Agano la Kale 2022
Agosti 15–21. Zaburi 49–51; 61–66; 69–72; 77–78; 85–86: “Nami Nitayatangaza Aliyonitendea Roho Yangu”


“Agosti 15–21. Zaburi 49–51; 61–66; 69–72; 77–78; 85–86: ‘Nami Nitayatangaza Aliyonitendea Roho Yangu’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano la Kale 2022 (2021)

“Agosti 15–21. Zaburi 49–51; 61–66; 69–72; 77–78; 85–86,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2022

Picha
Yesu ameshikilia taa

Kuokoa Kile Kilichokuwa Kimepotea, na Michael T. Malm

Agosti 15–21

Zaburi 49–51; 61–66; 69–72; 77–78; 85–86

“Nami Nitayatangaza Aliyonitendea Roho Yangu”

Mfano wako kama mwanafunzi wa injili unaweza kuwa na ushawishi wenye nguvu kwa watoto. Shiriki nao uzoefu wako wa kiroho wa kujifunza injili.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Shiriki na watoto mstari kutoka katika zaburi, wimbo wa Kanisa, au wimbo wa watoto ambao unakusaidia kuhisi upendo wa Mwokozi. Mpe kila mtoto nafasi ya kufanya vivyo hivyo.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Zaburi 51:10

Wakati ninapofanya uchaguzi usio sahihi, Yesu Kristo anaweza kunisaidia kubadilika.

Wasaidie watoto kuelewa kwamba makosa ni sehemu ya maisha ya duniani na kwamba tunaweza kupokea msaada wa kuyashinda kutoka kwa Yesu Kristo.

Shughuli Yamkini

  • Shiriki hadithi ya kawaida, kutoka katika maisha yako au kutoka katika majarida ya Friend au Liahona, kuhusu mtoto ambaye alifanya uchaguzi usio sahihi lakini alipokea msaada wa kuwa bora kutoka kwa Mwokozi (kwa mfano, ona video “The Shiny Bicycle” kwenye ChurchofJesusChrist.org). Soma Zaburi 51:10, na shiriki furaha unayohisi wakati Mwokozi anapokusaidia kuwa na “moyo mweupe” na “roho safi.”

  • Waonyeshe watoto ukurasa wa shughuli ya wiki hii. Onyesha kila picha, na uwaombe watoto waelezee kile wanachokiona. Soma maelezo mafupi yahusuyo picha ili kuwasaidia watoto kujifunza kuhusu toba na msamaha.

Zaburi 71:8

Ninaweza kuwaelezea wengine kuhusu Yesu Kristo.

Maneno yaliyojaa imani ya mtoto yana nguvu za kipekee za kugusa mioyo. Wafanye watoto wajiamini kwamba ushuhuda wao wa Yesu Kristo unaweza kuwasaidia wengine.

Picha
wavulana wawili wameketi pamoja kwenye kiti.

Tunaweza kuzungumza na wengine kuhusu kile Yesu Kristo amefanya kwa ajili yetu.

Shughuli Yamkini

  • Wasomee watoto Zaburi 71:8, na chora mdomo mkubwa ubaoni. Waombe wakusaidie “kujaza” mdomo huo na vitu tunavyoweza kuwaambia wengine kuhusu Yesu Kristo.

  • Pitisha picha ya Yesu Kristo. Waombe watoto wachukue zamu ya kushikilia picha na kusema kitu kimoja wanachojua kuhusu Yeye. Je, ni nini Yeye amefanya kwa ajili yetu sisi? (Picha katika Kitabu cha Sanaa ya Injili zinaweza kuwapa mawazo fulani.)

Zaburi 86:7

Baba wa Mbinguni husikia na kujibu maombi yangu.

Nyingi za zaburi ni kama maombi kwa Mungu kwa ajili ya msaada, mwongozo au ulinzi. Fikiria jinsi unavyoweza kuwasaidia watoto kujenga imani yao kwamba Baba wa Mbinguni huwasikia na kuwajibu wanapoomba.

Shughuli Yamkini

  • Waulize watoto jinsi wanaongea na watu wanaoishi mbali nao sana. Waonyeshe vitu tunavyoweza kutumia kuwasiliana, kama vile simu au barua. Wasomee Zaburi 86:7. Ni kwa jinsi gani tunaweza “kuliita jina” la Baba wa Mbinguni? Je, Yeye hujibu kwa namna gani?

  • Waalike watoto waigize vitu ambavyo huvifanya kila siku, kama vile kuamka, kula kifungua kinywa, kuondoka kwenda shule au kwenda kulala. Wasaidie kutafuta muda wakati wa mchana ambapo wanaweza kuomba kwa Baba wa Mbinguni. Shuhudia kwamba tunaweza kumwomba Yeye wakati wowote, na Yeye atatusikia daima.

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu sala, kama vile “A Child’s Prayer” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 12–13). Simulia kuhusu wakati ambapo Mungu alijibu maombi yako.

Zaburi 77:11

“Nitakumbuka kazi za Bwana.”

Maandiko yanaweza kujenga imani yetu katika Yesu Kristo kwa kutusaidia kukumbuka “maajabu Yake ya kale.”

