Agano la Kale 2022
Juni 27–Julai 3. 1 Wafalme 17–19: “Ikiwa Bwana ndiye Mungu Mfuate Yeye”


“Juni 27–Julai 3. 1 Wafalme 17–19: ‘Ikiwa Bwana ndiye Mungu Mfuate Yeye’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano la Kale 2022 (2021)

“Juni 27–Julai 3. 1 Wafalme 17–19,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2022

Picha
Eliya akiwa amesimama kando ya madhabahu inayowaka moto

Eliya Anabishana dhidi ya Makuhani wa Baali, na Jerry Harston

Juni 27–Julai 3

1 Wafalme 17–19

“Ikiwa Bwana ndiye Mungu Mfuate Yeye”

Unaposoma maandiko, unatumia imani, inayoandaa moyo wako na akili yako kusikia “sauti ndogo, ya utulivu” ya Roho (1 Wafalme 19:12).

Andika Misukumo Yako

Nyumba ya Israeli ilikuwa katika vurugu. Umoja na mafanikio yaliyopatikana chini ya Daudi na Sulemani yalikuwa yamepotea muda mrefu, na mahusiano ya maagano na Bwana ya taifa yalikuwa, kwa watu wengi, kumbukumbu ya mbali. Ufalme wa Israeli ulikuwa umegawanyika, kukiwa na makabila kumi yakiunda Ufalme wa Kaskazini wa Israeli na makabila mawili yakiunda Ufalme wa Kusini wa Yuda. Falme zote zilikuwa dhaifu kiroho, zikiongozwa na wafalme waliovunja maagano yao na Bwana na kuwashawishi wengine kufanya vivyo hivyo (ona 1 Wafalme 11–16). Ila ukengeufu ulikuwa mkubwa hasa katika Ufalme wa Kaskazini, ambapo Mfalme Ahabu aliwahimiza Israeli kumwabudu Baali mungu wa uongo.

Ilikuwa ni katika mazingira haya kwamba nabii Eliya aliitwa kuhubiri. Maelezo ya huduma yake yanaweka wazi kwamba imani binafsi katika Bwana inaweza kustawi miongoni mwa wenye haki hata katika mazingira ya uovu. Wakati mwingine Bwana anajibu kwenye imani kama hiyo kwa miujiza ya kuvutia na ya hadharani, kama kushuka kwa moto kutoka mbinguni. Lakini Yeye pia hufanya miujiza ya kimyakimya na binafsi kama kukidhi mahitaji binafsi ya mjane mwaminifu na mtoto wake. Na mara nyingi miujiza Yake ni ya binafsi kwamba inajulikana kwako tu—kwa mfano, wakati Bwana anapojidhihirisha Mwenyewe na mapenzi Yake kupitia “sauti ndogo, ya utulivu” (1 Wafalme 19:12).

Kwa mengi kuhusu Eliya, ona “Eliya” katika Kamusi ya Biblia.

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

1 Wafalme 17:1–16

Mwaliko wa kutoa dhabihu ni nafasi ya kutumia imani yangu.

Mwanzoni inaweza kuonekana vigumu kuelewa kwa nini nabii Eliya alimuomba mjane katika Sarepta kumpa chakula na maji kabla ya yeye mwenyewe na mwanawe mwenye njaa kula. Lakini ombi la Eliya lingeweza pia kuonekana kama baraka kwa familia hii ndogo. Walihitaji baraka za Bwana, na dhabihu mara nyingi huleta baraka—ikiwa ni pamoja na baraka ya imani thabiti.

Wakati unaposoma hadithi hii, jiweke katika nafasi ya huyu mjane wa kipekee. Nini kinachokuvutia kuhusu yeye? Fikiria nafasi ulizonazo kuonyesha imani yako—ikijumuisha nafasi za kutoa dhabihu. Je, ni kwa jinsi gani unaweza kuwa zaidi kama mjane huyu?

Ona pia Mathayo 6:25–33; Luka 4:24–26; Lynn G. Robbins, “Zaka—Amri Hata kwa Maskini,” Liahona, Mei 2005, 34–36.

1 Wafalme 18

“Ikiwa Bwana ndiye Mungu, mfuate yeye.”

Waisraeli huenda walihisi walikuwa na sababu za msingi za kumwabudu Baali licha ya amri ya Bwana, “Usiwe na miungu mingine ila mimi.” (Kutoka 20:3). Baali alijulikana kama mungu wa dhoruba na mvua, na baada ya miaka mitatu ya ukame, walikuwa na mahitaji makubwa ya dhoruba. Na kumwabudu Baali ilkuwa imekubaliwa kijamii na kuidhinishwa na mfalme na malkia. Unaposoma 1 Wafalme 18, fikiria hali zozote katika maisha yako ambazo zingeweza kulinganishwa na hali ambayo Waisraeli walikuwa wakikabiliwa nayo. Je, uliwahi kujikuta katika hali ya kusitasita kuhusu kumfuata Bwana kwa sababu mbadala unaonekana wenye busara na wenye kulazimisha? (ona 1 Wafalme18:21). Katika matukio yanayopatikana katika sura hii, unafikiri Bwana alikuwa anajaribu kufundisha nini kumhusu Yeye na kuhusu Baali? Ni uzoefu gani umekufundisha ukweli kama huo?

