Agano la Kale 2022
Juni 27–Julai 3. 1 Wafalme 17–19: “Bwana Akiwa Ndiye Mungu, Mfuateni”


“Juni 27–Julai 3: 1 Wafalme 17–19: ‘Bwana Akiwa Ndiye Mungu, Mfuateni’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano la Kale 2022 (2021)

“Juni 27–Julai 3: 1 Wafalme 17–19,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2022

Picha
Eliya amesimama karibu na madhabahu ya moto

Eliya Anabishana na Makuhani wa Baali, na Jerry Harston

Juni 27–Julai 3

1 Wafalme 17–19

“Bwana Akiwa Ndiye Mungu, Mfuateni”

Watoto wengi wanapenda hadithi. Wasaidie watoto kutambua kweli katika hadithi zinazopatikana katika 1 Wafalme 17–19 zinazoweza kuimarisha imani yao katika Yesu Kristo.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waonyeshe watoto picha zilizo katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia. Waombe watoto washiriki kile wanachokijua kuhusu hadithi zinazoashiriwa na picha. Tunajifunza nini kutoka kwenye hadithi hizi?

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

1 Wafalme 17

Bwana hubariki wale walio na imani.

1 Wafalme 17 imerekodi mifano kadhaa ya imani kubwa. Kama matokeo ya kuwa na imani kubwa, Eliya alilishwa na kunguru wakati wa ukame, mjane na mwanawe walipata chakula chao maradufu, na Eliya alimfufua mwana wa mjane kutoka kwa wafu.

Shughuli Yamkini

  • Tundika picha au vitu ambavyo vinaendana na hadithi katika 1 Wafalme 17, kama vile ndege, mkate, au mvulana. Wasimulie watoto hadithi hizi (“Eliya Nabii” katika Hadithi za Agano la Kale inaweza kusaidia), na waalike watafute picha au kitu ambacho kinaendana na kila hadithi. Sisitiza kwamba Eliya na mjane walikuwa na imani katika Yesu Kristo na walipokea baraka kuu.

  • Wasaidie watoto wafikirie njia wanazoweza kuonyesha kwamba wana imani katika Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo, ambayo inamaanisha kwamba wanawaamini na kuwatumaini Wao. Imba pamoja nao wimbo kuhusu imani, kama vile “I Know My Father Lives” (Kitabu cha Nyimbo za watoto, 5).

1 Wafalme 18:17–39

Ninaweza kuchagua kumfuata Yesu Kristo.

Eliya aliwasihi watu wa Israeli wafanye uamuzi wa kumfuata Yesu Kristo. Wasaidie watoto kuona kwamba wanaweza kufanya uchaguzi huo huo.

Shughuli Yamkini

  • Waelezee watoto kwamba watu wa wakati wa Eliya hawakuwa na hakika kama walitaka kumfuata Bwana. Shiriki hadithi ya jinsi Eliya alivyowaalika wao wachague kumfuata Bwana, inayopatikana katika 1 Wafalme 18:17–39 (ona pia “ Eliya na Makuhani wa Baali” katika Hadithi za Agano la Kale). Waambie watoto kwa nini wewe ulichagua kumfuata Yesu Kristo, na uwaulize kwa nini wao wanachagua kumfuata pia.

  • Wasomee watoto kile Eliya aliwaambia watu: “Bwana Akiwa Ndiye Mungu, Mfuateni” (1 Wafalme 18:21). Inamaanisha nini kumfuata Kristo? Wasaidie watoto kufikiria mambo mahususi watakayofanya kumfuata Yesu Kristo, na waalike wachore picha zao wenyewe wakifanya mambo hayo.

    Picha
    mvulana ndogo

    Tunaweza kuchagua kumfuata Yesu Kristo.

1 Wafalme 19:9–12

Roho Mtakatifu huongea nami kwa sauti ndogo, tulivu.

Pamoja na mwongozo fulani, watoto wadogo wanaweza kutambua ushawishi wa Roho Mtakatifu katika maisha yao. Tafakari jinsi unavyoweza kuwasaidia.

Shughuli Yamkini

  • Wafanyie watoto muhtasari wa hadithi inayopatikana katika 1 Wafalme 19:9–12, na wasomee mstari wa 11–12. Waalike wao wafanye vitendo kuwakilisha upepo mkali, tetemeko, na moto. Kisha waalike wakae wametulia kabisa unaposoma mwisho wa mstari wa 12 katika sauti laini: “baada ya moto sauti ndogo, ya utulivu.” Waombe wajaribu kusema kwa sauti ndogo, ya utulivu. Waambie kuhusu nyakati ulipopata uzoefu wa mnong’ono kutoka kwa Roho Mtakatifu.

  • Wasaidie watoto kutambua nyakati wanapoweza kuwa wanahisi ushawishi wa Roho Mtakatifu. Kwa mfano, cheza au imba wimbo wa unyenyekevu kuhusu Yesu, na uwaulize jinsi wanavyohisi wanapofikiria kumhusu Yeye. Waulize jinsi wanavyohisi wakati wa shughuli zingine za unyenyekevu, kama vile wanapoomba pamoja na familia zao au wanapopokea sakramenti. Waelezee kwamba hisia hizi hutoka kwa Roho Mtakatifu. Waambie watoto jinsi nguvu za Roho Mtakatifu zimebariki maisha yako.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

1 Wafalme 17:8–16

Wakati Bwana anaponiomba nifanye dhabihu, ninaweza kutii kwa imani.