Shughuli Yamkini

  • Wasomee watoto Zaburi 77:11, na uwaambie jinsi unavyojaribu “kukumbuka kazi za Bwana,” ikijumuisha kazi Zake katika maisha yako. Waalike watoto wachore picha za kuwasaidia kukumbuka mambo makuu Aliyoyafanya.

  • Onyesha picha kutoka katika kitabu hiki au kutoka katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia kuwakumbusha watoto hadithi walizojifunza katika Agano la Kale kuhusu mambo makuu ambayo Bwana ameyafanya kwa ajili ya watu Wake. Waulize ni ipi kati ya hizi hadithi wanaipenda sana na kwa nini.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Zaburi 51

Toba ni mabadiliko ya moyo.

Zaburi 51 ina kweli kadhaa kuhusu toba. Ni kwa jinsi gani utawasaidia watoto kugundua kweli hizi?

Shughuli Yamkini

  • Mpangie kila mtoto asome mojawapo wa marejeleo ya maandiko yanayopatikana kwenye ukurasa wa shughuli ya wiki hii. Waombe watafute maneno ambayo yanawafundisha kitu fulani kuhusu toba. Waache waandike maneno hayo ubaoni. Baada ya kila mtu kushiriki, waombe watoto waseme jinsi wangeweza kumjibu rafiki anayeuliza, “Inamaanisha nini kutubu?”

  • Chora moyo ubaoni. Waombe watoto wataje baadhi ya dhambi ambazo Shetani anatujaribu sisi tutende. Andika dhambi hizo ndani ya moyo. Waombe watoto watafute neno moyo katika Zaburi 51:10, 17. Je, mistari hii inatufundisha nini kuhusu toba? (ona pia mstari wa 6). Wasaidie watoto kuelewa kwamba hata kama tunaacha kutenda dhambi, mioyo yetu inahitaji kubadilika ili sisi tutubu. Waombe watoto wafute dhambi zilizo ndani ya moyo ubaoni na waandike maneno mapya ambayo yanaelezea mabadiliko katika mioyo yetu tunapotubu. Shiriki ushuhuda wako kwamba Mungu anaweza “kuumba ndani [yetu] moyo safi” tunapotubu (mstari wa 10).

Zaburi 66:16; 77:11; 78:7

“Nitakumbuka kazi za Bwana.”

Waisraeli waliwafunza watoto wao kuhusu miujiza ambayo Mungu aliwatendea ili kwamba watoto “waweke tumaini lao kwa Mungu” (Zaburi 78:7).

Shughuli Yamkini

  • Waombe watoto washiriki nawe baadhi ya hadithi zao wanazozipenda kutoka katika maandiko (picha kutoka kwenye Kitabu cha Sanaa ya Injili zinaweza kuwasaidia kufikiria hadithi hizo). Kwa nini wanapenda hadithi hizi? Ni nini hadithi hizi zinatufundisha kuhusu Bwana? Someni pamoja Zaburi 77:11; 78:7. Kwa nini ni muhimu “kukumbuka kazi za Bwana”?

  • Waombe watoto wasome Zaburi 66:16 na wafikirie kuhusu au waandike majibu ya swali “Ni nini Bwana aliyonitendea roho yangu?” Kisha waache washiriki majibu yao, kama watapenda. Tunaweza kufanya nini ili “daima tukumbuke” (Moroni 4:3; 5:2) kile Bwana amefanya kwa ajili yetu?

Zaburi 86:5, 13, 15.

Bwana anataka kusamehe.

Tunapotenda dhambi, Shetani anataka tufikirie kwamba Bwana kamwe hatatusamehe. Wasaidie watoto kujenga imani yao kwamba Bwana “yu tayari kusamehe, na mwingi wa fadhili” (Zaburi 86:5).

Shughuli Yamkini

  • Onyesha picha ya Mwokozi (kama ile iliyoko katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia), na waulize watoto ni maneno gani wanaweza kutumia kumwelezea Mwokozi. Waalike watoto watafute maneno ambayo yanamwelezea Mwokozi katika Zaburi 86:5, 13, 15. Kama inahitajika, wasaidie kutoa maana za maneno haya. Je, tunaweza kusema nini kwa rafiki ambaye anahisi kwamba Mungu anakasirishwa nao wanapotenda dhambi?

  • Imba pamoja na watoto wimbo ambao unahisi utawasaidia kuelewa asili ya Mwokozi ya kusamehe, kama vile “I Stand All Amazed” (Nyimbo za Kanisa, na.193). Shiriki ushuhuda wako kwamba Yesu Kristo anataka kutusamehe.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Mwalike kila mtoto kutaja sababu moja ya kumpenda Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Wahimize washiriki sababu hiyo na mtu fulani nyumbani. Shuhudia kwamba maneno yao yatambariki mtu huyo.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Onyesha kujiamini. “Ikiwa [watoto] watahisi kwamba unawaamini, kujiamini kwao katika uwezo wao mtakatifu utakua. … Kwa upendo wajulishe kwamba unajua wanaweza kuwajibika kwa mafunzo yao wenyewe” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 28).

Chapisha