto kuonyesha malaika kwa kidole katika picha. Wasimulie hadithi ya matembezi ya Moroni (ona “Sura ya 3: Malaika Moroni na Mabamba ya Dhahabu,” katika Hadithi za Mafundisho na Maagano, 13–17], au video inayohusiana kwenye ChurchofJesusChrist.org).

  • Waache watoto waigize hadithi ya Moroni akimtembelea Joseph Smith (ona Joseph Smith— Historia ya 1:29–35). Wasaidie kutaja baadhi ya baraka ambazo tunazifaidi kwa sababu ya injili ya Yesu Kristo kurejeshwa. Toa ushuhuda wako juu ya Urejesho.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Ufunuo 9:1–2

Injili inaweza kunisaidia kushinda majaribu.

Moshi ambao ulitia giza hewa katika Ufunuo 9:2 unaweza kufananishwa na majaribu (ona 1 Nefi 12:17).

Shughuli Yamkini

  • Chora picha za jua na wingu zito, na uzikate. Waalike watoto kusoma Ufunuo 9:2 na 1 Nefi 12:17 na andika juu ya hilo wingu zito kile ambacho moshi au ukungu katika mstari hii huwakilisha. Weka wingu zito juu ya ubao, na waombe watoto kutengeneza orodha ya majaribu ambayo watoto wa umri wao wanakabiliana nayo. Kisha weka jua juu ya ubao na waombe wao watengeneze orodha ya zana ambazo Baba wa Mbinguni ametupa ili kulishinda giza katika ulimwengu.

  • Ni kwa jinsi gani sisi tunaweza kuwasaidia wengine ambao wako gizani kiroho? Kuwasaidia kufikiria kuhusu swali hili, onyesha sehemu ya video “Choose the Light” (ChurchofJesusChrist.org), maalumu nusu ya mwisho ya video hiyo. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa kama yule mwendesha baiskeli ndani ya handaki?

Ufunuo wa Yohana 12:7–11

Nilionyesha imani katika Yesu Kristo katika maisha kabla ya kuja duniani.

Watoto unaowafundisha wapo duniani kwa sababu walikuwa na imani katika Yesu Kristo katika maisha kabla ya kuja duniani na walichagua kumfuata Yeye.

Shughuli za Yakini

  • Someni pamoja Ufunuo 12:7–11, na andika ubaoni maneno joka, Vita Mbinguni, tupwa nje, ushuhuda, na Mwanakondoo. Waalike watoto kufanya muhtasari wa mistari hii wakitumia maneno yaliyopo ubaoni. Je, tunajifunza nini kuhusu Yesu Kristo (mwana kondoo) kutoka mistari hii? Je, tunajifunza nini kuhusu chaguzi tulizofanya katika maisha kabla ya kuja duniani?

  • Kwenye ubao, tengeneza safu tatu na zitambulishe kama Kabla ya maisha haya, Wakati wa maisha haya, na Vyote. Tayarisha vipande vya karatasi ambavyo vinaeleza ukweli kuhusu maisha kabla ya kuja duniani na kuhusu maisha hapa duniani, kama vile Tunayo miili, Hatuna miili, tunaishi katika uwepo wa Mungu, Tupo vitani dhidi ya Shetani, Tunaonyesha imani katika Yesu Kristo, na Tunafuata mpango wa Mungu. Waache watoto wachukue zamu kuchagua kipande cha karatasi na kuamua ni safu gani kinastahili kuwemo. Shiriki kujiamimi kwako kwamba watoto wanaweza kuendelea kuonyesha imani katika Kristo.

Ufunuo 14:6–7

Kama sehemu ya Urejesho, injili hii itafundishwa ulimwenguni kote.

Watoto unaowafundisha wanaweza kusaidia kuhubiri injili “kwa kila taifa, na kabila, na lugha, na jamaa” (Ufunuo 14:6).

Shughuli Yamkini

  • Waombe watoto wasome Ufunuo 14:6–7 na kuandika ubaoni maneno au virai kutoka mistari hii ambavyo ni vyenye maana kwao. Waulize kwa nini walichagua maneno au virai hivyo. Eleza kwamba mistari hii inaelezea Urejesho wa injili katika siku yetu. Waulize ni kwa jinsi gani wao watashiriki katika kazi ya kuhubiri injili ulimwenguni.

  • Waalike watoto wasome Ufunuo 14:7 na kusema kwa maneno yao wenyewe ujumbe ule malaika aliokuwa nao kwa ajili ya ulimwengu. Au waalike kuchora picha ikiwakilisha ujumbe wa malaika. Tunaweza kushiriki nini na wengine kuhusu injili ya Yesu Kristo?

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Wasaidie watoto kuandika neno au kirai ambacho kitawasaidia kukumbuka kitu walichojifunza katika darasa leo. Waalike kuonyesha kile walichoandika kwa mtu nyumbani na wamsimulie kile walichojifunza.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Fundisha mafundisho kupitia muziki. Kuimba nyimbo na watoto kunaweza kuimarisha mafundisho unayoyafundisha kutoka katika maandiko. Kwa ajili ya mawazo, ona “Kutumia Muziki ili Kufundisha Mafundisho” katika sehemu yenye jina “Maelekezo kwa Ajili ya Muda wa Kuimba na Mawasilisho ya Watoto katika Mkutano wa Sakramenti” mwishoni mwa kitabu hiki cha kiada.