Agano la Kale 2022
Juni 20–26. 2 Samweli 5–7; 11–12; 1 Wafalme 3; 8; 11: “Ufalme Wako Utathibitishwa Milele”


“Juni 20–26. 2 Samweli 5–7; 11–12; 1 Wafalme 3; 8; 11: ‘Ufalme Wako Utathibitishwa Milele,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano la Kale 2022 (2021)

“Juni 20–26. 2 Samweli 5–7; 11–12; 1 Wafalme 3; 8; 11,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafisi na Familia: 2022

Picha
Mfalme Daudi amekaa kwenye kiti cha ufalme

Mfalme Daudi Akitawazwa, na Jerry Miles Harston

Juni 20–26

2 Samweli 5–7; 11–12; 1 Wafalme 3; 8; 11

“Ufalme Wako Utathibitishwa Milele”

“Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki” (2 Timotheo 3:16).

Andika Misukumo Yako

Utawala wa Mfalme Daudi ulianza kwa ahadi nyingi. Imani yake isiyokuwa na shaka katika kumshinda Goliathi ilikuwa ni ya kishujaa. Kama Mfalme, aliifanya Yerusalemu kama mji wake mkuu na kuiunganisha Israeli (ona 2 Samweli 5). Ufalme haukuwahi kuwa na nguvu sana. Na bado Daudi alishindwa na jaribu na kupoteza nguvu zake za kiroho.

Utawala wa Sulemani mwana wa Daudi vile vile ulianza kwa ahadi nyingi. Hekima yake ya kiungu na ufahamu aliopokea vilikuwa urithi. Kama Mfalme, alipanua mipaka ya Israeli na kumjengea Bwana hekalu zuri sana. Ufalme haukuwahi kuwa na nguvu sana. Na bado Sulemani kwa ujinga aliruhusu moyo wake kugeukia miungu mingine.

Tunaweza kujifunza nini kutoka hadithi hizi za majonzi? Labda somo moja ni kwamba bila kujali uzoefu wetu wa zamani, nguvu zetu za kiroho hutegemea chaguzi tunazofanya leo. Tunaweza pia kuona katika maelezo haya kuwa si nguvu zetu wenyewe au hamasa au hekima ambayo itatuokoa sisi—ni ya Bwana. Hadithi hizi zinatuonyesha sisi kwamba tumaini la kweli la Israeli—na la kwetu—haliko kwa Daudi, Sulemani, au mfalme yeyote wa kimwili, bali kwa “mwana wa Daudi” mwingine: Yesu Kristo (Mathayo 1:1), Mfalme wa Milele ambaye “atasamehe dhambi za watu [Wake] kama sisi “tutamgeukia tena [Yeye]” (1 Wafalme 8:33–34).

Kwa muhtasari wa vitabu vya 2 Samweli na 1 Wafalme, ona “Samweli, vitabu vya” na “Wafalme, vitabu vya” katika Kamusi ya Biblia.

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

2 Samweli 5:17–25

Bwana anaweza kunipa mimi mwelekeo.

Mara Daudi alipoweza kuiunganisha Israeli (ona 2 Samweli 5:1–5), alipaswa kuwalinda watu wake kutoka kwa Wafilisti. Unaposoma 2 Samweli 5:17–25, fikiria jinsi mfano wa Daudi unavyoweza kukusaidia wewe katika changamoto unazokabiliana nazo (ona pia 1 Samweli 23:2, 10–11; 30:8; 2 Samweli 2:1). Ni kwa jinsi gani unatafuta mwongozo wa Bwana katika maisha yako? Ni kwa jinsi gani unabarikiwa kwa kutenda kufuatana na ufunuo unaopokea?

Ona pia 1 Wakolosai 12; Richard G. Scott, “Namna ya Kupata Ufunuo na Misukumo Kwa ajili ya Maisha Yako Binafsi,” Liahona, Mei 2012, 45–47.

2 Samweli 7

Ni “nyumba” ipi Bwana alimuahidi Daudi?

Wakati Daudi alipojitoa kujenga nyumba, kwa maana ya hekalu, kwa ajili ya Bwana (ona 2 Samweli 7:1–3), Bwana aliitikia kwamba kimsingi mwana wa Daudi angeijenga (ona mistari 12–15; ona pia 1 Mambo ya Nyakati 17:1–15). Bwana pia alisema kwamba Yeye badala yake angemjengea Daudi “nyumba,” akimaanisha vizazi vijavyo, na kwamba kiti chake cha enzi kitadumu milele (ona 2 Samweli 7:11, 16, 25–29; Zaburi 89:3–4, 35–37). Ahadi hii ilitimizwa katika Yesu Kristo, Mfalme wetu wa Milele, ambaye alikuwa ni wa uzao wa Daudi (ona Mathayo 1:1; Luka 1:32–33; Yohana 18:33–37).

