Agano la Kale 2022
Agosti 1–7. Ayubu 1–3; 12–14; 19; 21–24; 38–40; 42: “Bado Nitamtumainia Yeye”


“Agosti 1–7. Ayubu 1–3; 12–14; 19; 21–24; 38–40; 42: ‘Bado Nitamtumainia Yeye,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano la Kale 2022 (2021)

“Agosti 1–7. Ayubu 1–3; 12–14; 19; 21–24; 38–40; 42 ,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Famila: 2022

wanaume watatu wakizungumza na mtu aliyeketi chini

Hukumu ya Ayubu, na Joseph Brickey

Agosti 1–7

Ayubu 1–3; 12–14; 19; 21–24; 38–4042

“Bado Nitamtumainia Yeye”

Unaposoma kuhusu Ayubu, Roho atakuongoza kugundua kweli muhimu zinazohusika kwako. Andika kile unachogundua, na tafakari jinsi kweli hizi zinavyohusika kwako.

Andika Misukumo Yako

Ni kawaida kujiuliza kwa nini mambo mabaya hutokea kwa watu wazuri—au kwa maana hiyo, kwa nini mambo mazuri hutokea kwa watu wabaya. Kwa nini Mungu, ambaye ni mwenye haki, anaruhusu hayo. Maswali kama haya yanapatikana kupitia uzoefu wa Ayubu, mmoja wa hao watu wazuri ambao mambo mabaya yalimtokea. Kwa sababu ya majaribu ya Ayubu, marafiki zake walijiuliza kama yeye kweli alikuwa mtu mzuri baada ya yote hayo. Ayubu alithibitisha uadilifu wake mwenyewe na kujiuliza ikiwa kweli Mungu alikuwa mwenye haki kwa wote. Lakini licha ya mateso yake na kujiuliza, Ayubu alidumisha uadilifu wake na imani katika Yesu Kristo. Katika kitabu cha Ayubu, imani inapimwa na kujaribiwa lakini haiachwi kabisa. Hii haimaanishi kwamba maswali yote yanajibiwa. Lakini kitabu cha Ayubu kinafundisha kwamba mpaka yanapojibiwa, maswali na imani vinaweza kuendelea kuwepo pamoja, na bila kujali kile kinachotokea sasa, “Bado Nitamtumainia Yeye” (Ayubu 13:15).

Kwa ajili ya muhtasari wa kitabu cha Ayubu, ona “Ayubu” katika Mwongozo kwenye Maandiko (maandiko.ChurchofJesusChrist.org).

Learn More image
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Ayubu 1–3; 12–13

Kutumaini kwangu katika Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo kunaweza kunisaidia mimi kubaki mwaminifu katika hali zote.

Sura za ufunguzi za Ayubu zinalenga kusisitiza jukumu la Shetani kama adui yetu au mshitaki wetu, na sio kuelezea jinsi Mungu na Shetani wanavyotangamana. Unaposoma madai ya Shetani kuhusu Ayubu (ona Ayubu 1:9–11; 2:4–5), unaweza kutafakari ikiwa hayo hayo yanaweza kusemwa kukuhusu wewe. Unaweza kujiuliza mwenyewe, Je, sababu zangu ni zipi za kubaki mwaminifu kwa Mungu? Tafakari majaribu aliyopewa Ayubu na mwitikio wake (ona Ayubu 1:20–22; 2:9–10). Unajifunza nini kutoka kwake ambacho kinaweza kukusaidia kuitikia changamoto zako?

Ingawa Ayubu alikuwa akijaribu kubaki mwaminifu, majaribu yake na mateso yaliendelea (gundua maombolezo yake katika sura ya 3). Kimsingi, mateso yake yalionekana kuzidi sana, na marafiki zake walipendekeza kwamba Mungu alikuwa anamwadhibu (ona Ayubu 4–5; 8; 11). Unaposoma sehemu ya jibu la Ayubu katika sura ya 12–13, fikiria Kile Ayubu alichofahamu kuhusu Mungu ambacho kilimwezesha kuendelea kuamini, licha ya mateso yake na maswali yasiyojibika. Unafahamu nini kuhusu Mungu ambacho kinakusaidia kukabiliana na changamoto? Ni kwa jinsi gani umekuja kujua kweli hizi zote, na ni kwa jinsi gani zimeimarisha imani yako?

Ayubu 19

Yesu Kristo ni Mkombozi wangu.

Wakati mwingine ukweli muhimu unafunuliwa kwetu katikati ya uchungu mkali. Tafakari majaribu Ayubu aliyoyaelezea katika Ayubu 19:1–22 na kweli alizozitangaza katika Ayubu 19:23–27. Kisha tafakari ni kwa jinsi gani unajua kwamba Mkombozi wako yu hai. Ni tofauti ipi maarifa haya yanaleta wakati unapokabiliana na majaribu magumu?

Ona pia Mafundisho na Maagano 121:1–12; 122.

mwanamume akitazama mbinguni

Ayubu, na Gary L. Kapp

Ayubu 21–24

“Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.”

