“Juni 6–12. Ruthu; 1 Samweli 1–3: ‘Moyo Wangu Wamshangilia Bwana,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano la Kale 2022 (2021)
“Juni 6–12. Ruthu; 1 Samweli 1–3,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2022
Juni 6–12
Ruthu; 1 Samweli 1–3
“Moyo Wangu Wamshangilia Bwana”
Unaposoma Ruthu and 1 Samweli 1–3, muombe Baba wa Mbinguni jinsi unavyoweza kuwasaidia watoto kujifunza ukweli uliomo katika sura hizi. Andika misukumo unayopokea.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Waombe watoto washiriki kile wanachokijua kuhusu Ruthu, Naomi, Hana, au Samweli. Inaweza pia kuwa msaada kuonyesha picha, kama zile zilizo katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo
Ruthu
Ninaweza kuonyesha upendo na ukarimu kwa wale wanaonizunguka.
Wakati mume wa Ruthu alipofariki, Ruthu angeweza kuishi katika nchi yake ya kuzaliwa, lakini alichagua kwenda na mama mkwe wake mjane, Naomi, na kumtunza. Fikiria jinsi mfano wa upendo kama Kristo wa Ruthu ungeweza kuwatia moyo watoto unaowafundisha kuwa wakarimu kwa wale wanaowazunguka.
Shughuli Yamkini
-
Waalike watoto kumwakilisha Naomi, Ruthu, Boazi, au wahusika wengine unaposimulia hadithi zao kutoka katika kitabu cha Ruthu (ona pia “Ruthu na Naomi” katika Hadithi za Agano la Kale). Waalike watoto wainue mikono yao kila mara wanaposikia kitendo cha ukarimu katika hadithi. Tunajisikiaje wakati watu ni wakarimu kwetu? Tunajisikiaje wakati sisi ni wakarimu kwa wengine?
-
Imbeni pamoja wimbo kuhusu kuwa mkarimu, kama vile “Kindness Begins with Me” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 145). Wasaidie watoto kufikiria njia wanazoweza kuwa wakarimu kwa familia zao na marafiki zao. Kama wanahitaji msaada, waonyeshe wao picha za watu wakionyesha ukarimu. Kwa kila wazo lililotajwa, waache watoto wachore moyo ubaoni.
Baba wa Mbinguni husikia na kujibu maombi yangu.
Wakati Hana alikuwa na huzuni kwa sababu hangeweza kupata watoto, alimgeukia Bwana kwa imani na Yeye alijibu maombi yake. Wasaidie watoto kuona kwamba wanaweza siku zote kuomba kwa Baba wa Mbinguni hasa wanapokuwa na huzuni.
Shughuli Yamkini
-
Kwa maneno yako mwenyewe, waambie watoto kwa nini Hana alikuwa na huzuni (ona 1 Samweli 1:2–8., ona pia “Hana” katika Hadithi za Agano la Kale). Tunaweza kufanya nini tunapokuwa na huzuni? Wasomee watoto 1 Samweli 1:10, na uwaombe watoto wasikilize kile ambacho Hana alifanya. Waulize watoto jinsi walivyohisi wakati wanapoomba. Soma kutoka mstari wa 18 ili kuelezea kwamba baada ya maombi yake, Hana “hakuwa na huzuni tena.”
-
Tumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii kuwafundisha watoto kwamba wanaweza kuomba kwa Baba wa Mbinguni. Na Yeye atawasaidia. Wakati watoto wanapopaka rangi, wakiimba, au wakicheza wimbo uliorekodiwa ambao unafunza kuhusu maombi, kama vile “A Child’s Prayer” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 12–13).
Bwana amenifanyia mambo mengi ya ajabu.
Hana alionyesha shukrani zake kwa Bwana kwa shairi zuri la sifa. Mfano wake unaweza kuwasaidia watoto kufikiria kuhusu vitu vingi wanavyoweza kumshukuru Baba wa Mbinguni kwavyo.
Shughuli Yamkini
-
Wasomee watoto baadhi ya kile Hana alichosema baada ya Bwana kumbariki na mwana (ona 1 Samweli 2:1–2). Shiriki na watoto baraka ambayo umepokea kutoka kwa Bwana na jinsi ilikufanya uhisi. Kisha waalike watoto kuzungumza kuhusu baraka ambazo Bwana amewapa. Je, tunawezaje kuonyesha shukrani zetu Kwake?
-
Imbeni wimbo pamoja ambao unaelezea baadhi ya baraka ambazo Bwana ametupatia, kama vile “My Heavenly Father Loves Me” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 228–29). Waalike watoto wachore picha za baraka ambazo wamepokea kutoka kwa Bwana.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa
Ruthu
Ninaweza kuwa na imani katika Bwana.