2 Samweli 11; 12:1–14

Napaswa daima kuwa macho dhidi ya dhambi.

Uaminifu wa Daudi kwa Bwana katika siku za nyuma haukumfanya yeye kuwa na kinga dhidi ya majaribu wakati “alipotembea juu ya dari la nyumba” ya mfalme na “kumwona mwanamke akioga” (2 Samweli 11:2). Fikiria somo unaloweza kujifunza kutokana na uzoefu wake. Maswali kama haya yanaweza kukusaidia katika kujifunza tukio hili:

  • Ni chaguzi zipi Daudi alizifanya ambazo zilimwongoza chini kwenye njia ya ongezeko la dhambi? Ni chaguzi zipi za haki angeweza kufanya badala yake?

  • Ni kwa jinsi gani adui anajaribu kukuongoza katika njia za dhambi katika maisha yako? Ni chaguzi zipi ungeweza kufanya kurudi katika usalama?

Ona pia 2 Nefi 28:20–24; “To Look Upon” (video), ChurchofJesusChrist.org.

1 Wafalme 3:1–15

Karama ya utambuzi inanisaidia mimi kutofautisha mema na mabaya.

Ikiwa Bwana atakwambia, “Omba utakalo nikupe” (1 Wafalme 3:5), ni nini ungeomba? Ni nini kinachokupendeza kuhusu ombi la Sulemani? Tafakari kwa nini, “moyo wa adili” “kupambanua kati ya mema na mabaya” (mstari 9) ni karama ya thamani. Je, unaweza kufanya nini ili kutafuta karama hii?

Ona pia 2 Mambo ya Nyakati 1; Moroni 7:12–19; David A. Bednar, “Mwepesi Kutambua,” Ensign, Des. 2006, 30–36.

1 Wafalme 8:12– 61

Hekalu ni nyumba ya Bwana.

Kwa mamia ya miaka, uwepo wa Mungu uliwakilishwa na tabenako dogo ambalo Musa alijenga. Ingawa Daudi alitaka kumjengea Mungu nyumba ya kudumu ya kukaa, badala yake Mungu alimchagua Sulemani mwana wa Daudi kujenga hekalu la Bwana. Unaposoma sala ya Sulemani na maneno aliyotamka kwa watu wake wakati wa kukamilisha hekalu, gundua jinsi alivyojisikia kuhusu Bwana na nyumba Yake. Unaweza pia kutengeneza orodha ya baraka Sulemani alizoomba kwenye sala yake. Unagundua nini kuhusu baraka hizi? Ni kwa jinsi gani umebarikiwa na nyumba ya Bwana katika siku yetu?

Ona pia 2 Mambo ya Nyakati 6.

Picha
Hekalu la Barranquilla Colombia

Hekalu la Barranquilla Colombia

Picha
ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa Ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

2 Samweli 5:19, 23.Ni lini “tumemwomba Bwana” kwa ajili ya mwongozo na maelekezo? Ni kwa namna gani Yeye ametujibu?

2 Samweli 7:16.Bwana alipomwambia Daudi, “Ufalme Wako utathibitishwa milele,” Alikuwa akirejelea mfalme ajaye katika familia ya Daudi ambaye angetawala milele: Yesu Kristo. Labda familia yako ingeweza kufurahia kutengeneza mataji wakati mkijadili kwa nini mna shukrani kuwa Yesu Kristo ni Mfalme wenu wa Milele.

2 Samweli 11.Kusoma kuhusu dhambi za majonzi za Daudi kunaweza kuwa nafasi nzuri ya kujadili hatari za picha za ponografia, mawazo mabaya, na ukosefu wa maadili. Vyanzo vifuatavyo vinaweza kuwa vya msaada katika mjadala wenu: toleo la Oktoba 2019 la Liahona, nyenzo za Kanisa za kushughulia Ponografia (ChurchofJesusChrist.org/addressing-pornography), na video “What Should I Do When I See Pornography?” na “Watch Your Step” (ChurchofJesusChrist.org). Wanafamilia wangeweza kutengeneza mpango kuhusu nini wataweza kufanya wakati wanapokabiliana na ponografia.

1 Wafalme 11:9–11.Ni nini baadhi ya “miungu mingine” (mstari wa10) ambayo inaweza kugeuza mioyo yetu kutoka kwa Bwana? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuweka mioyo yetu ikilenga kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “More Holiness Give Me,” Nyimbo za Kanisa, na. 131.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Zingatia kanuni ambazo zitabariki familia yako. Unapojifunza neno la Mungu kwa sala jiulize, “Ni nini ninachopata hapa ambacho kitakuwa cha muhimu hasa kwa familia yangu?” (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 17).

Picha
Hekalu la Sulemani

Kielelezo cha hekalu la Sulemani, na Sam Lawlor

Chapisha