Agano Jipya 2023
Novembe 27– Desemba 3. 1–3 Yohana; Yuda: “Mungu ni Upendo”


“Novemba 27–Desemba 3, 1–3, Yohana; Yuda: ‘Mungu ni Upendo’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2021)

“Novemba 27–Desemba 3. 1–3, Yohana; Yuda.” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023

Picha
Yesu Kristo akitabasamu akiwa amekaa na watoto wenye kutabasamu

Upendo Mkamilifu, na Del Parson

Novemba 27–Desemba 3

1–3 Yohana; Yuda

“Mungu ni Upendo”

Nyaraka za Yohana na Yuda zinafundisha kuhusu upendo na nuru ya Baba wa Mbinguni. Unapojifunza wiki hii, tafakari kwa nini watoto unaowafundisha wanahitaji nuru Yake na upendo Wake katika maisha yao. Kumbuka kuzingatia shughuli zote katika muhtasari huu, sio tu hizo zilizoorodheshwa chini ya rika unalofundisha.

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waalike watoto kuelezea jinsi walivyouhisi upendo wa Baba wa Mbinguni na Yesu au kwa nini wanafikiri Baba wa Mbinguni na Yesu ni kama nuru kwetu sisi.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

1 Yohana 1:5–7; 2:8–11

Kumfuata Yesu kunaleta nuru kwenye maisha yangu.

Yohana aliandika kuhusu nuru ili kufundisha kuhusu nguvu ya Baba wa Mbinguni na Yesu katika maisha yetu. Fikiria jinsi unavyoweza kuwasaidia watoto kujifunza kuhusu nuru ambayo Wao wanatupatia.

Shughuli Yamkini

  • Waombe watoto wataje vitu vinavyotoa nuru. Zungumza nao kuhusu faida za nuru, kama kusaidia mimea kukua, kutuwezesha kuona, na kutoa joto. Ili kuelewa jinsi Yesu anavyotupatia nuru, wangeweza kupeana zamu wamulike tochi kwenye picha ya Yesu Kristo wanapokuwa wakisema, “Mungu ni nuru” (1 Yohana 1:5). Shuhudia kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanaweza kuleta nuru katika maisha yetu tunapojaribu kufuata kile Wao wanasema.

  • Waalike watoto kuchukua zamu ya kushikilia picha ya balbu ya umeme au mshumaa. Kila mtoto anaposhikilia picha, msaidie kufikiria njia tunayoweza kuleta nuru ya Yesu Kristo ndani ya maisha yetu.

1 Yohana 4:10–11, 20–21

Ninaonyesha upendo wangu kwa Mungu ninapoonyesha upendo kwa wengine.

Wasaidie watoto kuona uhusiano kati ya upendo wanaouhisi kwa Baba wa Mbinguni na upendo wanaoonyesha kwa watoto Wake.

Shughuli Yamkini

  • Wasomee watoto 1 Yohana 4:11 na uimbe wimbo kuhusu upendo wa Mungu, kama vile “My Heavenly Father Loves Me” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 228). Waombe watoto wachache kuelezea jinsi wanavyojua kwamba Baba wa Mbinguni anawapenda. Baada ya kila jibu, waalike watoto kukumbatiana na kusema, “Mungu ni upendo, na Mungu ananipenda.”

  • Wasomee watoto 1 Yohana 4:21. Waalike kuelezea kuhusu au kuigiza njia mbalimbali wanazoweza kuonyesha upendo kwa rafiki, kama vile kumkumbatia au kumtengenezea kadi. Je, vitu hivi vinamfanya rafiki yetu ajisikieje? Baba wa Mbinguni anajisikiaje tunapofanya mambo ya ukarimu kwa wengine?

1 Yohana 2:3–5; 5:3

Ninaonyesha upendo wangu kwa Mungu ninaposhika amri Zake.

Yohana alifundisha kwamba “amri za Mungu siyo nzito” (1 Yohana 5:3). Bali, kufuata amri ni njia ya kuonyesha upendo wetu Kwake.

Shughuli Yamkini

  • Soma 1 Yohana 5:3, na waombe watoto wasikilize ni nini mstari huu unasema kuhusu jinsi tunavyoweza kuonyesha kwamba tunampenda Mungu. Waalike watoto kutaja amri nyingi kadiri wanavyoweza. Tunajisikiaje tunapotii amri za Baba wa Mbinguni?

  • Waalike watoto kuchora picha inayoonesha mojawapo ya njia wanayoweza kumwonyesha Baba wa Mbinguni kwamba wanampenda. Kwa mfano, wanaweza kuchora picha yao wenyewe wakishika moja ya amri hizo.

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu utii, kama vile “Choose the Right Way” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 160). Tunajisikiaje tunapotii?

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

1 Yohana 2:8–11; 4:7–8, 20–21

Ninaonyesha upendo wangu kwa Mungu ninapoonyesha upendo kwa wengine.

