Agano la Kale 2022
Juni 20–26. 2 Samweli 5–7; 11–12; 1 Wafalme 3; 8; 11: “Ufalme Wako Utathibitishwa Milele”


“Juni 20–26. 2 Samweli 5–7; 11–12; 1 Wafalme 3; 8; 11: ‘Ufalme Wako Utathibitishwa Milele,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano la Kale 2022 (2021)

“Juni 20–26. 2 Samweli 5–7; 11–12; 1 Wafalme 3; 8; 11,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2022

Picha
Mfalme Daudi ameketi kwenye kiti cha enzi

Mfalme Daudi Akitawazwa Kuwa Mfalme, na Jerry Miles Harston

Juni 20–26

2 Samweli 5–7; 11–12; 1 Wafalme 3; 8; 11

“Ufalme Wako Utathibitishwa Milele”

Unaposoma maandiko, Roho Mtakatifu anaweza kukupatia misukumo na kukuongoza kujua kile chenye maana zaidi kwa watoto unaowafundisha.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waombe watoto wachache wazungumze kuhusu uzoefu wao wa kusoma maandiko (kibinafsi, pamoja na familia, au kanisani). Ni lini na wapi wanaposoma maandiko? Je, wanahisi vipi wanaposoma maandiko? Ni baraka gani ambazo wanapokea kwa kutii amri hii?

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

2 Samweli 5:19, 23

Kama ninahitaji mwongozo, ninaweza kumuomba Baba wa Mbinguni.

Mistari hii inaelezea jinsi Daudi alivyoomba kwa ajili ya mwongozo na maelekezo kama mfalme wa Israeli. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwatia moyo watoto kumgeukia Bwana katika maombi wanapokuwa na mahitaji?

Shughuli Yamkini

  • Waeleze watoto kwamba wakati Daudi alihitaji msaada, “aliuliza,” au aliomba, kwa ajili ya majibu. Unaposoma 2 Samweli 5:19, 23, waalike watoto wasikilize neno “aliuliza” na wakunje mikono yao wanapolisikia. Shuhudia kwamba daima tunaweza kuomba kwa Baba wa Mbinguni tunapohitaji msaada.

  • Ili kuwasaidia watoto kufikiria kuhusu kile wanachoweza kusema wanapoomba, ungeweza kuwauliza jinsi ambavyo wangekamilisha sentensi hizi: “Sisi tunakushukuru Wewe kwa ajili ya …” na “Tunakuomba Wewe kwa ajili ya …” Waache watoto wachore picha ya vitu ambavyo wangeweza kushukuru kwavyo au kuviomba katika maombi.

    Picha
    msichana akiomba

    Tunaweza kumuomba Baba wa Mbinguni msaada na mwongozo.

  • Waambie watoto kuhusu wakati ambapo uliomba msaada kwa Baba wa Mbinguni. Ni kwa jinsi gani Yeye alijibu maombi yako? Ilileta tofauti gani kwa Yeye kukusaidia? Waalike watoto kushiriki uzoefu wao.

2 Samweli 7:16

Yesu Kristo ni Mfalme wetu.

Wakati Daudi alikuwa mfalme wa Israeli, Bwana alimwambia kwamba “Ufalme Wake Utathibitishwa Milele” (2 Samweli 7:16). Ahadi hii ilimrejea Yesu Kristo, Mfalme wetu wa Milele, ambaye alizaliwa kupitia uzao wa Daudi.

Shughuli Yamkini

  • Mwalike mmojawapo wa watoto ajifanye kuwa mfalme au malkia. Kama inawezekana, mpe kila mtoto vitu vya kishika. Mfalme au malkia ni nani? Wanafanya nini? Waambie watoto kwamba Daudi alikuwa mfalme, na yeye alikuwa babu wa Yesu Kristo, ambaye tunamwita “Mfalme wa wafalme” (Ufunuo 19:16). Wasaidie watoto kufikiria njia tunazoweza kuonyesha kwamba tunaamini Yesu kuwa Mfalme wetu wa Milele.

  • Watoto wanapokamilisha ukurasa wa shughuli wa wiki hii, imbeni au chezeni nyimbo ambazo zinamrejea Kristo kama Mfalme wetu, kama vile “He Died That We Might Live Again,” “Called to Serve,” “Rejoice, the Lord Is King!” au “I Believe in Christ” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 65, 174–75; Nyimbo, na. 66, 134). Waombe watoto wasikilize neno “mfalme” na wanyanyue picha ya Yesu Kristo wanapolisikia. Je, tunahisi vipi wakati tunapoimba kuhusu Yesu?

1 Wafalme 8:57–58

Ninaweza kutembea katika njia za Mungu.