Inaweza kuwa ya kufurahisha kujua mambo ambayo Eliya alisema na kufanya katika sura hii ambayo yanaonyesha imani yake katika Bwana. Je, tunajifunza nini kutoka kwa Eliya kuhusu imani?

Ona pia Yoshua 24:15; 2 Nefi 2:26–28; D. Todd Christofferson, “Uchaguzi na Msimamo” (worldwide devotional for young adults, Jan. 12, 2020), ChurchofJesusChrist.org.

Picha
Eliya akiwa amesimama juu ya mwamba

Maelezo ya kiishara ya 1 Wafalme 19:11–12. Nabii, © Robert Booth Charles/Bridgeman Images

1 Wafalme 19:1–18

Bwana mara nyingi huzungumza katika njia za kimya na rahisi.

Wakati Malkia Yezebeli aliposikia kilichotokea kwa makuhani wake katika Mlima Karmeli, hakuwa ameongoka—alikuwa amegadhabika. Akihofia maisha yake, Eliya alikimbilia nyikani na kutafuta hifadhi kwenye pango. Hapo, alisumbuliwa na upweke na kukata tamaa, alikuwa na uzoefu na Bwana ambao ulikuwa tofauti na kile kilichokuwa kimetokea juu ya Mlima Karmeli. Uzoefu wa Eliya katika 1 Wafalme 19:1–18 unakufundisha nini kuhusu jinsi Bwana anavyowasiliana na wewe katika wakati wako wa uhitaji? Fikiria nyakati katika maisha yako ambapo ulipata uzoefu wa sauti Yake. Je, unahitaji kufanya nini ili kupokea mwongozo Wake kila mara?

Tafakari maneno na vifungu vilivyotumika katika mistari ifuatayo kuelezea jinsi Bwana anavyowasiliana nasi: Helamani 5:30; 3 Nefi 11:3–7; Mafundisho na Maagano 6:22–23; 8:2–3; 9:8–9; 11:12–14; 36:2.

Ona pia Zaburi 46:10; 1 Nefi 17:45; Russell M. Nelson, “Msikilize Yeye,” Liahona, Mei 2020, 88–92.

1 Wafalme 19:19–21

Kumtumikia Bwana huchukua nafasi ya kwanza juu ya mahitaji ya kidunia.

Ukweli kwamba Elisha alimiliki nira 12 za mafahali inaashiria kwamba labda alikuwa mtu tajiri. Je, ni kitu gani kinakuvutia kuhusu matendo yake yaliyoandikwa katika 1 Wafalme 19:19–21? Unawezaje kufuata mfano wa Elisha?

Ona pia Mathayo 4:18–22.

Picha
ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

1 Wafalme 17:1–16.Video “Elijah and the Widow of Zarephath” (ChurchofJesusChrist.org) na picha katika muhtasari huu vingeweza kuisaidia familia yako kuona vyema maelezo katika 1 Wafalme 17:1–16. Baada ya kusoma mistari na kuangalia nyenzo hizi, kila mwanafamilia anaweza kuorodhesha sifa za kuhamasisha ambazo mjane huyu alikuwa nazo. Bwana anatutaka sisi tufanye nini ili kuonyesha imani yetu?

1 Wafalme 18.“Eliya na makuhani wa Baali” (katika Hadithi za Agano la Kale) inaweza kusaidia familia yako kujifunza hadithi katika 1 Wafalme 18. Je, kuna mambo ambayo yanatuzuia sisi kuwa na msimamo mkamilifu kwa Bwana? Je, tunawezaje kuonyesha utashi wetu kwa kumchagua Yeye? (ona mstari wa 21).

1 Wafalme 19:11–12.Ni nini kingeweza kuisaidia familia yako kuelewa umuhimu wa kusikiliza “sauti ndogo, ya utulivu”? Mnaweza kusoma 1 Wafalme 19:11–12 kwa pamoja katika sauti nyororo au kuimba kimyakimya wimbo kuhusu Roho, kama vile “The Holy Ghost” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 105). Mnaweza kuongeza kelele za usumbufu kuonyesha jinsi Shetani anavyojaribu kutuzuia sisi tusiisikie, sauti ndogo, ya utulivu. Wanafamilia wanaweza kushiriki kile wanachofanya ili kusikia minong’ono ya Roho.

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa “The Holy Ghost,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 105.

Kuboresha Kujifunza Binafsi

Andika Misukumo Yako. Unapohisi Roho akizungumza na wewe, fikiria kuandika kile unachohisi Yeye anakwambia wewe. Wazo linalochukua kuweka misukumo hii katika maneno linaweza kukusaidia kutafakari na kuipa thamani.

Picha
mwanamke na mtoto

Mjane wa Sarepta, na Rose Datoc Dall

Chapisha