Agano Jipya 2023
Disemba 4–10. Ufunuo wa Yohana 1–5: “Utukufu, na Ukuu, Kuwa kwa … Mwana Kondoo Milele’”


“Disemba 4–10. Ufunuo 1–5: ‘Utukufu, na Ukuu Kuwa kwa … Mwana kondoo Milele’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2021)

“Disemba 4–10. Ufunuo 1–5.“ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023

Picha
Mwanakondoo amekaa kwenye nyasi

Disemba 4–10

Ufunuo 1– 5

“Utukufu, na Ukuu, Kuwa kwa … Mwana Kondoo Milele”

Kitabu cha Ufunuo kinaweza kuwa kigumu kueleweka kwa watoto, lakini pia kina mafundisho muhimu ambayo ni mazuri na rahisi.

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waalike watoto kushiriki jinsi wanavyoweza kuhisi kama wangemwona Yesu Kristo katika ono. Waombe watoto washiriki cho chote wanachokijua kuhusu ono la Yohana katika kitabu cha Ufunuo.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Ufunuo 1:20

Ninaweza kuangaza nuru ya Mwokozi.

Katika Ufunuo 1:20, Mwokozi analinganisha Kanisa Lake na minara ya mshumaa. Wasaidie watoto kuelewa kwamba wanaweza kuangaza nuru ya Mwokozi kwa kuishi mafundisho Yake.

Shughuli Yamkini

  • Waonyeshe watoto picha za vyanzo mbali mbali vya nuru, kama balbu ya umeme, mshumaa, na jua. Unaposoma “Vinara saba vya mishumaa ulivyoviona ni makanisa saba” (Ufunuo 1:20), waalike watoto kuonyesha kwa kidole kwenye picha ya nuru inayotajwa katika mstari huu. Wasaidie watoto kujadili jinsi sisi, kama waumini wa Kanisa la Yesu, tunavyoweza kuwa kama nuru ya mshumaa—kwa mfano, tunapofanya vitu vizuri kwa wengine.

  • Imbeni wimbo kuhusu kuwa nuru kwa wengine, kama vile “Jesus Wants Me for a Sunbeam” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 60–61). Shiriki njia ulizoona watoto wakiishi injili ya Yesu Kristo na kuwa nuru kwa watu wanaowazunguka. Shiriki jinsi kuwa nuru kwa wengine kulivyokusaidia wewe kujiona uko karibu zaidi na Baba Mbinguni na Yesu Kristo.

Ufunuo 3:20

Ninaweza kumwalika Yesu Kristo katika maisha yangu.

Sitiari ya Yesu akisimama mlangoni na akigonga inaweza kuwasaidia watoto kuelewa kwamba anataka kuwa karibu nao.

Shughuli Yamkini

  • Unaposoma Ufunuo 3:20, onyesha picha ya Mwokozi akiwa mlangoni kutoka muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia. Waalike watoto wawaze kwamba Yesu alikuwa anagonga mlangoni kwenye nyumba zao. Acha wazungumze kuhusu kile ambacho wangeweza kufanya.

  • Waalike watoto wakuelezee kuhusu nyakati walipomsubiri mtu fulani kutembelea nyumbani kwao mtu ambaye walikuwa na shauku ya kumwona. Je, ilikuwaje kumsubiri mtu yule agonge mlango? Je, ingekuwaje kama tusingemruhusu aingie ndani? Soma Ufunuo 3:20, na waache watoto wachukue zamu kushika picha ya Yesu na kujifanya kuwa anagonga mlango. Washiriki wengine wa darasa wajifanye wanamfungulia mlango. Je, tunaweza kufanya nini ili kumwacha Yesu awe karibu nasi, hata kama hatuwezi kumwona?

Ufunuo 5:1–10

Yesu Kristo ni mtu pekee anayestahili kuwa Mwokozi wangu.

Yohana alijifunza kutoka katika ono lake kwamba Yesu Kristo ni mtu pekee (aliyewakilishwa na mwana kondoo) ambaye angeweza kuwa Mwokozi wetu na kutimiza mpango wa Baba (uliowakilishwa na kitabu kilichotiwa muhuri).

Shughuli Yamkini

  • Kabla ya darasa, fungasha nakala ya Kitabu cha Sanaa ya Injili ukitumia karatasi au kamba. Ukitumia virai vichache muhimu kutoka Ufunuo 5:1–10, elezea ono Yohana aliloona. Waoneshe watoto kitabu hicho, na waambie kwamba njia pekee ya kufungua kitabu ni kutafuta picha ya Yesu ambayo umeificha ndani ya chumba. Watakapoipata picha, fungua kitabu na shiriki pamoja na watoto baadhi ya picha zilizoko ndani ya kitabu ambazo zinawakilisha baraka zillizoko kwa sababu ya Upatanisho wa Yesu Kristo (kama vile hekalu, ubatizo, na familia). Shuhudia kwamba Mwokozi ndiye mtu pekee ambaye angeweza kufanya vitu hivyo viwezekane.

