Agano la Kale 2022
Julai 25–31. Esta: “Umekuja … kwa Wakati Kama Huu”


“Julai 25–31. Esta: ‘Umekuja … kwa Wakati Kama Huu’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano la Kale 2022 (2021)

“Julai 25–31. Esta,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2022

Picha
Esta akiomba

Esta, na James Johnson

Julai 25–31

Esta

Esta: “Umekuja … kwa Wakati Kama Huu”

Maandiko yote yanamshuhudia Yesu Kristo. Tafakari jinsi utakavyoweza kuwasaidia watoto kuona ushawishi wa Mwokozi katika hadithi ya Esta.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Onesha picha ya Esta (ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia.). Wakati watoto wanaposhikilia picha, waalike washiriki kitu wanachokijua kuhusu hadithi ya Esta.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Esta 2:5–7

Naweza kuitumikia familia yangu.

Wakati wazazi wa Esta walipofariki, Mordekai binamu yake alimtunza. Unaweza kutumia uzoefu wao kama fursa ya kuzungumzia kuhusu kuwatumikia wanafamilia wetu.

Shughuli Yamkini

  • Ubaoni, chora maumbo ambayo yanamwakilisha Esta, wazazi wake, na Mordekai binamu yake. Elezea kwamba wazazi wa Esta walifariki, kwa hiyo Esta alihitaji mtu wa kumtunza. Wasomee watoto Esta 2:7 na waombe watoto wasikilize kile Mordekai alichofanya. Wasaidie watoto kufikiria juu ya mahitaji wanafamilia wao wanaweza kuwa nayo ambayo watoto wanaweza kusaidia.

  • Waalike baadhi ya watoto waigize kitu cha ukarimu ambacho wangeweza kufanya ili kumtumikia mtu katika familia zao, na waombe watoto wengine wabashiri kile wanachokifanya. Waalike wazungumze kuhusu vitu wanavyofanya kubariki familia zao, na uwaambie kuhusu baadhi ya vitu unavyofanya.

  • Imbeni wimbo kuhusu kusaidia familia zetu, kama vile “When We’re Helping” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 198). Shiriki ushuhuda wako kwamba kusaidia familia zetu hutufanya tuwe na furaha.

Esta 4:15–16

Naweza kuwa jasiri.

Watoto unaowafundisha watakabiliwa na hali ambapo wanahitaji msaada wa Bwana ili kuwa jasiri. Ni kwa jinsi gani utawasaidia kujifunza kutoka kwa mfano wa ujasiri wa Esta?

Shughuli Yamkini

  • Je, watoto unaowafundisha wanajua inamaanisha nini kuwa jasiri? Shiriki maana rahisi, kama vile “Kuwa jasiri humaanisha kufanya kile kilicho sahihi hata kama unaogopa.” Shiriki hadithi ya Esta (ona “Malkia Esta” katika Hadithi za Agano la Kale), na wasaidie watoto kuona jinsi Esta alivyokuwa jasiri. Waache watoto watumie maumbo kwenye ukurasa wa shughuli ya wiki kusimulia tena hadithi hii.

  • Onyesha picha ya Esta (ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia). Imba pamoja na watoto wimbo kuhusu kuwa jasiri, kama vile “I Will Be Valiant” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 162). Taja maneno au vifungu vya maneno katika wimbo ambavyo vinamuelezea Esta, na ushuhudie kwamba Mwokozi anaweza kuwasaidia watoto kuwa jasiri.

  • Waambie watoto kuhusu nyakati ambapo Yesu Kristo alikuwa jasiri; kwa mfano, wakati Alipoteseka kwa ajili ya dhambi zetu, huko Gethsemane na msalabani (ona Mathayo 26:36–39; 27:33–35). Waombe watoto kueleza kuhusu wakati walipokuwa jasiri (fikiria kuwasiliana na familia zao mapema ili kuwapa watoto mifano kadhaa). Ni nini kiliwasaidia kuwa jasiri? Waambie watoto jinsi Bwana alivyokusaidia wewe kuwa jasiri ulipokuwa na uoga.

    Picha
    Esta na mfalme

    Esta mbele ya mfalme, na Minerva K. Teichert

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Esta 4:14

Ninaweza kuwa chombo katika mikono ya Mungu.

Wakati Esta alipokuwa na uoga, Mordekai alimtia moyo kwa kumfundisha kwamba labda Bwana alikuwa amemfanya kuwa malkia “kwa ajili ya wakati kama huu” (Esta 4:14). Tafakari jinsi Bwana anavyowaandaa watoto unaowafundisha kwa nafasi zao za kuwabariki wengine.

