Agano la Kale 2022
Agosti 22–28. Zaburi 102–103; 110; 116–119; 127–128; 135–139; 146–150: “Kila Mwenye Pumzi na Amsifu Bwana”


“Agosti 22–28. Zaburi 102–103; 110; 116–119; 127–128; 135–139; 146–150: ‘Kila Mwenye Pumzi na Amsifu Bwana’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano la Kale 2022 (2021)

“Agosti 22–28. Zaburi 102–103; 110; 116–119; 127–128; 135–139;146–150,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2022

Picha
Kristo akiwa amevaa joho jekundu akizungukwa na watu waliopiga magoti

Kila Goti Litapigwa, na J. Kirk Richards

Agosti 22–28

Zaburi 102–103; 110; 116–119; 127–128; 135–139; 146–150

“Kila Mwenye Pumzi na Amsifu Bwana”

Zaburi 119:105 inafundisha kwamba neno la Mungu ni “mwanga wa njia [yako].” Unaposoma Zaburi, andika virai na mawazo yanayokupa msukumo na kukusaidia kuangaza njia yako ya kurudi kwa Baba wa Mbinguni.

Andika Misukumo Yako

Jina la utamaduni la Kiyahudi kwa kitabu cha Zaburi ni neno la Kiebrania linalomaanisha “sifa.” Neno hilo, Tehillim, linahusiana pia na shangilio la “haleluya” (maana yake “msifu Yehova” au “msifu Bwana”). Kama ungechagua neno moja kujumuisha ujumbe mkuu wa Zaburi, “sifa” lingekua chaguo zuri. Baadhi ya Zaburi zinajumuisha mwaliko wa moja kwa moja wa “kumsifu Bwana” (ona hasa Zaburi 146–50), na zote zinaweza kutoa msukumo wa hisia ya kuabudu na kusifu. Zaburi inatualika sisi kutafakari juu ya nguvu za Bwana, katika huruma Yake, na katika mambo makubwa ambayo Yeye ameyafanya. Kamwe hatuwezi kumlipa Yeye katika mojawapo ya haya, ila tunaweza kumsifu Yeye kwa ajili ya hayo. Kusifu huku kunaweza kuchukua mifumo tofauti kwa watu tofauti—kunaweza kujumuisha kuimba, kusali, au kutoa ushuhuda. Mara nyingi hukuongoza katika ahadi za kina kwa Bwana na kwenye kufuata mafundisho Yake. Vyovyote vile, “kumsifu Bwana” inachomaanisha katika maisha yako, unaweza kupata mwongozo zaidi kufanya hivyo wakati unaposoma na kutafakari Zaburi.

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Zaburi 102–3116

Bwana anaweza kunifariji katika mateso yangu.

Angalia jinsi Zaburi 102:1–11 inavyoelezea hisia za wasiwasi na kutengwa ambazo mara nyingi huja wakati wa matatizo. Huenda umewahi kupatwa na hisia hizi, na maelezo haya yanakusaidia kuelewa uzoefu wako vizuri zaidi. Au mistari hii inaweza kukusaidia kuelewa hisia za wengine ambao wanateseka.

Unaposoma Zaburi 102:12–28; 103116, tafuta virai ambavyo vinakupa kujiamini kwamba unaweza “kulitangaza jina la Bwana” katika majaribu yako (Zaburi 116:13). Unaweza kutaka kuwekea alama, kukariri, au kushiriki na wengine virai vinavyokupa tumaini katika Yeye.

Ona pia Isaya 25:8; 2 Wakorintho 1:3–7; Waebrania 2:17–18; Alma 7:11–13; Evan A. Schmutz, “Mungu Atapangusa Machozi Yote,” Liahona, Nov. 2016, 116–18.

Picha
Yesu akiponya

Uponyaji, na J. Kirk Richards

Zaburi 110118

Zaburi inaweza kunielekeza kwa Mwokozi.

Zaburi imejumuisha vifungu vinavyoelekeza kwenye maisha na huduma ya Yesu Kristo. Hapa kuna mifano michache:

Ni kweli zipi mistari hii inakufundisha kuhusu Yesu Kristo? Ni kwa jinsi gani kujua kweli hizi kunakubariki?

Unaposoma Zaburi wiki hii, endelea kuandika vifungu vingine ambavyo hukufundisha kuhusu Mwokozi. Unaweza pia kusoma au kusikiliza baadhi ya nyimbo za kanisa uzipendazo ambazo hukusaidia kufikiria kumhusu Yeye.

Zaburi 119

Neno la Mungu litaniweka daima katika njia Yake.