Kwa Waisraeli, kujenga na kuweka wakfu hekalu ilikuwa nafasi ya kugeuza mioyo yao kwa Bwana na kuweka dhamira ya “kutembea katika njia zake zote” (1 Wafalme 8:58). Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha “kutembea katika njia zake zote?

Shughuli Yamkini

  • Waoneshe watoto picha ya hekalu la kisasa na hekalu ambalo Sulemani alijenga (ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia). Elezea kwamba wakati Sulemani alipojenga hekalu kwa ajili ya Waisraeli, aliwahimiza “watembee katika njia zote [za Bwana] ” (1 Wafalme 8:58). Waambie watoto jinsi hekalu hukusaidia kutembea katika njia za Bwana. Waalike watoto washiriki jinsi wanavyohisi kuhusu hekalu. Imba pamoja na watoto wimbo kuhusu hekalu, kama vile “I Love to See the Temple” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 95).

  • Wape baadhi ya watoto mioyo ya karatasi na watoto wengine nyayo za karatasi. Soma 1 Wafalme 8:58, na uwaombe watoto wanyanyue mioyo mnaposema neno “tembea katika njia zake zote.” Wasaidie watoto kuelewa kwamba tunatembea katika njia za Bwana wakati tunamfuata Yesu na kujaribu kuwa kama Yeye. Waulize watoto nini wanachofanya kutembea katika njia za Mwokozi. Mngeweza kuimba wimbo kuhusu kumfuata Yesu, kama vile “I’m Trying to Be like Jesus” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 78–79).

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

2 Samweli 7:16–17

Yesu Kristo ni Mfalme wetu.

Wafalme tunaosoma kuwahusu katika Agano la Kale wote walikuwa na dosari na walifanya makosa—hata wale waliokuwa wazuri. Lakini Mfalme aliyetabiriwa kutoka katika ukoo wa Daudi, Yesu Kristo, ni mkamilifu na atatawala milele.

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto wasome kile nabii Nathani alimwambia Mfalme Daudi katika 2 Samweli 7:16–17, na uwaulize nini wanafikiria huu unabii ungemaanisha. Ni kwa jinsi gani ufalme wa Daudi haungekuwa na mwisho? Wasaidie watoto kutafuta na kusoma vifungu vya maandiko ambavyo vinafundisha kwamba Yesu Kristo, wa ukoo wa Daudi, ni Mfalme, kama vile Luka 1:32–33; Yohana 18:33–37; and Ufunuo 19:16. Ni kwa njia gani Yesu Kristo ni kama mfalme? Je, ni baadhi ya njia zipi ambazo tunaweza kuonyesha kwamba Yesu Kristo ni Mfalme wetu wa Milele?

  • Imba pamoja na watoto baadhi ya nyimbo ambazo zinamrejea Kristo kama Mfalme wetu, kama vile “Come, O Thou King of Kings,” “Rejoice, the Lord Is King!” au “Jesus, Once of Humble Birth” (Nyimbo, na. 59, 66, 196). Nyimbo hizi zinatufundisha nini kuhusu kile inachomaanisha kuwa na Yesu Kristo kama Mfalme wetu?

2 Samweli 11

Ninaweza kushinda majaribu.

Watoto unaowafundisha hufanya maamuzi madogo lakini muhimu kila siku. Unawezaje kuwasaidia waelewe umuhimu wa kuchagua kile kilicho sahihi hata wakati ni vigumu?

Shughuli Yamkini

  • Pitia 2 Samweli 11 pamoja na watoto, ukitaja wazi chaguzi ambazo Daudi alifanya. Waulize watoto ni chaguzi zipi nzuri Daudi alipaswa kuzifanya. Ni nini baadhi ya vitu tunavyoweza kufanya tunapokuwa tunajaribiwa ambavyo vinaweza kutusaidia kuchagua kile kilicho sahihi?

  • Ili kushiriki mfano wa mtu ambaye, kinyume na Daudi, aliepuka majaribu, na uwaulize watoto kama wanakumbuka hadithi ya Yusufu na mke wa Potifa (ona Mwanzo 39:7–12). Unaweza kupitia upya hadithi hii pamoja na watoto na kuwasaidia kuilinganisha na hadithi ya Daudi. Je, tunaweza kujifunza nini kutoka kwa hadithi ya Daudi na ya Yusufu kuhusu jinsi ya kuepuka majaribu?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Wasaidie watoto kufikiri juu ya kitu wanachoweza kufanya ili kutumia kile walichojifunza leo. Kisha watie moyo kutenda juu ya mipango yao.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Fuatilia Mialiko ya Kutenda. Unapowaalika watoto kutenda katika kile wanachojifunza, fuatilia katika mwaliko wako wakati wa darasa lijalo. Hii inawaonyesha watoto kuwa unajali kuhusu jinsi gani injili inabariki maisha yao. Wanaposhiriki uzoefu wao, wataimarishwa na watasaidiana kuishi injili.

Chapisha