Agano la Kale 2022
Mawazo ya Kuweka Akilini: “Yesu Atasema kwa Israeli Yote, ‘Njooni Nyumbani’”


“Mawazo ya Kuweka Akilini: ‘Yesu Atasema kwa Israeli Yote, “Njooni Nyumbani”’” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano la Kale 2022 (2021)

“Mawazo ya kuweka akilini: ‘Yesu Atasema kwa Israeli Yote, “Njooni Nyumbani,”’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafisi na Familia: 2022

Picha
ikoni ya mawazo

Mawazo ya Kuweka Akilini

“Yesu Atasema kwa Israeli Yote, ‘Njooni Nyumbani’”

Katika jangwa la Sinai, Musa aliwakusanya wana wa Israeli chini ya mlima. Pale Bwana alitangaza kwamba Yeye alitaka kuwageuza kundi la watumwa waliokombolewa karibuni kuwa watu imara. “Mtakuwa kwangu,” Alisema, “ufalme wa makuhani, na taifa takatifu” (Kutoka 19:6). Aliahidi kwamba watastawi na kufanikiwa, hata kama watakuwa wamezungukwa na kundi kubwa na lenye nguvu la maadui (ona Kumbukumbu la Torati 28:1–14).

Haya yote yangetokea sio kwa sababu Waisraeli walikuwa wengi au wenye nguvu au wajuzi. Yangetokea, Bwana alielezea, “ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu” (Kutoka 19:5). Ilikuwa ni nguvu za Mungu, na sio zao wenyewe, ambazo zingewafanya wao kuwa imara.

Na bado Waisraeli daima hawakutii sauti Yake, na kwa muda waliacha kushika maagano Yake. Wengi walianza kuabudu miungu mingine na kurithi mapokeo ya tamaduni zilizowazunguka. Walikataa kitu kile hasa kilichowafanya wao kuwa taifa, tofauti na wengine wote—uhusiano wao wa maagano na Bwana. Bila nguvu za Mungu kuwalinda (ona 2 Wafalme 17:6–7), hapakuwepo na kitu chochote kuwazuia maadui zao (ona 2 Mambo ya Nyakati 36:12–20).

Kutawanyika

Mara nyingi kati ya 735 na 720 KK, Waashuri walivamia Ufalme wa Kaskazini wa Israeli, nyumbani kwa makabila kumi kati ya kumi na mawili, na kuwachukua mateka maelfu ya Waisraeli na kuwapeleka sehemu mbalimbali za Himaya ya Ashuru (ona 2 Wafalme 17:1–7).1 Hawa Waisraeli walikuja kujulikana kama “makabila yaliyopotea,” kwa sehemu kwa sababu walikuwa wametolewa kutoka katika nchi yao na kutawanywa kati ya mataifa mengine. Lakini walikuwa pia wamepotea katika ufahamu mpana: kwa muda walipoteza ufahamu wao wa utambulisho kama watu wa agano wa Mungu.

Kwa sababu Ufalme wa Kusini wa Yuda ulikuwa, kwa wakati fulani wenye haki zaidi kuliko Ufalme wa Kaskazini, ulidumu sana.2 Lakini hatimaye watu huko pia walianza kugeukia mbali na Bwana. Waashuri walivamia na kushinda Falme nyingi za Kusini; isipokuwa tu Yerusalemu iliyookolewa kimiujiza (ona 2 Wafalme 19; Isaya 10:12–13). Baadaye, kati ya 597 na 580 KK, Wababeli waliiangamiza Yerusalemu, pamoja na hekalu, na kuchukua wengi wa wakazi wa mji mateka (ona 2 Wafalme 24–25; 2 Mambo ya Nyakati 36; Yeremia 3952). Karibia miaka 70 baadaye, masazo ya Yuda yaliruhusiwa kurudi Yerusalemu na kujenga upya hekalu. Wengi, hata hivyo, walibaki Babeli.3

Kadiri vizazi vilipopita, Waisraeli kutoka makabila yote “walitawanywa … kwa upepo wa kisulisuli, katikati ya mataifa yote wasiowajua.” (Zakaria 7:14; ona pia Amosi 9:8–9). Baadhi waliongozwa na Bwana katika nchi zingine (ona 2 Nefi 1:1–5; Omni 1:15–16). Wengine waliondoka Israeli kukwepa kukamatwa (ona 2 Wafalme 25:22–26; Yeremia 42:13–19; 43:1–7) au kwa sababu za kisiasa au za kiuchumi.4

Tunaita matukio yote haya kutawanywa kwa Israeli. Na ni muhimu kujua kuhusu kutawanywa kwa sababu kadhaa. Kwa sababu moja, ni mada kuu ya Agano la Kale: Manabii wengi wa Agano la Kale walikuwa ni mashahidi wa kudorora kiroho ambako kulisababisha kutawanywa kwa Israeli. Waliona kabla kutawanywa huko na kuonya kuhusu hilo, na baadhi yao waliishi kupitia hilo.5 Hiyo inasaidia kukumbuka wakati unaposoma kitabu cha Isaya, Yeremia, Amosi, na vingi kati ya vitabu vingine katika sehemu ya mwisho ya Agano la Kale. Pamoja na muktadha huu akilini, unaposoma unabii wao kuhusu Ashuru na Babeli, kuabudu sanamu na utumwa, ukiwa na hatimaye urejesho, utajua nini wanachokiongelea.

