Agano la Kale 2022
Juni 13–19. 1 Samweli 8–10; 13; 15–18: “Vita ni Vya Bwana”


“Juni 13–19. 1 Samweli 8–10; 13; 15–18: ‘Vita ni Vya Bwana,’” Njoo, Unifuate —Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano la Kale 2022 (2021)

“Juni 13–19. 1 Samweli 8–10; 13; 15–18,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2022

Picha
Kijana Daudi na kombeo

Daudi na Goliathi, na Steve Nethercott

Juni 13–19

1 Samweli 8–10; 13; 15–18

“Vita ni Vya Bwana”

Mapendekezo katika muhtasari huu yanaweza kukusaidia kutambua baadhi ya kanuni muhimu zaidi katika sura hizi. Unaweza kupata kanuni zingine unaposoma.

Andika Misukumo Yako

Tangu makabila ya Israeli yalipofanya makazi katika nchi ya ahadi, Wafilisi walikuwa tishio endelevu kwa usalama wao. Mara nyingi nyakati za nyuma, Bwana alikua amewaokoa Waisraeli kutoka kwa maadui zao. Ila kwa sasa wazee wa Israeli walidai, “Tunataka kuwa na mfalme … [ili] atoke mbele yetu na kutupigia vita vyetu” (1 Samweli 8:19–20). Bwana akakata tamaa, na Sauli alipakwa mafuta kuwa Mfalme. Na bado wakati tishio kubwa Goliathi akitupa changamoto zake kwa jeshi la Waisraeli, Sauli—kama wengine kwenye jeshi lake—“aliogopa sana” (1 Samweli 17:11). Katika siku hiyo, si mfalme Sauli aliyewaokoa Waisraeli, bali kijana mpole mchungaji aliyeitwa Daudi, ambaye hakuvaa vazi la vita lakini alikuwa amevaa imani isiyopenyeka katika Bwana. Mapigano haya yalithibitisha kwa Israeli, na kwa yeyote ambaye ana vita ya kiroho, kwamba “Bwana haokoi kwa upanga na mkuki” na kwamba “vita ni vya Bwana” (1 Samweli 17:47).

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

1 Samweli 8

Yesu Kristo ni Mfalme wangu

Unaposoma 1 Samweli 8, angalia namna gani Bwana alivyohisi kuhusu tamanio la Waisraeli kwa ajili ya mfalme zaidi ya Yeye mwenyewe. Inamaanisha nini kumchagua Bwana “kuwa mfalme juu [yako]” ? (1 1 Samweli 8:7. Unaweza kufikiria pia njia ambazo unajaribiwa kufuata mienendo isiyo ya haki ya ulimwengu badala ya kumfuata Bwana. Ni kwa jinsi gani unaweza kuonyesha kwamba unataka Yesu Kristo kuwa Mfalme wako wa Milele?

Ona pia Waamuzi 8:22–23; Mosia 29:1–36; Neil L. Andersen, “Kuushinda Ulimwengu,” Liahona, Mei 2017, 58–62.

1 Samweli 9:15–17; 10:1–12; 16:1–13

Mungu huwaita watu kutumikia katika ufalme Wake kwa njia ya unabii.

Mungu aliwachagua Sauli na Daudi kuwa wafalme kupitia unabii na maono (ona 1 Samweli 9:15–17; 10:1–12; 16:1–13). Hivi pia ndivyo Anavyowaita wanaume na wanawake kutumikia katika Kanisa Lake leo. Unajifunza nini kutoka katika maelezo haya kuhusu kile inachomaanisha “kuitwa na Mungu, kwa unabii”? (Makala ya Imani 1:5. Ni baraka zipi zinapatikana kutokana na kuitwa na kusimikwa na watumishi wa Bwana wenye mamlaka?

Picha
Samweli akimpaka mafuta Sauli

Kielelezo cha Samweli akimpaka Sauli mafuta,© Lifeway Collection/licensed from goodsalt.com

1 Samweli 13:5–14; 15

“Kutii ni bora zaidi kuliko dhabihu.”

Ingawa Sauli alikuwa mrefu kimaumbile, alihisi “mdogo machoni [pake] mwenyewe” wakati alipokuwa mfalme (1 Samweli 15:17). Ingawa, kadiri alivyobarikiwa kwa mafanikio, alianza kujiamini zaidi na kumwamini Bwana kidogo. Ni ushahidi gani unauona juu ya hili katika 1 Samweli 13:5–14; 15? Kama ungekuwa na Sauli nyakati hizo, nini ungeweza kumwambia ambacho kingemsaidia kushinda “uasi” wake na “ukaidi”? (1 Samweli 15:23).