Unaposoma mjadala zaidi kati ya Ayubu na rafiki zake kuhusu sababu ya mateso ya Ayubu, unaweza kutafakari jinsi ambavyo ungejibu maswali katikati ya mjadala wao: Kwa nini wakati mwingine watu wema huteseka na waovu wakati mwingine hawaadhibiwi? Fikiria kuhusu hili unaposoma Ayubu 21–24. Je, unajua nini kuhusu Baba wa Mbinguni na mpango Wake ambao unaweza kutusaidia kutoa majibu? Ona, kwa mfano, 2 Nefi 2:11–13; Mosia 23:21–23; 24:10–16; Ibrahimu 3:22–26; Dallin H. Oaks, “Upinzani katika Mambo Yote,” Liahona, Mei 2016, 114–17.

Ona pia L. Todd Budge, “Uaminifu Endelevu na Thabiti,” Liahona, Nov. 2019, 47–49.

Ayubu 38; 40; 42

Mtazamo wa Mungu ni mkubwa kuliko wangu.

Akisumbuliwa na tuhuma za rafiki zake (ona Ayubu 16:1–5; 19:1–3), Ayubu alimlilia Mungu tena na tena akitafuta maelezo ya mateso yake (ona Ayubu 19:6–7; 23:1–931). Mzee Neal A. Maxwell aliona kwamba “tunapokosa subira kwenye muda na Mungu mwenye uweza,”kama Ayubu alivyoonekana kuwa, “hakika tunapendekeza kwamba tunajua kulicho bora. Inashangaza, sivyo—sisi tunaovaa saa za mkononi tunatafuta kumshauri Yeye ambaye anaangalia saa na kalenda ya ulimwengu mzima” (“Tumaini kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo,” Ensign, Nov. 1998, 63). Tafakari maneno haya unaposoma jibu la Mungu kwa Ayubu katika sura ya 38 na 40. Ni kweli zipi alikuwa akimfundisha Ayubu? Je, kwa nini kweli hizi ni muhimu kwetu kujua wakati tunaposhindana na adui na maswali hapa katika maisha ya duniani? Je, ni kitu gani kinakuvutia kuhusu jibu la Ayubu katika Ayubu 42:1–6?

ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Ayubu 1:20–22.Kujua jinsi ambavyo Ayubu yaweza kuwa alihisi, kama ilivyoelezwa katika mistari hii, familia yako ingeweza kusoma “Ayubu” katika Hadithi za Agano la Kale au igiza Ayubu 1:13–22. Tunaweza kujifunza nini kutokana na mfano wa Ayubu?

Ayubu 14:14.Tungewezaje kujibu swali la Ayubu katika mstari huu? Ni kwa jinsi gani Alma 11:42–44 inatusaidia? (Ona pia video “He Lives—Celebrate Easter Because Jesus Christ Lives,” ChurchofJesusChrist.org.)

Ayubu 16:1–5.Je, tumewahi kuwa kama marafiki wa Ayubu, waliomhukumu na kumkosoa Ayubu wakati alipohitaji faraja? (ona Ayubu 16:1–4; ona pia Yohana 7:24). Ni kwa jinsi gani maneno yetu yanaweza kuwaimarisha wengine katika huzuni yao? (ona Ayubu 16:5).

Ayubu 19:23–27.Baada ya kusoma mistari hii, wanafamila wanaweza kushiriki jinsi wanavyojua kuwa Mwokozi wetu yu hai. Mnaweza kufanya kazi kwa pamoja kuunganisha maneno yenu ya ushuhuda (au michoro ya watoto ya Mwokozi) katika kitabu, kama vile shajara ya familia (ona mstari wa 23). Mngeweza pia kuimba wimbo unaomshuhudia Mwokozi, kama vile “I Know That My Redeemer Lives” (Nyimbo za Kanisa, na. 136), na kushiriki vifungu vinavyoimarisha imani yenu katika Yeye.

Ayubu 23:8–11.Inamaanisha nini “kutoka” kwenye majaribu yetu “kama dhahabu”? (ona pia video “The Refiner’s Fire,” ChurchofJesusChrist.org). Nani tunamjua ambaye amefanya hili? Watoto wanaweza kufurahia kutengeneza kitu kwa kutumia maneno kutoka katika mstari wa 10 yakiwa yameandikwa juu yake. Mnaweza pia kujadili jinsi Yesu Kristo alivyoshinda majaribu Yake (ona Luka 22:41–44; Mafundisho na Maagano 19:16–19).

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “My Redeemer Lives,” Nyimbo za Kanisa, na. 135.

Kuboresha Kujifunza Binafsi

Vuta taswira. Umaizi wa maana unaweza kuja wakati tunapojaribu kujiweka kwenye maandiko. Kwa mfano, kujiweka katika hali ya Ayubu kunaweza kukusaidi kutafakari uhusiano wako na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

wanaume wakizungumza na mtu aliyeketi chini

Ayubu na Rafiki Zake, na Ilya Repin