Unawezaje kuwasaidia watoto kujua kwamba kumpenda Mungu kunahusisha kuwapenda wale wanaotuzunguka—hata watu wanaoweza kuwa tofauti nasi au vigumu kuwapenda?

Shughuli Yamkini

  • Waombe watoto wawaze kwamba mtu mpya ameanza kuhudhuria shule yao au kata na hamjui mtu yo yote pale. Mtu huyu anaweza kuwa anajisikiaje? Mwalike mtoto asome 1 Yohana 4:7–8. Mstari huu unapendekeza nini kuhusu jinsi tunavyotakiwa kumtendea mtu huyu? Elezea matukio yanayofanana, au waombe watoto kufikiria hali ambazo wao wanaweza kuwa na nafasi za kuonyesha upendo.

  • Waombe watoto wasome 1 Yohana 4:7–8, 20–21, na waalike kila mmoja kuandika sentensi moja ili kufanya muhtasari wa kile wanachofikiri ni somo muhimu sana katika mistari hii. Baada ya kushiriki sentensi zao, shiriki hadithi kutoka katika maisha yako au kutoka gazeti la Rafiki au Liahona ambayo unahisi huonyesha kile mistari hii inafundisha (ona, kwa mfano, “Say Hello to Halim,” Rafiki, Juni 2019, 8–9; au Liahona, Juni 2019, F18–F19). Waalike watoto kushiriki mifano yao wenyewe. Tunawezaje kuonyesha upendo kwa wale wanaotuzunguka?

1 Yohana 2:3–6; 4:17–18; 5:2–5

Ninaonyesha upendo wangu kwa Mungu ninaposhika amri Zake.

Kushika amri kunaweza kuwa rahisi mno wakati tunapoelewa kweli zinazofundishwa ndani yake 1 Yohana 5:3. Je, unawezaje kuwasaidia watoto kuziona amri sio kama mizigo bali kama fursa za kuonyesha upendo wao kwa Mungu?

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto kuorodhesha ubaoni njia wanazoweza kumwonesha Mungu kwamba wanampenda. Kisha someni pamoja 1 Yohana 2:5–6; 5:2–5 kwa mawazo ya ziada. Je, ni kwa jinsi gani kushika amri kunaonyesha kwamba tunampenda Baba wa Mbinguni?

Picha
familia imepiga magoti pamoja katika sala

Kutii amri za Mungu hutusaidia kuushinda ulimwengu.

  • Soma 1 Yohana 4:17, na uwaelezee watoto kwamba “kuwa na ujasiri katika siku ya hukumu” maana yake ni kuwa na kujiamini na amani wakati watakaposimama mbele ya Mungu kuhukumiwa. Je, mstari huu unafundisha nini ambacho tunahitaji kufanya ili kuwa na kujiamini huko? Je, ni vitu gani vingine tunavyoweza kufanya sasa ili tuwe na kujiamini mbele ya Mungu?

Yuda 1:18–22

Naweza kuwa mwaminifu hata wakati wengine wanaponifanyia mzaha.

Kwa sababu sisi ni wafuasi wa Yesu Kristo, wengine wakati mwingine hutukejeli kwa ajili ya imani yetu au njia tunazoishi. Mistari hii ina ushauri wa Yuda juu ya jinsi ya kubaki waaminifu katika hali kama hizo.

Shughuli Yamkini

  • Waombe watoto kusimulia nyakati walipofanyiwa mzaha au mtu wanayemjua kwa sababu wao walifanya kitu kilicho sahihi. Waalike watoto wasome Yuda 1:18–22 na kutafuta jinsi tunavyoweza kubaki waaminifu tunapokejeliwa au kufanyiwa mzaha. Andika ubaoni kile wanachokipata, na jadili njia wanazoweza kufuata ushauri huu.

  • Fanya muhtasari wa ndoto ya Lehi (ona 1 Nefi 8:1–35), waombe watoto wachache wasome mistari kutoka 1 Nefi 8:26–28, 33. Jadili jinsi watu katika jumba kubwa na pana walivyokuwa kama wafanya mzaha ambao Yuda alizungumzia. Je, tufanye nini ili tusishawishiwe na hao wanaotufanyia mzaha au wasiokubaliani na kile tunachoamini? (ona 1 Nefi 8:30, 33).

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Wahimize watoto kutengeneza mpango wa kufanya kitu fulani ili kushiriki nuru yao pamoja na familia zao.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Watoto ni wachangamfu. Wakati mwingine unaweza kuhisi kwamba uchangamfu wa watoto ni vurugu kwenye kujifunza. Lakini unaweza kujenga katika asili ya uchangamfu wao kwa kuwaalika kuigiza, kuchora, au kuimba kuhusu kanuni ya injili. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi25–26.)

Chapisha