“Disemba 25–31. Ufunuo 15–22: ‘Yeye Ashindaye Atayarithi Vitu Vyote’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023 (2021)
“Disemba 25–31. Ufunuo 15–22,“ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2023
Disemba 25–31
Ufunuo 15–22
“Yeye Ashindaye Atarithi Vitu Vyote”
Unapojiandaa kufundisha, fikiria juu ya uzoefu wako mwenyewe wa kujifunza Ufunuo 15–22 wewe binafsi au pamoja na familia yako. Je, ni kitu gani kilichokuwa cha kipekee kwako? Je, ni misukumo gani ulipokea? Kumbuka kwamba shughuli zilizopendekezwa katika muhtasari huu zinaweza kutoholewa kwa ajili ya watoto wa umri wo wote.
Alika Kushiriki
Waombe watoto kushiriki kwa nini wanataka kuishi na Baba wa Mbinguni tena. Katika somo hili, wasaidie kutafuta vitu wanavyoweza kufanya ili kujiandaa kurudi Kwake.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo
Ninaweza kumsifu Mungu kwa kuimba.
Watakatifu wanaoelezwa na Yohana katika Ufunuo 15:2–4 waliimba sifa kwa Mungu kwa ajili ya wema Wake. Nyimbo gani za sifa zinazoweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kuonyesha upendo wao kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo?
Shughuli Yamkini
-
Unaposoma kwa sauti sehemu za Ufunuo 15;2–4, waombe watoto wafanye vitendo kama vile kujifanya kupiga kinubi au kuongoza kwaya Je, tunahisi vipi wakati tunapoimba kuhusu Yesu?
-
Waombe watoto kushiriki baadhi ya nyimbo wazipendazo kuhusu Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Imbeni nyimbo chache kati ya hizo kwa pamoja, na wasaidie watoto kuelewa kile ambacho nyimbo hizi hutufundisha kuhusu Baba wa Mbinguni na Mwokozi.
Ninaweza kujiandaa kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Yesu Kristo kwa kuchagua yaliyo mema.
Je, unawezaje kuwasaidia watoto kuelewa kwamba Ujio wa Pili utakuwa wa matukio ya furaha kwetu sisi kama tutafuata amri za Yesu?
Shughuli za Yakini
-
Waulize watoto kama wamewahi kuhudhuria sherehe za harusi. Je, ilikuwaje? Kwa nini watu wanafurahi katika harusi? Onyesha picha ya Ujio wa Pili wa Mwokozi katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia, na usome Ufunuo 19:7. Eleza kwamba “ndoa ya mwana kondoo” inawakilisha Ujio wa Pili wa Yesu Kristo. Kwa nini tushangilie wakati Mwokozi atakapokuja? Wasaidie watoto kulinganisha shangwe ya harusi na shangwe ya kurudi kwa Mwokozi.
-
Shiriki pamoja na watoto kwa nini wewe unatazamia Ujio wa Pili wa Yesu. Mngeweza pia kuimba pamoja wimbo kuhusu Ujio wa Pili, kama vile “When He Comes Again” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 82–83).
-
Waalike watoto kuelezea kile wanachokifanya ili kuwa tayari kwa ajili ya kanisani siku ya Jumapili. Je, ni kwa nini tunafanya vitu hivi kabla hatujaja kanisani? Je, ni kwa nini tujiandae kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Kristo? Kwenye ukurasa wa shughuli ya wiki hii, waache watoto wachore kile wanachoweza kufanya ili kujiandaa kwa ajili ya Ujio wa Pili.
Ufunuo 21:1, 3–4, 22–27; 22:1–2
Baba wa Mbinguni ananitaka mimi kuishi pamoja Naye katika ufalme wa selestia.
Katika sura mbili za mwisho za Ufunuo, Yohana alitumia lugha nzuri kuelezea utukufu wa selestia ambao waaminifu watafurahia.
Shughuli Yamkini
-
Wasaidie watoto wachore mti uliosimuliwa katika Ufunuo 22:2 ubaoni. Eleza kwamba mti huu ni mti wa uzima, na matunda yake yanawakilisha upendo wa Mungu (ona 1 Nefi 11:21–22). Wape watoto vipande vya karatasi vyenye umbo kama tunda, na waalike wachore kwenye karatasi hizo kitu fulani ambacho kinawasaidia kuhisi upendo wa Baba wa Mbinguni. Eleza kwamba wale wanaompenda na kumtii Baba wa Mbinguni wataishi pamoja na Yeye katika ufalme wa selestia.