Mjane wa Sarepta alimtumainia Bwana na nabii Wake, ingawa alijua alikuwa ameombwa kufanya dhabihu kubwa. Hii hadithi inaweza kuwasaidia watoto wakati Bwana anapowaomba kufanya dhabihu.

Shughuli Yamkini

  • Wasomee watoto 1 Wafalme 17:8–16. Waalike waigize hadithi hii unapoisoma kwa mara ya pili. Simama katika vituo kadhaa wakati unaposoma na uwaulize jinsi ambavyo wangehisi kama wao wangekuwa Eliya au mjane. Waalike kushiriki kile wanachojifunza kutoka katika hadithi hii.

  • Mwalike mtoto achore ubaoni picha ya kile ambacho Bwana alimuomba mjane ampe Eliya (ona 1 Wafalme 17:12–13). Mwalike mtoto mwingine achore picha ya kile mjane alipata kama malipo (ona 1 Wafalme 17:15–16.). Ni nini baadhi ya vitu Bwana anatuomba tutoe dhabihu? Waalike watoto washiriki jinsi ambavyo wamebarikiwa kwa kufanya dhabihu.

1 Wafalme 18:17–39

Ninaweza kuchagua kumfuata Yesu Kristo.

Waisraeli walikuwa wanasita kuhusu kumfuata Bwana. Tafakari jinsi unavyoweza kuwatia moyo watoto kuwa na dhamira ya dhati katika ufuasi wao.

Shughuli Yamkini

  • Mpe kila mtoto kazi ya kusoma mistari kadhaa kutoka katika 1 Wafalme 18:17–39 na wachore picha ya kile mstari wake unaelezea. Wasaidie watoto kuelewa mistari hii kama inahitajika. Kisha waache watumie picha zao kusimulia hadithi hiyo. Ni nini hadithi hii inatufundisha kuhusu Bwana?

  • Waombe watoto wazungumze kuhusu nyakati walipohitaji kufanya uamuzi kati ya vitu viwili tofauti. Nini kiliwasaidia kuamua? Wasaidie wafikirie hali watakapohitajika kuamua kumfuata au kutokumfuata Yesu Kristo. Ni kweli gani kutoka kwenye hadithi katika 1 Wafalme 18:17–39 zinazoweza kuwasaidia kuamua?

1 Wafalme 19:9–12

Roho Mtakatifu huongea nami kwa sauti ndogo, ya utulivu.

Ulimwengu umejaa kelele za kuvuruga ambazo zinafanya kuwa vigumu kusikia sauti ndogo, ya utulivu ya Roho. Ni kwa jinsi gani utawasaidia watoto kuisikia?

Shughuli Yamkini

  • Alika watoto kusikiliza kwa makini unapowasomea wao 1 Wafalme 19:11–12 kwa sauti ndogo sana. Waalike wapekue 1 Wafalme 19 kutafuta mistari uliyosoma na wajifunze kile Eliya alikuwa anafanya. Zungumza kuhusu kile walitakiwa kufanya ili wasikie kile ulichokuwa unasema, na wasaidie kulinganisha hiki na kile tunachotakiwa kufanya ili kuisikia ile “sauti ndogo, ya utulivu” ya Roho. Waache watoto wachukue zamu kusoma kwa sauti ndogo mistari mingine kutoka katika 1 Wafalme 19 wakati watoto wengine wanatafuta mistari hiyo katika maandiko.

  • Shiriki pamoja na watoto baadhi ya maandiko ya ziada ambayo yanaelezea jinsi Roho anavyowasiliana nasi (ona Mwongozo wa Maandiko,“Msukumo, Tia msukumo,” scriptures.ChurchofJesusChrist.org). Waombe watoto wazungumze kuhusu nyakati ambapo walihisi Roho Mtakatifu akiwaongoza au akiwashuhudia. Walikuwa wanafanya nini? Ni nini kinaweza kutuvuruga tusiweze kumtambua Roho? Someni pamoja Moroni 4:3, na uwatie moyo watoto kuchagua kitu kimoja watakachofanya ili “daima Roho wake apate kuwa pamoja nao.”

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Alika watoto wafikirie kitu ambacho wangependa kufanya kwa sababu ya kile walichojifunza leo. Kwa mfano, wanaweza kuweka lengo la kiroho, kiakili, kimwili, au kijamii ili kuwa zaidi kama Yesu Kristo.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wasaidie watoto kumtambua Roho. “Mojawapo ya mambo muhimu unayoweza kufanya kama mwalimu ni kuwasaidia wale unaowafundisha kutambua ushawishi wa Roho Mtakatifu. … Wasaidie [watoto] kuhusisha hisia zao za kiroho na ushawishi wa Roho Mtakatifu.” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 11).

Chapisha