Kuelewa kutawanywa kwa Israeli kutakusaidia pia kuelewa kitabu cha Mormoni vizuri, kwa sababu kitabu cha Mormoni ni kumbukumbu ya tawi la Israeli iliotawanywa (ona 1 Nefi 15:12). Kumbukumbu hii inaanza na familia ya Lehi wakitoroka Yerusalemu mnamo 600 KK, kabla ya uvamizi wa Wababeli. Lehi alikuwa mmojawapo wa manabii hao waliotoa unabii wa kutawanywa kwa Israeli.6 Na familia yake ilisaidia kutimiza unabii huo, wakichukua tawi lao la nyumba ya Israeli na kulipanda katika upande mwingine wa dunia, katika Amerika.

Picha
watu wakiondoka katika mji unaoteketea

Kuangamizwa kwa Yerusalemu na Nebuzari-adani, na William Brassey Hole, © Providence Collection/licensed from goodsalt.com

Kusanyiko

Kutawanywa kwa Israeli, hata hivyo, ni nusu tu ya hadithi. Bwana hasahau watu Wake, wala hawaachi kabisa milele, hata wakati wao wamemwacha Yeye. Unabii mwingi kwamba Israeli ingetawanyika uliendana na ahadi nyingi kwamba Mungu siku moja angewakusanya tena.7

Siku hiyo ni leo—siku yetu. Kukusanyika kumeshaanza. Katika mwaka 1836, maelfu ya miaka tangu Musa awakusanye wana wa Israeli chini ya Mlima Sinai, Musa alitokea katika Hekalu la Kirtland kumkabidhi Joseph Smith “funguo za kukusanyika kwa Israeli kutoka pande nne za dunia” (Mafundisho na Maagano 110:11). Sasa, chini ya uelekezi wa wale wanaoshikilia funguo hizi, makabila ya Israeli yanakusanywa kutoka kila taifa ambapo watumishi wa Bwana wanaweza kwenda.

Rais Russell M. Nelson ameliita kusanyiko hili “jambo muhimu sana linalofanyika duniani leo. Hakuna kingine chochote cha kulinganishwa katika ukubwa, hakuna kingine chochote cha kulinganishwa katika umuhimu, hakuna kingine chochote cha kulinganishwa katika utukufu. Na kama utachagua, kama unataka, unaweza kuwa sehemu kubwa ya hilo.”8

Unalifanyaje hilo? Inamaanisha nini kuikusanya Israeli? Je, inamaanisha kurejesha makabila kumi na mbili katika nchi ambayo iliwahi kuwa ya urithi wao? Kimsingi, inamaanisha kitu kikubwa zaidi, cha milele zaidi. Kama Rais Nelson alivyofafanua:

“Tunapozungumza kuhusu kukusanyika, kiurahisi tunamaanisha kanuni hii ya kweli: Kila mmoja wa watoto wa Baba yetu wa Mbinguni, katika pande zote za pazia, anastahili kusikia ujumbe wa injili ya urejesho ya Yesu Kristo. …

Wakati wowote unapofanya kitu chochote kinachomsaidia mtu yeyote—upande wowote wa pazia—kuchukua hatua kuelekea kufanya maagano na Mungu na kupokea ibada zao muhimu za ubatizo na za hekaluni, unasaidia katika kukusanya Israeli. Ni rahisi kiasi hicho.”9

Hii inatokea, kama Isaya alivyosema, “mmoja mmoja” (Isaya 27:12) au, kama Yeremia alivyotabiri, “mji mmoja, na wawili wa jamaa moja” (Yeremia 3:14).

Kukusanya Israeli inamaanisha kuwarudisha watoto wa Mungu Kwake. Inamaanisha kuwarejesha kwenye mahusiano ya maagano yao na Yeye. Inamaanisha kuanzisha upya “taifa takatifu” Yeye alilopendekeza kulianzisha muda mrefu uliopita (Kutoka 19:6).

Njooni Nyumbani

Kama mtunza agano, wewe ni sehemu ya nyumba ya Israeli.10 Umekusanywa, na wewe ni mkusanyaji. Hadithi kuu ya karne-nyingi ambayo ilianza na agano kati ya Mungu na Ibrahimu inajengeka kwa kiwango kikubwa, na wewe ni mhusika muhimu. Sasa ni muda wakati “Yesu atasema kwa Israeli Yote, ‘Njooni Nyumbani.’”11

Huu ni ujumbe wa wakusanyaji: Njooni nyumbani kwenye agano. Njooni Nyumbani Sayuni. Njooni nyumbani kwa Yesu Kristo, Mtakatifu wa Israeli, na Yeye atawaleta nyumbani kwa Mungu, Baba yenu.

Chapisha