Shughuli Yamkini

  • Mwalike mtu acheze wimbo kwa ajili ya watoto kwenye chombo cha muziki, au uonyeshe picha ya mtu akicheza chombo cha muziki. Zungumza kuhusu inamaanisha nini kuwa chombo katika mikono ya Mungu. Rejelea pamoja na watoto hadithi ya Esta (ona “Malkia Esta” katika Hadithi za Agano la Kale), na waalike wao wazungumze kuhusu jinsi Esta alivyokuwa chombo cha Bwana katika kutimiza makusudi Yake. Tunawezaje kuwa vyombo vya Bwana?

  • Baada ya kurejelea hadithi ya Esta, bandika kadi iliyo na jina la wahusika kutoka katika hadithi hii kwenye mgongo wa kila mtoto. Waalike watoto kujaribu kujua ni jina la nani lililo kwenye migongo yao kwa kuwauliza watoto wengine maswali kama “Mtu huyu alikuwa mwema?” au “Mtu huyu alikuwa mwanamke?” Kisha jadili jinsi Mordekai na Esta walivyokuwa vyombo kwa Bwana kuwaokoa Wayahudi.

Esta 3:1–11; 4:10–17

Baba wa Mbinguni hunisaidia kuwa jasiri wakati nikiwa na woga.

Lini umewaona watoto unaowafundisha wakiwa jasiri? Ni uzoefu gani unaoweza kuushiriki wakati ulipohitaji msaada wa Bwana wa kuwa jasiri?

Shughuli Yamkini

  • Andika ubaoni Mordekai alionyesha ujasiri kwa … na Esta alionyesha ujasiri kwa … Waalike baadhi ya watoto wasome Esta 3:1–11 na wengine wasome Esta 4:10–17. Waombe watumie kile wanachosoma kukamilisha sentensi ubaoni. Kisha andika Nitaonyesha ujasiri kwa … na waalike watoto waorodheshe vitu ambavyo Baba wa Mbinguni anawataka wafanye ambavyo vinahitaji ujasiri. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa kama Mordekai na Esta?

  • Waalike watoto wafikirie hali ambazo wao wanakabiliwa nazo ambazo zinaweza kuwa vigumu kufanya kitu sahihi. Andika ubaoni maneno ya ujasiri ya Esta “Kisha nitaingia kwa mfalme, … nami nikiangamia, na niangamie” (Esta 4:16). Wasaidie watoto kutumia maneno ya Esta kwao wenyewe kwa kubadili “nitaingia kwa mfalme” kwa uamuzi wa haki lakini mgumu watakaohitajika kuufanya. Kisha waalike wabadili “kuangamia” na kitu kisicho cha kupendeza ambacho kinaweza kuja kwa kufanya kile kilicho sahihi. Kwa nini ni vyema kufanya kitu sahihi, hata kama kuna matokeo magumu?

  • Onesha video “Choose the Harder Right” (ChurchofJesusChrist.org), na waalike watoto waamue juu ya “gumu lilio sahihi” katika maisha yao ambalo watachagua. Jadili jinsi Yesu Kristo ni mfano wa kanuni hii.

Esta 4:1–3, 10–17

Kufunga kunaweza kunisaidia mimi na kuwabariki wengine.

Wakati kulikuwa na hitaji, Esta na Wayahudi walifunga. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kuelewa baraka za kiroho za kufunga?

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto kutengeneza orodha ya vitu ambavyo wangeweza kufungia (ikiwa inahitajika, wanaweza kutazama “Kufunga na Matoleo ya Mfungo” katika Kweli kwa Imani,66-69). Kisha waombe wasome Esta 4:1–3, 10–17 ili kugundua kwa nini Wayahudi na Esta walifunga. Wahimize watoto wafikirie sababu ambayo wangeweza kuhitaji msaada maalumu kutoka kwa Bwana, na upendekeze watumie sababu hiyo kama sehemu ya mfungo wao wakati wa Jumapili ya mfungo ijayo.

  • Waalike watoto wajifanye wanamwelezea rafiki kwa nini wao hufunga. Wangesema nini? Waelekeze kwenye Mwongozo wa Maandiko, “Mfungo, Kufunga” (scriptures.ChurchofJesusChrist.org) kama wanahitaji msaada. Shiriki uzoefu wako wakati ulipofunga ili upokee msaada wa Bwana. Waalike watoto washiriki uzoefu ambao waliweza kuupata kwa kufunga.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Imbeni pamoja wimbo kuhusu kanuni uliyojifunza katika darasa leo (ona kiambatisho cha mada katika Kitabu cha Nyimbo za Watoto kwa mapendekezo). Waalike watoto waimbe wimbo huo pamoja na familia zao.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Ishi kile unachofundisha. Ufundishaji wako utakuwa na nguvu zaidi kama utashuhudia kutoka kwenye uzoefu wako binafsi kuhusu baraka za kuishi injili. Unapochagua kanuni za kuwafundisha watoto, tafakari jinsi unavyoweza kuishi kanuni hizo kwa ukamilifu zaidi. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 13–14.)

Chapisha