Ona pia 2 Nefi 9:28–29; Helamani 12:4–5; Mafundisho na Maagano 121:39–40; Thomas S. Monson, “Tafakari Njia za Miguu Yako,” Liahona, Nov. 2014, 86–88.

1 Samweli 16:7

“Bwana huutazama moyo.”

Ni baadhi ya njia gani ambazo watu huwahukumu wengine “kwa mwonekano wa nje”? Inamaanisha nini kutazama “kwenye moyo,” kama Bwana afanyavyo? (1 Samweli 16:7. Fikiria jinsi unavyoweza kutumia kanuni hii kwenye jinsi unavyowatazama wengine—na wewe mwenyewe. Ni jinsi gani kufanya hivyo kunaweza kuathiri mwingiliano wako au mahusiano yako na wengine?

1 Samweli 17

Kwa msaada wa Bwana, naweza kushinda changamoto yoyote.

Unaposoma 1 Samweli 17, tafakari maneno ya watu mbalimbali katika sura hii (ona orodha hapo chini) Maneno yao yanaonyesha nini kuhusu wao? Ni kwa jinsi gani maneno ya Daudi yanaonyesha ujasiri na imani yake kwa Bwana?

Tafakari vita yako binafsi unayokabiliana nayo. Unaweza kupata nini katika 1 Samweli 17 kinachoimarisha imani yako kwamba Bwana anaweza kukusaidia?

Ona pia Gordon B. Hinckley, “Kumshinda Goliathi katika Maisha Yetu,” Ensign, Mei 1983, 46, 51–52.

Picha
ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

1 Samweli 9:15–21; 16:7.Kusoma mistari hii sambamba na maneno kutoka kwa Mzee Dieter F. Uchtdorf kungeweza kuchochea mjadala kuhusu kwa nini Bwana alimchagua Sauli na Daudi: “ikiwa tutajiangalia wenyewe kupitia macho yetu ya kimwili, tunaweza tusijione wenyewe kama wazuri vya kutosha. Lakini Baba wa Mbinguni anatuona kama tulivyo hasa, na vile tunavyoweza kuwa” (“Inafanya kwa kushangaza!Liahona, Nov. 2015, 23. Labda wanafamilia wanaweza kufanya zamu kuzungumza kuhusu sifa zipi nzuri wanaziona katika moyo wa kila mmoja (ona 1 Samweli 16:7).

1 Samweli 10:6–12.Lini tumemwona Mungu akimbariki mtu kwa nguvu za kiroho ili kutimiza kazi au wito kama alivyombariki Sauli? Ni uzoefu gani tunaweza kushiriki wakati “Mungu alipotupa [sisi] moyo mwingine” au “Roho ya Mungu ikatujilia [sisi]” katika huduma Yake? (mistari 9–10).

1 Samweli 17:20–54.Familia yako inaweza kufurahia kusoma kwa pamoja hadithi ya Daudi na Goliathi (“Daudi na Goliathi” katika Hadithi za Agano la Kale ingeweza kusaidia) au kutazama video “The Lord Will Deliver Me” (ChurchofJesusChrist.org). Hii inaweza kuongoza kwenye majadiliano kuhusu changamoto tunazokabiliana nazo ambazo zinaweza kuwa kama “Goliathi” kwetu. Ungeweza hata kuandika baadhi ya hizi changamoto kwenye shabaha au mchoro wa Goliathi na kufanya zamu kurusha vitu (kama mpira wa karatasi) kwenye shabaha au mchoro.

Inaweza pia kuwa ya kuvutiwa kusoma kuhusu vazi la vita na silaha alizokuwa nazo Goliathi (ona mistari 4–7). Daudi alikuwa na nini? (ona mistari 38–40, 45–47). Bwana ametoa nini kutusaidia kuwashinda Goliathi wetu?

1 Samweli 18:1–4.Ni kwa jinsi gani Daudi na Yonathani walikuwa marafiki wazuri? Ni kwa jinsi gani marafiki wazuri wametubariki? Tunaweza kufanya nini kuwa marafiki wazuri—ikijumuisha kwa wanafamilia wetu?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa “I Will Be Valiant,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto,162.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Toa ushuhuda wako kila mara. “Ushuhuda wako rahisi, wa dhati wa ukweli wa kiroho unaweza kuwa na ushawishi wenye nguvu kwa [familia yako]. Ushuhuda unakuwa na nguvu zaidi unapokuwa wa moja kwa moja na wa kutoka moyoni. Hauhitajiki kuwa wa maelezo mengi au mrefu” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 11).

Picha
Daudi

Kielelezo cha Daudi, na Dilleen Marsh

Chapisha