  • Fanya muhtasari wa ono lililoelezwa katika Ufunuo 5:1–10, na waalike watoto waigize jinsi Yohana na wengine walivyojisikia wakati wa sehemu tofauti za ono. Kwa mfano, wanaweza kujifanya wanalia wakati hakuna yoyote anayeweza kufungua kitabu, au wanaweza kushangilia wakati Mwokozi alipokifungua.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Ufunuo 3:5,12–21

Kama nikijizaatiti kwenye injili ya Mwokozi, nitapokea baraka kubwa mbinguni.

Inamaanisha nini kwako kuwa “vuguvugu na siyobaridi wala moto”? Zingatia njia za kuwasaidia watoto kuwa kinyume cha uvuguvugu—kuwa wenye shauku katika kujitolea kwa Mwokozi na injili Yake.

Shughuli Yamkini

  • Someni pamoja Ufunuo 3:5, 12, 21, na ufafanue neno lo lote ambalo yawezekana watoto hawalijui. Je, ni nini maana ya “kushinda”? Waalike watoto kuchora picha ya moja ya baraka zilizoahidiwa katika mistari hii na kushiriki na darasa.

  • Someni pamoja Ufunuo 3:15–16. Waombe watoto kuzungumzia kuhusu vitu ambavyo vinatumika zaidi au vyenye kufurahisha vinapokuwa bado moto (kama vile supu) au baridi (kama vile aisi krimu). Je, ni kwa jinsi gani kuwa uvuguvugu kuhusu Mwokozi kunatuzuia sisi kupokea baraka zilizoahidiwa katika mstari wa 5, 12, na 21?

  • Ubaoni, andika uvuguvugu, sambamba na baadhi ya visawe, kama vile shingo upande, siyojali, au kawaida. Tumia maneno haya ili kuwasaidia watoto kuelewa kwa nini Bwana hataki sisi tuwe wa uvuguvugu. Ni maneno gani tunaweza kuyafikiria ili kuelezea njia ambazo Yeye anatutaka sisi tuwe? Shiriki ni kwa nini wewe unataka kuwa mtu aliyejitolea kwa dhati kwa Mwokozi, na waalike watoto nao washiriki mawazo yao.

Ufunuo 3:20

Ninaweza kuchagua kumruhusu Yesu Kristo kuwa sehemu ya maisha yangu.

Je, unawezaje kuwasaidia watoto unaowafundisha kufungua mioyo yao na maisha kwa uwezo na ushawishi wa Yesu Kristo?

Shughuli Yamkini

  • Unaposoma Ufunuo 3:20, onyesha picha ya Mwokozi akiwa mlangoni kutoka muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia. Ili kuwasaidia watoto kupata maana kutoka kwenye picha, waalike kufanya kazi katika majozi ili kujibu maswali kama haya: Je, kwa nini unafikiri Yesu anagonga mlangoni? Je, kwa nini hakuna kitasa chenye mkono nje ya mlango? Je, inamaanisha nini kumruhusu Yesu ndani ya maisha yetu?

  • Waombe watoto kuandika ubaoni njia tofauti za “kufungua mlango” kwa ajili ya Yesu. Baadhi ya mifano inaweza kujumuisha kuwahudumia wengine, kusoma maandiko, kushika maagano tunayofanya kwenye ubatizo, na kupokea sakramenti.

Ufunuo 5:1–10

Yesu Kristo ni mtu pekee anayestahili kuwa Mwokozi wangu.

Ono lililoelezwa katika Ufunuo 5 lilifundisha kwamba Yesu Kristo pekee ndiye alistahili na kuweza kutekeleza Upatanisho na kutuokoa kutokana na dhambi.

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto kueleza juu ya wakati ambapo walimhitaji mtu fulani kufanya kitu wasichoweza kujifanyia wao wenyewe. Waombe kusoma Ufunuo 5:1–10 na kutafuta kile kilichotakiwa kufanywa ambacho mtu mmoja pekee ndiye angeweza kufanya (eleza kwamba mwana kondoo ni Yesu Kristo na kitabu kinawakilisha mpango wa Mungu). Je, Yesu alifanya nini kwa ajili yetu ambacho hakuna mtu mwingine ye yote angeweza kufanya?

  • Waombe watoto kutafuta wimbo au wimbo wa watoto ambao unamshuhudia Yesu Kristo (kama vile “Beautiful SaviorKitabu cha Nyimbo za Watoto, 62–63). Maneno ya wimbo yanafundisha nini kuhusu Yesu Kristo? Je, ni kwa jinsi gani wimbo huu ungeweza kuwa kama wimbo wa sifa ulioimbwa kuhusu Yesu Kristo katika Ufunuo 5:9–10?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kushiriki na familia zao njia wanazoweza kukaribisha ushawishi wa Mwokozi ndani ya nyumba zao.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Himiza staha. Kipengele muhimu cha staha ni kufikiria juu ya Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Unaweza kuwakumbusha watoto kuwa wenye staha kwa kuimba kimya kimya au kwa mvumo au kuonyesha picha ya Yesu.

Chapisha