Agano la Kale 2022
Agosti 1–7. Ayubu 1–3; 12–14; 19; 21–24; 38–40; 42: “Bado Nitamtumaini”


“Agosti 1–7. Ayubu 1–3; 12–14; 19; 21–24; 38–40; 42: ‘Bado Nitamtumaini’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano la Kale 2022 (2021)

“Agosti 1–7. Ayubu 1–3; 12–14; 19; 21–24; 38–40; 42,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2022

wanaume watatu wakiongea na mtu aliyeketi chini.

Hukumu za Ayubu, na Joseph Brickey

Agosti 1–7

Ayubu 1–3; 12–14; 19; 21–24; 38–4042

“Bado Nitamtumaini”

Unapojifunza tukio la Ayubu, ni jumbe zipi unazopata kwa ajili ya maisha yako mwenyewe? Ni jumbe zipi kati ya hizi unahisi watoto unaowafundisha wanahitaji kuzisikia?

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waonyesha watoto picha ya Ayubu (ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia). Waulize watoto jinsi wanavyofikiria mtu katika picha anavyoweza kuwa anahisi. Waalike washiriki kitu chochote kingine wanachojua kumhusu Ayubu.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Ayubu 1–2; 13:15

Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo watanisaidia katika nyakati ngumu ninapokuwa na imani Kwao.

Ayubu alimtumaini Mungu na aliweza kubaki mwaminifu hata wakati alipokumbana na majaribu makali. Hadithi ya Ayubu inaweza kuwasaidia watoto kuimarisha imani yao katika Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo hivyo watakuwa wamejiaanda kukabiliana na majaribu yao magumu.

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto washiriki kile wanachojua kumhusu Ayubu, na uwasaidie kuelewa kile kilichomtokea (ona Ayubu 1–2; “Ayubu” katika Hadithi za Agano la Kale). Waulize watoto jinsi ambavyo wangehisi kama wangekuwa Ayubu. Ni nani anaweza kutusaidia wakati mambo mabaya yanapotokea katika maisha yetu? Onyesha picha ya Yesu Kristo, na ueleze kwamba imani ya Ayubu katika Bwana ilimsaidia wakati wa majaribu yake (ona Ayubu 1:21).

  • Wasomee watoto maneno ya Ayubu katika Ayubu 13:15: “Nitamtumaini yeye.” Ili kuwasaidia watoto kuelewa kutumaini katika Mungu kunamaanisha nini, zungumza nao kuhusu watu wengine wanaowatumaini. Kwa mfano, ni nini tunachotumaini wazazi wetu kufanya? Je, ni nini tunachotumaini walimu wetu kufanya? Je, ni nini tunachotumaini Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo kufanya. Elezea tumaini lako kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo, na uwasaidie watoto kufikiria njia wanazoweza kuwaonyesha kwamba wanawapenda na kuwatumaini.

Ayubu 19:25

Yesu Kristo ni Mkombozi wangu.

Ayubu aliweza kustahimili majaribu na mateso yake kwa sababu ya imani yake katika Bwana. Ni kwa jinsi gani utawasaidia watoto kujenga imani yao katika Yesu Kristo, Mkombozi wetu?

Shughuli Yamkini

  • Onesha picha ya Yesu msalabani au akizikwa kaburini (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 57, 58). Waombe watoto waelezee nini kinatokea katika picha. Wasomee watoto ushuhuda wa Ayubu katika Ayubu 19:25. Onyesha picha ya Mwokozi aliyefufuka (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 59, 60; ona pia ukurasa wa shughuli wa wiki hii), na ushuhudie kwamba Yesu Kristo alifufuka na yu hai leo. Kwa nini tuna shukrani kwamba Yesu Kristo alifufuka?

  • Onyesha picha ya Ayubu, na uelezee kwamba Ayubu alikuwa katika maumivu mengi kwa sababu ngozi yake yote ilikuwa na majipu. Alipoteza nyumba yake, na watoto wake walifariki. Lakini Ayubu alijua kitu muhimu sana ambacho kilimpa faraja. Soma Ayubu 19:25, na uwaulize watoto kile Ayubu alichojua. Shiriki na watoto jinsi unavyojua kwamba Yesu Kristo yu hai, na waalike wao kushiriki ushuhuda wao juu Yake.

    mtu akitazama juu

    Ayubu, na Gary L. Kapp

  • Waalike watoto wapake rangi ukurasa wa shughuli ya wiki hii. Wapokuwa wanafanya hivyo, cheza au imba wimbo kuhusu Ufufuo wa Yesu, kama vile “Did Jesus Really Live Again?” au “Jesus Has Risen” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 64, 70). Waombe washiriki jinsi wanavyohisi kuhusu Yesu, na uwasaidie kuelewa kwamba tunaweza kuwa na hisia nzuri kutoka kwa Roho Mtakatifu ili kutusaidia kujua kwamba Yesu Kristo ni mtu halisi.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Ayubu 1–2; 1219

Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo watanisaidia kushinda changamoto zangu ninapokuwa na imani Nao.

