Agano la Kale 2022
Juni 6–12. Ruthu; 1 Samweli 1–3: “Moyo Wangu Wamshangilia Bwana”


“Juni 6-12. Ruthu; 1 Samweli 1–3: ‘Moyo Wangu Wamshangilia Bwana,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano la Kale 2022 (2021)

“Juni 6-12. Ruthu; 1 Samweli 1–3,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Famila: 2022

Picha
Ruthu na Naomi

Wewe Uendako, na Sandy Freckleton Gagon

Juni 6–12

Ruthu; 1 Samweli 1–3

“Moyo Wangu Wamshangilia Bwana”

Unapojifunza maisha ya Ruthu, Naomi, Hana, na wengine wiki hii, msikilize kwa ukaribu Roho na andika misukumo yoyote unayopata. Je, unashawishika kufanya nini?

Andika Misukumo Yako

Wakati mwingine tunawaza kwamba maisha yetu lazima yafuate njia iliyo wazi kuanzia mwanzo hadi mwisho. Umbali mfupi kati ya nukta moja hadi nyingine ni mstari ulionyooka, pamoja na yote. Na bado maisha yamejaa vikwazo vingi na njia ya mzunguko ambayo hutupeleka katika mwelekeo tusiotarajia. Tunaweza kukuta kwamba maisha yetu ni tofauti kabisa na vile tulivyofikiria yangekuwa.

Ruthu na Hana hakika walilijua hili. Ruthu hakuwa Mwisraeli, ila aliolewa na mmoja wao, na wakati mume wake alpofariki, alikuwa na uchaguzi wa kufanya. Je, angerudi kwenye familia yake na maisha yake ya awali, maisha aliyozoea, au angekumbatia imani ya Waisraeli na familia mpya pamoja na mama mkwe wake? (ona Ruthu 1:4–18). Mpango wa Hana wa maisha yake ulikuwa ni kuzaa watoto, na kutoweza kufanya hivyo kulimwacha yeye “katika maumivu ya moyo” (ona 1 Samweli 1:1–10). Unaposoma kuhusu Ruthu na Hana, fikiria imani wanayoweza kuwa walikuwa nayo ili kuweka maisha yao kwenye mikono ya Bwana na kusafiri katika njia zao wasizotarajia. Kisha unaweza kufikiria safari yako mwenyewe. Itaonekana tofauti na ya Ruthu na Hana—na yeyote yule. Lakini kipindi chote cha majaribu na mshangao kati ya hapa na takdiri yako ya milele, unaweza kujifunza kusema pamoja na Hana, “Moyo Wangu Wamshangilia Bwana” (1 Samweli 2:1).

Kwa ajili ya muhtasari wa vitabu vya Ruthu na 1 Samweli, ona “Ruthu” na “Samweli, vitabu vya” katika Kamusi ya Biblia.

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Ruthu

Kristo anaweza kugeuza majanga kuwa ushindi.

Wakati mume wa Ruthu alipofariki, majanga yalikuwa na matokeo kwake kiasi kwamba yalikuwa makali zaidi kuliko yale mjane wa leo angeweza kukabiliana nayo. Katika utamaduni wa Kiisraeli kwa wakati huo, mwanamke asiye na mume au watoto hakuwa na haki ya kumiliki mali na hakuwa na njia ya kujipatia kipato. Unaposoma hadithi ya Ruthu, gundua jinsi Bwana alivyobadili majanga kuwa baraka kuu. Unagundua nini kuhusu Ruthu ambacho kingeweza kumsaidia? Nini ulikuwa wajibu wa Boazi katika kumkomboa Ruthu kutoka kwenye hali yake ya kukata tamaa? (ona Ruthu 4:4–7). Ni sifa zipi kama za Kristo unaziona kwa wote Ruthu na Boazi?

Ruthu; 1 Samweli 1

Ninaweza kuamini kwamba Mungu anaweza kunilinda na kunisaidia bila kujali hali yangu.

Je, naweza kujiona katika hadithi ya Ruthu, Naomi, na Hana? Labda umeumia sana kwa kupoteza, kama Ruthu na Naomi (ona Ruthu 1:1–5). Au kama, Hana, unasubiria baraka ambazo bado hujazipata (ona 1 Samweli 1:1–10). Tafakari ni jumbe zipi unaweza kujifunza kutokana na mifano ya hawa wanawake waaminifu. Je, ni kwa jinsi gani Ruthu na Hana walionyesha kwamba walikuwa na imani katika Mungu? Je! Ni baraka gani walipokea? Je! unawezaje kufuata mifano yao? Zingatia jinsi ambavyo “umekuja kumtumainia” Bwana (Ruthu 2:12) hata wakati maisha yanapoonekana magumu.