-
Shiriki na watoto baadhi ya picha au maelezo ambayo Yohana anaelezea utukufu wa selestia (ona Ufunuo 21:1, 3–4, 22–27; 22:1–2), na waombe watoto wachore picha za vitu hivi.
-
Imbeni pamoja wimbo ambao unafundisha jinsi tunavyoweza kujiandaa kurudi katika uwepo wa Mungu, kama vile “I Will Follow God’s Plan” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 164–65). Waalike watoto kutambua kile wanachoweza kufanya ili kuishi na Baba wa Mbinguni tena.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa
Ninaweza kujiandaa kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Yesu Kristo kwa kuchagua yaliyo mema.
Je, ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kuelewa kwamba Ujio wa Pili wa Yesu Kristo utakuwa tukio la furaha kwa wenye haki?
Shughuli za Yakini
-
Someni pamoja Ufunuo 19:7–8, na wasaidie watoto kuelewa uashiriaji uliotumika katika mistari hii—harusi ni Ujio wa Pili wa Mwokozi, Mwana Kondoo ni Mwokozi, na mke Wake ni Kanisa (au sisi wote). Je, ni mambo gani tunatakiwa kufanya ili kujiandaa kwa ajili ya Mwokozi kuja tena?
-
Rejelea na ukariri Makala ya Imani 1:10 pamoja na watoto. Eleza kwamba makala hii ya imani inaelezea matukio ya kusisimua, na kufurahisha sana ambayo yatatokea wakati Yesu anapokuja tena. Onyesha picha ya Ujio wa Pili wa Yesu katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia, na waalike watoto kuchora kile wanachofikiri Ujio wa Pili wa Yesu utakukuwa kama nini.
Mimi nitahukumiwa na Mungu.
Sisi sote siku moja tutasimama mbele ya Mungu ili kuhukumiwa. Unaweza kuwasaidia watoto kuelewa kwamba hukumu Yake itakuwa ya haki na yenye huruma.
Shughuli Yamkini
-
Andika ubaoni Siku ya Hukumu itafananaje? Waalike watoto kutafuta majibu ya swali katika Ufunuo 20: 12–13 na katika “Hukumu, ya Mwisho” katika Mwongozo wa Maandiko (scriptures.ChurchofJesusChrist.org). Mwokozi amefanya nini hata kwamba Siku ya Hukumu iweze kuwa siku ya shangwe? (ona Makala ya Imani 1:3–4). Tunaweza kufanya nini ili kwamba iwe siku ya shangwe kwetu sisi?
-
Leta daftari darasani ikiwakilisha “kitabu cha uzima” (Ufunuo 20:12), ambamo ndani yake imeandika baadhi ya tabia za kama Kristo na matendo mema ya watoto katika darasa lako. Wasomee watoto mambo uliyoandika, na waalike kuzungumzia kuhusu tabia kama ya Kristo ambazo wao wameziona ndani ya kila mmoja. Toa ushuhuda wako kwamba Yesu Kristo anatusaidia sisi kuwa zaidi kama Yeye na anatoa njia kwa ajili yetu kutubu na kuishinda dhambi.
Ufunuo 21:1, 3–4,22–27; 22:1–2,17
Baba wa Mbinguni ananitaka mimi kuishi pamoja Naye katika ufalme wa selestia.
Unaposoma maelezo ya Yohana juu ya utukufu wa selestia katika Ufunuo 21–22, nini cha kipekee kwako wewe? Ni nini unashawishika kushiriki na watoto unaowafundisha?
Shughuli Yamkini
-
Waalike watoto kutafuta mistari ifuatayo kwa ajili ya maneno au virai ambavyo Yohana alitumia kuelezea utukufu wa selestia: Ufunuo 21:1, 3–4, 22–27; 22:1–2. Waache wachague kitu katika mistari hii ambacho wangependa kuchora. Kisha wanaweza kuzungumza kuhusu michoro yao na darasa. Watie moyo kuonyesha michoro yao kwa familia zao nyumbani.
-
Someni pamoja Ufunuo 22:17, na uelezee kwamba bibi harusi anayesema “Njoo” ni Kanisa. Ni nani, kama waumini wa Kanisa, anataka kuwaalika wengine “kuja” kwa? (ona Moroni 10:30–33). Wale wanaotuzunguka wangekuwa na “kiu” cha nini? Je, baadhi ya njia nzuri za kuwaalika watu “kuja” ni zipi?
Himiza Kujifunza Nyumbani
Wasaidie watoto kujiandaa kusoma Kitabu cha Mormoni mwaka ujao kwa kuwataka wamuulize mwanafamilia au rafiki kushiriki mstari au hadithi aipendayo kutoka katika Kitabu cha Mormoni.