Kila mtu anakuwa na siku zake ngumu, na baadhi ya watu wana majaribu ambayo yanadumu muda mrefu. Imani ya Ayubu katika Mungu ilimfanya astahimili wakati wa majaribu yake. Fikiria jinsi hadithi hii inaweza kuwasaidia watoto kujenga imani yao katika Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo ili kwamba waweze kupambana na majaribu yao, sasa na wakati ujao.

Shughuli Yamkini

  • Waombe watoto washiriki kile wanachokijua kuhusu hadithi ya Ayubu. Je, alikuwa mtu wa aina gani? Ni nini kilichomtokea? Ni kwa jinsi gani alijibu changamoto zake? Waelekeze kwenye mistari katika Ayubu 1–2 ili kuwasaidia kusimulia hadithi hii (ona Ayubu 1:1, 13–22; 2:7–10; ona pia “Ayubu” katika Hadithi za Agano la Kale). Waalike watoto washiriki kile wanachohisi kwamba ni ujumbe mkuu wa hadithi ya Ayubu.

  • Onyesha picha chache za Yesu Kristo akichangamana na wengine, na uwaulize watoto kile wanachohisi picha hizi zinatufundisha kuhusu Yesu Kristo ni nani na Yeye yukoje. Je, ni kitu gani kingine tunachokijua kumhusu Yeye? Waalike watoto wasome baadhi ya mistari ifuatayo kutafuta baadhi ya vitu ambavyo Ayubu alijua kuhusu Bwana: Ayubu 12:10, 13, 16; 19:25–27. Kwa nini ni muhimu kujua vitu hivi kuhusu Mwokozi?

  • Waalike watoto wasome Ayubu 19:14–19, na uwaulize kile mistari hii inasema kuhusu jinsi watu wengine walivyokuwa wanamtendea Ayubu. Tungeweza kuhisi vipi kama haya yangetutokea sisi? Waalike watoto wasome Ayubu 19:23–27 ili kujua ni jinsi gani Ayubu alipata faraja katika hali hii. Mistari hii inatufundisha nini kuhusu Mwokozi? Kwa nini ni muhimu kujua kwamba Anaishi na Anatupenda? (ona Yohana 17:3).

  • Imbeni pamoja wimbo ambao unamshuhudia Yesu Kristo, kama vile “I Know That My Redeemer Lives” (Nyimbo za Kanisa, na.136). Je, wimbo unapendekeza nini kuhusu kwa nini ni muhimu kuwa na ushuhuda kwamba Yesu Kristo Anaishi? Waambie watoto ni kwa jinsi unajua kwamba Mwokozi Anaishi na kwa nini una shukrani kwa ajili ya elimu hiyo. Wahimize washiriki hisia zao na shuhuda zao pia.

Ayubu 19:13–19; 22:5

Marafiki wema huinuana na kutiana moyo wao kwa wao.

Wakati Ayubu alikuwa anasumbuka, marafiki zake walisema kwamba Mungu alikuwa anamuadhibu kwa sababu alikuwa ametenda dhambi. Hadithi hii inaweza kukusaidia kuwafundisha watoto njia bora ya kujibu wakati rafiki anapokuwa na changamoto (ona Ayubu 16:1–5).

Shughuli Yamkini

  • Waombe watoto warejelee vitu vingi vigumu ambavyo vilimtokea Ayubu (ona Ayubu 1:13–19; 2:7). Someni pamoja Ayubu 19:14, 19, mkitafuta jinsi marafiki wa Ayubu walijibu kuhusu majaribu yake (ona pia Ayubu 22:1–5). Waalike watoto wafikirie kwamba walikuwa marafiki wa Ayubu—je, wangejaribu vipi kumsaidia? Wahimize wafikirie rafiki ambaye anaweza kuwa anapitia wakati mgumu na wapange kitu wachoweza kufanya kuonyesha upendo na msaada kwa rafiki yao.

  • Waombe watoto waorodheshe baadhi ya sifa za rafiki mwema na wamtaje rafiki mwenye sifa hizi. Onyesha picha ya Yesu Kristo. Ni kwa njia gani Yesu ni rafiki mwema wa kila mmoja wetu? Je, ni kwa jinsi gani sisi tunaweza kufuata mfano Wake?

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto washiriki na mwanafamilia au rafiki njia ambayo Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanaweza kuwasaidia wakati wanapokuwa na wakati mgumu.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Shuhudia juu ya baraka zilizoahidiwa. Wakati Bwana anapotoa amri, mara nyingi Yeye huhaidi baraka kwa kutii amri hiyo. Wakati unapowaalika watoto wa msingi kuishi kanuni fulani, shiriki ahadi ambazo Mungu amezifanya kupitia manabii kwa wale wanaoishi kanuni hiyo. Unaweza pia kutoa ushuhuda wa baraka ambazo umepokea kwa kuishi kanuni hiyo.