Ona pia Reyna I. Aburto, “Katika Mawingu na Jua, Bwana, Kaa Nami!Liahona, Nov. 2019, 57–60.

Picha
Hana na Samweli

Kwa ajili ya Mtoto huyu Nilisali, na Elspeth Young

1 Samweli 2:1–10

Moyo wangu unaweza kushangilia katika Bwana.

Baada ya Hana kumchukua Samweli mdogo hekaluni, alizungumza maneno mazuri kumsifu Bwana, yaliyoandikwa katika 1 Samweli 2:1–10. Maneno haya ni ya kugusa sana wakati unapofikiria kwamba muda mfupi kabla, “alikuwa na uchungu rohoni, … na akalia sana.” (1 Samweli 1:10). Unapojifunza mistari hii, ni jumbe zipi unapata ambazo zinaongeza hisia zako za sifa na shukrani kwa Bwana? Labda wimbo wa Hana utakupa msukumo kutafuta njia ya ubunifu ya kuelezea shukrani zako kwa Bwana—wimbo, mchoro, kitendo cha kuhudumia, au chochote kile kinachowasilisha hisia zako kuelekea Kwake.

Ndio, si sala zote za dhati zinajibiwa kama za Hana. Unapata nini katika ujumbe wa Rais Dieter F. Uchtdorf “Shukrani katika Hali Yoyote” ambacho kinaweza kukusaidia wewe wakati sala zako hazijibiwi katika njia unayotumainia? (Liahona, Mei 2014, 70–77).

1 Samweli 3

Ninaweza kusikia na kutii sauti ya Bwana.

Kama sisi wote, Samweli alipaswa kujifunza namna ya kutambua sauti ya Bwana. Wakati unaposoma 1 Samweli 3, unajifunza nini kutoka kwa mvulana huyu mdogo kuhusu kusikia na kutii sauti ya Bwana? Je, ni uzoefu upi umekuwa nao kuhusu kusikia sauti Yake? Ni fursa zipi unazo, kama Eli, kuwasaidia wengine kutambua wakati Bwana anapozungumza nao? (ona 1 Samweli 3:7).

Ona pia Yohana 14:14–21; David P. Homer, “Kusikia Sauti Yake,” Liahona, Nov. 2019, 41–43.

Picha
ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Ruthu 1:16–18; 2:5–8, 11–12.Familia yako ingeweza kutafuta mifano ya huruma na utiifu katika mistari hii. Tunawezaje kuonyesha ukarimu kwa familia yetu na kwa wengine na utiifu kwa Yesu Kristo? Sura, “Ruthu na Naomi” (katika Hadithi za Agano la Kale) zingeweza kusaidia familia yako kujifunza kutoka kwenye mfano wa Ruthu.

1 Samweli 1:15.Labda ungeweza kumimina kitu chochote kutoka kwenye chombo ili kuwasaidia wanafamilia kuona kile Hana alichomaanisha aliposema, “Mimi … nimeimimina roho yangu mbele za Bwana.” Kwa nini hii ni nija nzuri ya kuelezea namna gani sala zetu zinapaswa kuwa? Je, tunaweza kuboresha vipi sala zetu binafisi na za familia?

1 Samweli 2:1–10.Shairi la Hana la kumsifu Bwana linaweza kukuongoza wewe kufikiria nyimbo ambazo unatumia kumsifu Bwana. Mngeweza kuimba baadhi ya hizi nyimbo pamoja. Wanafamilia wako pia wanaweza kufikiria njia nyingine za kuelezea hisia zao kwa Yesu Kristo. Kwa mfano, wanaweza kuchora picha zinazoonyesha kwa nini wanampenda Mwokozi.

1 Samweli 3:1–11.Inaweza kuwa ya kuburudisha kuigiza hadithi ya Bwana akimwita Samweli, au familia yako inaweza kutazama video “Samuel and Eli” (ChurchofJesusChrist.org). Wanafamilia wanaweza kuzungumza kuhusu nyakati walipohisi Bwana akizungumza nao na jinsi walivyotenda juu ya maneno Yake.

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “There Is Sunshine in My Soul Today,” Nyimbo za Kanisa, na. 227.

Kuboresha Kujifunza Kibinafsi

Mruhusu Roho aongoze kujifunza kwako. Omba kwamba Roho Mtakatifu akuongoze kwenye mambo unayohitaji kujifunza. Kuwa makini kwa minong’ono Yake, hata kama hii itakupelekea kusoma kuhusu mada ambayo hukuitarajia au kujifunza katika njia tofauti.

Picha
mvulana Samweli katika hema

Kielelezo cha Samweli akimsikia Bwana, na Sam Lawlor

Chapisha