“Juni 13–19. 1 Samweli 8–10; 13; 15–18: ‘Vita ni Vya Bwana,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano la Kale 2022 (2021)
“Juni 13–19. 1 Samweli 8–10; 13; 15–18,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2022
Juni 13–19
1 Samweli 8–10; 13; 15–18
“Vita ni Vya Bwana”
Ingawa shughuli hapo chini zimepangwa kwa ajili ya watoto wadogo au wakubwa, unaweza kutohoa yoyote kati yake kukidhi mahitaji ya wale unaowafundisha.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Onyesha picha ya Daudi na Goliathi kutoka katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia. Waalike watoto washiriki kile wanachojua juu ya hadithi hii, na uwaulize maswali ili kuwasaidia kukumbuka sehemu za hadithi ambazo waliziacha.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo
Bwana anajua kile kilicho katika moyo wangu.
Kushiriki hadithi ya jinsi Bwana alivyomwambia Samweli amchague Daudi kama mfalme kunaweza kuwasaidia watoto kujua kwamba Bwana anatujua kibinafsi.
Shughuli Yamkini
-
Shiriki jinsi Bwana alivyomwambia Samweli kwamba Daudi angekuwa mfalme wa Israeli (ona 1 Samweli 16:1–13). Unaposimulia hadithi, unaweza kumuacha mtoto mmoja kumwakilisha Samweli. Yeye anaweza kumpa taji la karatasi mtoto mwingine, anayemwakilisha Daudi. Shiriki ushuhuda wako kwamba Bwana alijua moyo wa Daudi na kwamba Yeye anamjua kila mmoja wetu.
-
Shiriki uzoefu ambapo wewe ulihisi Bwana anakufahamu wewe. Imbeni pamoja wimbo ambao unafundisha kwamba Mwokozi anatujua na anatupenda, kama vile “Jesus Is Our Loving Friend” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 58).
Imani katika Yesu Kristo inaweza kunisaidia kuwa na ujasiri.
Watoto wanaweza kuelewa kwa urahisi kijana Daudi kwa sababu hata ingawa Daudi alikuwa mdogo, alishinda changamoto kubwa. Wasaidie kuona kwamba chanzo cha ujasiri wake na nguvu zake kilikuwa imani yake katika Yesu Kristo.
Shughuli Yamkini
-
Rejelea pamoja na watoto hadithi ya Daudi na Goliathi (ona “Daudi na Goliathi” katika Hadithi za Agano la Kale), na waache wachukue zamu kuigiza sehemu za hadithi. Mshawishi mtoto kuwa Goliathi aseme, “Nipeni mtu tupigane ” (1 Samweli 17:10). Mshawishi mtoto akijifanya kuwa Daudi aseme, “Mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana” (1 Samweli 17:45). Shuhudia kwamba wakati sisi tunapokuwa na imani katika Bwana, Yeye atatusaidia kuwa na ujasiri kama alivyokuwa Daudi.
-
Tumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii kuonyesha jinsi Goliathi alivyokuwa mrefu kulinganishwa na mvulana mdogo kama Daudi. Elezea kwamba jeshi la Israeli lilikuwa linamwogopa Goliathi. Waombe watoto wajifanye wanaogopa. Kisha onyesha picha ya Yesu Kristo, na uwaambie watoto kwamba kwa sababu Daudi alikuwa na imani katika Bwana, angekuwa na ujasiri. Waombe wasimame wima, kama vile wao ni jasiri.
-
Waalike watoto watembee kama vile wao ni Daudi akienda kupigana na Goliathi huko wakiimba wimbo kuhusu kuwa na ujasiri, kama vile “I Will Be Valiant” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,162).
Marafiki wazuri wanaweza kuwa baraka kwangu.
Urafiki wa Yonathani na Daudi ni mfano mkubwa wa baraka ambazo zinatokana na marafiki wazuri.
Shughuli Yamkini
-
Chora maumbo mawili ubaoni, moja kumwakilisha Daudi na lingine kumwakilisha Yonathani. Wasomee watoto vifungu vya maneno vichache kutoka katika 1 Samweli 18:1–4 ambavyo vinasisitiza upendo ambao hawa rafiki wawili walihisi kwa kila mmoja. Mpe kila mtoto kipande cha moyo wa karatasi, na uwaulize jinsi wanavyoweza kuonyesha upendo kwa rafiki. Baada ya kila mtoto kushiriki wazo, mwalike mtoto ashikishe moyo wa karatasi kwenye ubao.