Ruthu alifanya dhabihu za kuwa mwaminifu kwa Bwana na kubakia mwaminifu kwa Naomi. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kujifunza kutoka kwa vitendo vya Ruthu?
Shughuli Yamkini
-
Onesha picha ya Ruthu na Naomi (ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia). Kisha andika vichwa vya habari vitatu ubaoni: Majaribu, Vitendo, Baraka. Waalike watoto wasome Ruthu 1:3–5, 8, 16; 2:1–3, 8–12; 4:13–17, na waandike chini ya vichwa kile wanachopata kwenye mistari hii. Je, Ruthu alionyesha vipi imani yake katika Bwana? Shiriki mfano wa jinsi ulivyobarikiwa kwa sababu una imani katika Yesu Kristo, na uwaache watoto washiriki uzoefu wao wenyewe.
-
Imbeni pamoja wimbo kuhusu imani, kama vile “The Lord Is My Light” (Nyimbo za Kanisa, na. 89) au “Faith” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 96-97). Ni nini wimbo huu unatufundisha kuhusu kumwamini Bwana? Je, kwa jinsi gani tunaweza kuwa na imani katika Yesu Kristo hata katika wakati wa magumu.
Baba wa Mbinguni husikia na hujibu maombi yangu.
Wakati Hana “alikuwa na uchungu moyoni mwake,” alimgeukia Baba wa Mbinguni katika maombi (1 Samweli 1:10). Unawezaje kuwatia moyo watoto unaowafundisha kufanya vivyo hivyo?
Shughuli Yamkini
-
Ili kuwasaidia watoto kujifunza kuhusu Hana kutoka katika 1 Samweli 1, mpe kila mtoto mistari michache ya kusoma kutoka katika sura hii (au onyesha video “Hannah’s Faith,” ChurchofJesusChrist.org). Baadaye, rusha mpira au kitu kidogo kwa mtoto mmoja na umwalike yeye asimulie sehemu ya hadithi hiyo kabla ya kupitisha mpira kwa mtoto mwingine ili asimulie sehemu nyingine ya hadithi hiyo. Wakati hadithi imemalizika, waombe watoto washiriki jambo fulani ambalo wamejifunza kutoka kwenye mfano wa Hana.
-
Someni pamoja 1 Samweli 1:15, na mjadili inamaanisha nini kuzimimina nafsi zetu mbele ya Bwana. Pamoja na watoto, tengenezeni orodha ya vitu ambavyo tunaweza kuzungumza kuvihusu na Mungu wakati tunapoomba. Imbeni pamoja wimbo kuhusu sala, kama vile “A Child’s Prayer” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 12–13). Shuhudia juu ya upendo wa Mungu kwa watoto Wake na shauku Yake ya kusikia na kujibu maombi yao.
-
Waombe watoto kuorodhesha (kila mmoja pekee au katika makundi) mifano ya watu katika maandiko ambao waliomba kwa Baba wa Mbinguni. (Kama wanahitaji msaada, unaweza kuwaelekeza kwenye Luka 22:41–43; Enoshi 1:2–6; Joseph Smith—Historia ya 1:14–17.) Waombe washiriki kile wanachojifunza kutoka katika hadithi hizi.
Ninaweza kusikia na kutii sauti ya Bwana.
Wakati Samweli alipokuwa kijana mdogo, alisikia sauti ya Bwana lakini hakuitambua hapo mwanzo. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kusikia na kutenda juu ya misukumo wanayoipokea?
Shughuli Yamkini
-
Mwalike mtoto mmoja kujifanya kuwa Samweli na mtoto mwingine ajifanye kuwa Eli, unaposimulia hadithi katika 1 Samweli 3:1–10 (au onyesha video “Samweli na Eli,” ChurchofJesusChrist.org). Tunaweza kujifunza nini kutoka kwa Samweli kuhusu jinsi ya kusikia sauti ya Bwana? Je, ni kwa jinsi gani tunaonyesha kwamba tuko radhi kumsikia Bwana anaposema nasi?
-
Waalike watoto kufikiria juu ya jinsi ambavyo wangemwelezea mtu jinsi Bwana anavyosema nao. Waalike watafute majibu katika moja au zaidi ya maandiko yafuatayo: Mafundisho na Maagano 6:22–23; 8:2–3; 9:7–9.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Wahimize watoto wafikirie juu ya mtu au kitu wanachoweza kuomba kukihusu wiki hii. Wape nafasi siku zijazo kushiriki jinsi Baba wa Mbinguni alivyojibu maombi yao.