Zaburi hii imejumuisha virai vingi ambavyo hulinganisha maisha yetu na safari ya kurudi kwa Baba yetu wa Mbinguni. Unaposoma, angalia maneno kama tembea, njia, namna, nyayo, na tangatanga. Tafakari safari ya maisha yako—pale ulipokuwa, pale ulipo sasa, na njia ipi unaelekea. Je, unajifunza nini kutoka kwenye zaburi hii kuhusu safari yako ya kurudi nyumbani? Kulingana na zaburi hii, Mungu ametoa nini kukusaidia wewe kubaki katika njia sahihi?

Ungeweza kupendelea kujua kwamba katika Kiebrania asili, mistari minane ya mwanzo katika Zaburi 119 inaanza na herufi ya kwanza katika alfabeti ya Kiebrania. Mistari minane inayofuatia inaanza na herufi inayofuata, na kuendelea mpaka mwisho wa alfabeti.

Ona pia Isaya 42:16; 2 Nefi 31:17–21; Alma 7:19–20.

Zaburi 134–36

Bwana ni mwenye nguvu sana kuliko sanamu yoyote.

Angalia sababu zilizotolewa katika Zaburi 135:15–18 kuhusu kwa nini ni ujinga kuamini katika miungu ya uongo. Je, unaweza kujaribiwa kuamini nini ambacho ni sawa na miungu iliyooelezwa katika mistari hii?

Unaweza kutengeneza orodha ya mambo makuu yenye nguvu ambayo Bwana anaweza kufanya, kama ilivyoelezwa katika Zaburi 134–36. Je, ni mambo gani makuu yenye nguvu Yeye aliyokutendea?

Zaburi 146–50

“Mhimidini Bwana.”

Unaposoma zaburi hizi za mwisho za sifa, fikiria kuhusu sababu ulizonazo za kumsifu Bwana. Kwa nini ni muhimu kumsifu Yeye? Ni njia zipi unazoweza kumsifu Yeye?

Picha
ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Zaburi 119:105.Pengine familia yako ingeweza kutengeneza njia na kutembea juu yake katika giza, wakitumia mwanga kuangaza njia mbele. Mnapotembea, mngeweza kujiuliza swali kama “Ni nini katika maisha yetu ni kama giza hili?” au “ Ni kwa namna gani neno la Mungu ni kama mwanga?” Kuimba wimbo unaohusiana na mwanga wa Mungu, kama vile “Teach Me to Walk in the Light” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 177), kunaweza kukusaidia kusisitiza kanuni inayofundishwa katika Zaburi 119:105.

Zaburi 127–28.Inamaanisha nini kwa Bwana kutusaidia sisi “kujenga nyumba [yetu]”? (Zaburi 127:1). Ni kwa jinsi gani tunaweza kumhusisha Yeye vizuri zaidi katika jitihada zetu za kutengeneza nyumba ya haki? Ili kuisaidia familia yako kujibu swali hili, unaweza kuchora picha ya nyumba katika kipande cha karatasi na kuikata katika vipande vya fumbo. Nyuma ya kila kipande, wanafamilia wanaweza kuandika au kuchora njia za kumfanya Bwana kuwa sehemu ya nyumba yenu. Kisha mngeweza kuweka fumbo pamoja. Ni kipi kingine tunachokipata katika zaburi hizi ambacho hutupa msukumo kutembea katika njia za Bwana?

Zaburi 139.Baada ya kusoma mistari 1–4, wanafamilia wangeweza kuzungumza kuhusu jinsi gani wameweza kujua kwamba Mungu anawajua kibinafsi (ona pia mistari 14–15, 23–24).

Zaburi 146–50.Unaweza kuwaalika familia yako kusoma mistari michache ya Zaburi 146–50 kwa sauti, wakijaribu kuwasilisha hisia za mwandishi. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuelezea sifa zetu kwa Bwana? Wanafamilia wanaweza kufurahia kuandika zaburi zao wenyewe za sifa na kuzishiriki kati yao wenyewe.

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “Teach Me to Walk in the Light,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 177.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tumia rekodi za kusikiliza. Unapowafundisha familia yako, fikiria kusikiliza kutoka katika toleo la kusikiliza la maandiko, linalopatikana kwenye ChurchofJesusChrist.org au katika programu ya Maktaba ya Injili. Kusikiliza zaburi kunaweza kimsingi kuwa na nguvu kwa sababu ilidhamiriwa kukaririwa kwa sauti.

Picha
njia kwenye msitu

“Uniendeshe katika mapito ya maagizo yako, Kwa maana nimependezwa nayo” (Zaburi 119:35).

Chapisha