-
Waambie watoto kuhusu rafiki mzuri ambaye hukusaidia kuishi injili au kujenga imani yako katika Yesu Kristo, na uwaalike watoto washiriki kuhusu yule anayewasaidia wao. Waalike watoto kuigiza wakifanya kitu kizuri kwa rafiki.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa
1 Samweli 8:6; 9:15–17; 10:1–24; 16:1–13
Wale wanaohudumu katika Kanisa wameitwa na Mungu.
Matukio ya Mungu akiwachagua Sauli na Daudi kuwa wafalme yanaweza kusaidia darasa lako kuelewa jinsi watu wanavyoitwa kutumikia katika Kanisa leo. Matukio haya yanaweza kujenga imani kwamba miito hutoka kwa Mungu kupitia watumishi wake walioidhinishwa.
Shughuli Yamkini
-
Kwenye vipande tofauti vya karatasi, andika kauli zifuatazo na maandiko: watu walikuwa wanataka mfalme (1 Samweli 8:6); Bwana alimwambia Samweli kwamba Sauli angekuwa mfalme (1 Samweli 9:15–17); Samweli alimpaka mafuta Sauli (1 Samweli 10:1); Samweli alimwasilisha Sauli kwa watu (1 Samweli 10:24). Waombe watoto wasome vifungu vya maandiko na kuviweka katika utaratibu sahihi.
-
Jifunzeni pamoja makala ya Imani ya tano. Kwa ufupi waambie watoto jinsi ulivyopokea wito wako kufundisha katika Msingi. Unajuaje kwamba wewe ulikuwa umeitwa na Mungu? Shuhudia kwamba Mungu huwatia msukumo viongozi kuwaita watu kutumikia.
“Bwana huutazama moyo.”
Ni kawaida kuwahukumu wengine kwa kutazama kile tunachoona, lakini sehemu ya kuwa zaidi kama Yesu ni kujifunza jinsi ya kuona vile Yeye anavyoona—kwa kutazama “moyo” (1 Samweli 16:7).
Shughuli Yamkini
-
Waalike watoto wafikirie kwamba waliombwa kumchagua mtu kuwa mfalme. Ni sifa gani wangetazama? Someni pamoja 1 Samweli 16:6–7 kutafuta kile Bwana alichomwambia Samweli alipokuwa akitafuta mfalme mpya wa Israeli. Tunajifunza nini kutokana na maelekezo ya Bwana?
-
Wasilisha somo linalofundishwa kwa vielelezo kuwaonesha watoto kwamba hukumu tunazozifanya kwa kutegemea “mwonekano wa nje” (mstari wa 7) zinaweze zisiwe sahihi. Kwa mfano, ungeweza kuwaonyesha baadhi ya chakula au kitabu chenye jalada ambalo haliendani na maudhui yake ya kweli. Ni nini 1 Samweli 16:7 na somo hili linalofundishwa kwa vielelezo linapendekeza kuhusu jinsi tunavyopaswa kujitazama na kuwatazama wengine?
-
Shiriki uzoefu ambao ulijifunza kwa nini unapaswa “kutazama moyo,” sio tu “mwonekano wa nje” (mstari wa 7). Waache watoto washiriki uzoefu wowote ambao wamekuwa nao. Imbeni wimbo ambao unasisitiza kanuni hii, kama vile “I’ll Walk with You” au “We Are Different” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 140–41, 263).
Yesu Kristo anaweza kunisaidia kushinda changamoto yoyote.
Watoto wanaweza kuwa wanakabiliwa na changamoto ambazo zinaonekana kuwa ngumu kama vile kushinda jitu kama Goliathi. Mfano wa Daudi unaweza kuwapa tumaini kwamba Bwana atawasaidia kipigana vita vyao.
Shughuli Yamkini
-
Wapangie watoto kuchora picha za sehemu tofauti za hadithi katika 1 Samweli 17:20–54. Tundika picha katika utaratibu ubaoni, na uwaalike watoto kushiriki hadithi kwa kuzungumza kuhusu kila picha walizochora. Bwana anataka sisi tujifunze nini kutoka kwenye hadithi hii?
-
Wasaidie watoto kutengeneza orodha ubaoni ya baadhi ya changamoto ngumu ambazo mtu anaweza kukabiliana nazo. Waalike watafute vitu ambavyo Daudi alisema ambavyo vinaweza kumtia moyo mtu anayekabiliana na changamoto kama hizo (ona 1 Samweli 17:26, 32, 34–37, 45–47). Waambie watoto jinsi Yesu Kristo alivyokusaidia wakati wa changamoto.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Waulize watoto swali kuhusu kitu walichojifunza leo. Andika hilo swali, mpe kila mtoto nakala kwenda nayo nyumbani na kujadili na familia yake.